Usaili kwa wanaoomba kazi(Job Interview), ni mfumo muhimu unaotumiwa na waajiri kukutana na waomba kazi.
Waombaji wanatakiwa kujiandaa vizuri ili kuushinda mtihani huu, kwani ndio utakao amua uajiriwe au uachwe.
Hapa leo tuyatambue maswali 25 ambayo mara kwa mara huwa mara yanaulizwa:
1.TUAMBIE KUHUSU WEWE.
Kwa yeyote anayehudhuria usaili hili ndio huwa swali kuu la ufunguzi, kuwa makini usianze kupoteza dira hapa mwanzo.
Weka jibu lako katika muda wa dakika moja hadi mbili.
Kazia maeneo manne makuu: Miaka ya nyuma, elimu yako, historia yako ya kazi, na uzoefu wako wa kazi wa hivi karibuni.
Kazia zaidi hili la uzoefu wa karibuni.
Kumbuka hili ni swali la kukupasha moto tu lisije likakufanya upoteze hatua zako zote.
2.UNAFAHAMU NINI KUHUSU KAMPUNI YETU?:
Unatakiwa uwe na uwezo wa kuwaelezea kuhusu wao katika bidhaa au huduma,soko, sifa, muonekano, malengo ya kampuni,changamoto, mfumo wa uongozi, historia au hata falsafa yao.
Hapa usianze kuigiza kana kwamba unajua kila kitu. Jibu maswali yako katika mfumo utakaoonyesha kwamba ulifanya uchunguzi japo kidogo kuhusu wao, usijaribu kuwazuga wasairi, na weka wazi kwamba unataka kujifunza zaidi.
Unaweza ukaanza kwa kusema, "Katika kutafuta kwangu kazi niliangalia kampuni nyingi, lakini hii ya kwenu ilinivutia zaidi".
3.KWANINI UNATAKA KUFANYA KAZI NA SISI?
Hapa na kwingineko jibu zuri utalitoa kama ulifanya vizuri utafiti wako, kwani kinachotakiwa hapa ni jibu lako liendane na mahitaji ya kampuni yao.
Mathalani unaweza ukajibu kwamba, shughuli inayofanywa na hiyo kampuni unapenda sana kujihusisha nayo.
4.UNAWEZA UKAIFANYIA NINI KAMPUNI AMBACHO WENGINE HAWAWEZI?
Hapa ndio eneo lako la kumwaga mbwe mbwe zako, na jinsi gani una tofauti na wengine.
Elezea historia yako ya kufanikisha mambo kadhaa. Zungumzia kwamba ujuzi wako ukichanganya na historia hiyo vinakufanya uwe mtu wa pekee.
Taja uwezo wako wa kufanya shughuli kwa kuweka vipaumbele, kuainisha matatizo, na kutumia uzoefu wako kutatua.
5.KITU GANI KIMEKUVUTIA ZAIDI KATIKA HII NAFASI UNAYOOMBA NA KIPI HAKIVUTII?
Hapa usije kulogwa ukaelezea vitu vingi visivyovutia katika hiyo nafasi.
Jaribu kuorodhesha mambo matatu au manne yanayovutia katika hiyo nafasi na labda moja tu lisilovutia.
6.KWANINI TUKUAJIRI WEWE?
Hapa usiume maneno kabisa, bali jaribu kuwashawishi kwa kuwaelezea uwezo wako, uzoefu na hata nguvu yako wa kufanya kazi kwa bidii.
7.UNATARAJIA NINI KATIKA HII KAZI?
Weka jibu lako katika fursa zinazopatikana katika hiyo kampuni.
Elezea shauku yako ya kutaka kufanya kazi nzuri na kutambuliwa mchango wako na kampuni hiyo.
Weka maelezo yako katika mtazamo wa fursa zinazotolewa na kampuni husika na si kuhusu wewe zaidi.
8.HEBU NIPE TAFSIRI YA NAFASI YA KAZI UNAYOOMBA.
Hapa jibu kwa kifupi na elekeza zaidi katika utendaji kazi wa nafasi hiyo.
Jibu kwa kujikita zaidi katika majukumu na uwajibikaji wa hiyo nafasi unayoomba.
Hakikisha kabla hujaanza kujibu hili swali, unayajua majukumu ya kazi unayoomba, usianze kujing'ata ng'ata maelezo utaonekana hujui unachoomba.
Na ukiona hujui kuwa mkweli, na muombe msairi akutajie japo chache.
9.ITAKUCHUKUA MUDA GANI MPAKA MCHANGO WAKO UANZE KUONEKANA KATIKA KAMPUNI?
Hapa ndugu yangu jitahidi kuwa mkweli. Jaribu kuwaeleza kuwa utaanza kukutana na mahitaji ya kampuni tangu siku ile unaanza kazi,
lakini itakuchukua si chini ya nusu mwaka au mwaka mzima, kuielewa vizuri kampuni na hapo ndipo mchango wako utakapoonekana.
10.UTAKAA KWA MUDA GANI NA SISI(KAMPUNI)?
Eleza kuwa una maslahi na kazi hiyo pamoja na kampuni yenyewe.
Lakini unapaswa pia ukiri kuwa kutakuwa na changamoto nyingi za wewe kuendelea kubaki hapo kipindi cha utumishi wako.
HAYO NI MASWALI KUMI NA MENGINE YALIYOBAKI 15 TUTAENDELEA KUJUZANA ENDELEA KUTEMBELEA TU HII BLOG.
1 comments:
Unakaribishwa kutoa maoni juu ya hili...
Post a Comment