Pasipoti ni hati inayotolewa na serikali ya nchi kuthibitisha kwamba anayeimiliki ni raia wake kwa madhumuni ya kusafiria katika nchi za nje na ikiomba atambuliwe kama raia wake.
Serikali ya Tanzania inatoa aina tofauti tofauti za pasipoti kwa raia wake kutokana na sheria yake ya mwaka 2002 na utekelezaji wake wa mwaka 2004.

Chombo pekee kilichopewa mamlaka ya kusimamia zoezi la utoaji wa pasipoti ni Idara  ya Uhamiaji Tanzania chini ya kamishna mkuu wa uhamiaji.
Mpaka sasa Pasipoti zinapigwa chapa katika makao makuu ya ofisi za Idara ya uhamiaji Dar es salaam na Zanzibar.

Hebu sasa tuzitupie macho aina hizo tofauti za pasipoti zinazotolewa Tanzania:

1.PASIPOTI ZA KAWAIDA(ORDINARY PASSPORTS):
Pasipoti hii anaweza kupewa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya kusafiria nje ya Jamhuri ya Tanzania.

2.PASIPOTI ZA HUDUMA(SERVICE PASSPORTS):
Pasipoti hii hutolewa kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanya huduma za jamii.

3.PASIPOTI ZA KIDIPLOMASIA(DIPLOMATIC PASSPORTS):
Pasipoti hii hutolewa  kwa raia ambaye amepewa haki maalumu ya kupewa pasipoti hiyo na sheria ya mwaka 2002.

4.PASIPOTI ZA AFRIKA MASHARIKI(EAST AFRICAN PASSPORTS):
Pasipoti hii hutolewa kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye nia ya kusafiri katika nchi za umoja wa Afrika mashariki.

5.HATI YA KUSAFIRIA YA DHARURA(EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT):
Hati hii hutolewa kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ana safari ya dharura lakini hajakamilisha taratibu za kupata pasipoti.
Wakati mwengine hutolewa kwa raia anayetaka kusafiri nchi za nje na hawezi kupata pasipoti katika muda muafaka au anayerudishwa kwao kutoka nchi za nje.

6.CHETI CHA UTAMBULISHO(CERTIFICATE OF IDENTIFY):
Inaweza kutolewa hata kwa mtu asiye raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtu huyu ambaye hawezi kupata pasipoti kutoka katika nchi ambayo yeye ni raia au ambaye hana uraia wa nchi yoyote kwa madhumini ya kusafiri nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

7.HATI YA KUSAFIRIA YA MKUTANO WA GENEVA(GENEVA CONVECTION TRAVEL DOCUMENT):
Hati hii hutolewa kwa mkimbizi aliyepewa hifadhi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sasa hebu tuangalie vitu gani vinavyohitajika wakati wa kutuma maombi ya kuomba pasipoti ya Tanzania:

1.Cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo au cheti cha uasilia wa muombaji(Iwapo muombaji ana uraia wa kuzaliwa).

2.Cheti cha kuzaliwa cha mzazi au hati ya kiapo ya mzazi au cheti cha uasilia wa mzazi(Iwapo mzazi ana urai wa kuzaliwa).

3.Picha za pasipoti za hivi karibuni zinazokuonyesha vizuri na kama zitakavyoainishwa na mamlaka husika.

4.Kwa suala kama la muombaji kuwa chini ya umri wa maika 18, mzazi au mlezi ataandika makubaliano.

ZINGATIA:

Hati ya kiapo ya kuzaliwa ya muombaji inatakiwa iapwe na:
*Mzazi au mlezi wa kisheria;

*Mtu aliyeshuhudia kuzaliwa kwa muombaji wa pasipoti na ambaye anamzidi muombaji si chini ya miaka 5;

*Ndugu wa karibu wa muombaji ambaye alitaarifiwa kuzaliwa kwa muombaji na wazazi wake.

Kuna kipindi Kamishna mkuu wa uhamiaji anaweza akamtaka muombaji athibitishe uraia wa wazazi wake.
SASA UMESHAYAJUA MAHITAJI YA KUPATA PASIPOTI, JIPANGE NA TAARIFA HIZO ILI UNAPOHITAJI USIPATE USUMBUFU.


Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz