Hebu tujaribu kuondoa utata wa maana ya majina haya yanayofanana huduma lakini kimuundo na yanayopatikana ndani huwa ni tofauti.
CHUO(COLLEGE):
Kinatoa elimu na kuzawadia wahitimu shahada mbalimbali kwa kuegemea eneo moja tu la elimu. Mfano chuo cha biashara hutoa mafunzo yanayohusu biashara katika ujumla wake na haitagusa taaluma nyingine ya elimu zaidi ya biashara.
CHUO KIKUU(UNIVERSITY):
Kina mkusanyiko wa vyuo tofauti tofauti huku kila chuo kikiegemea eneo fulani la taaluma kwa jamii.
Mfano chuo kikuu cha Dar es salaam kina vyuo tofauti tofauti ndani yake vingine vikifundisha Ualimu, Biashara na hata Sayansi ya jamii.
TAASISI(INSTITUTE):
Ni chombo kinachotoa elimu ya ujuzi na inaweza pia kuwa sehemu ya chuo kikuu au taasisi nyingine za elimu ya juu na mara nyingi huwa ni mkusanyiko wa idara tofauti tofauti.


Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

3 comments:

Unknown

ahsanten sana kwa kazi nzuri sana kwasababu ni wengi tulishindwA KUTOFAUTISHA KATI YA HIVYO VITU.KEEP IT UP

Unknown

Hakika, ninashukuru kwa maelezo na mafundisho yenu, yamenifanya nijue mambo
ambayo kabla sikuyajua.
AHSANTENI SANA.

Anonymous

Asante sana 🙏🙏

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz