Kutoa pumzi mbaya ni tatizo linalowakabili watu wengi pasipo kujua chanzo ni nini.
Kila siku wanasafisha meno lakini bado harufu imegoma kuisha mdomoni wanapoongea au kupumua.

Leo tujaribu kujuzana japo kwa ufupi hali hiyo husababishwa na nini.
Tatizo hili kitaalamu huitwa Halitosis, huletwa na bakteria wanaotoa harufu mbaya kinywani.
Tunapokula chakula,mabaki mengi ya chakula hujificha katika uwazi kati ya jino na jino na mabaki mengine madogo sana hukusanywa katika ulimi.

Bakteria hawa wanapokaa kwa muda maeneo hayo ,huzalisha kampaundi ya salfa ambayo ndiyo chanzo kikuu cha harufu inayotoka mdomoni.

Na pia aina ya chakula kama kitunguu chenye mafuta ya garlic ambayo hufyonzwa katika mishipa ya damu na kupelekwa kwenye mapafu huzalisha harufu mbaya wakati wa kupumua na pia hata uvutaji wa sigara huchangia hili tatizo.
Hebu tuangalie njia chache tunazoweza kuzitumia ili kupunguza tatizo japo kidogo.
*Kusafisha kinywa(meno na ulimi) kila siku unapoamka kwa brashi nzuri na dawa ya meno ambayo ni salama.

*Unapomaliza kula piga mswaki, sukutua mdomo kwa maji mengi au chukua kipande cha uzi na pitisha katikati ya nafasi ya jino na jino ili kuondoa mabaki ya chakula.

*Kila mara hakikisha mdomo wako haukauki mate, kwani mdomo mkavu hutoa harufu mbaya. Hii ni kwasababu mate yana kemikali ambazo huua bakteria na pia husidia kumeng'enya mabaki ya chakula mdomoni.

*Tumia bazoka zisizo na sukari nyingi kuzalisha mate pale unapoona mdomo wako ni mkavu.

*Pia unaweza ukamuona Daktari wa magonjwa ya kinywa ili asaidie kugundua chanzo cha tatizo ili kutibu.

Basi sisi wenye hili tatizo tujitahidi kulimaliza.
Mwisho wa siku watu wako wa karibu, wanaweza wasikwambie kama kinywa chako kinatoa harufu lakini ukajikuta unatengwa pindi unapotaka kuwasiliana nao kwa karibu.
Maeneo kama shuleni na vyuoni ambako wanafunzi wengi huunda vikundi vya kujadiliana masomo utaona wewe unatengwa bila sababu za msingi na huleta hali ya kunyanyapaliwa.



Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz