Kujiamini, ni hali ya kujisikia hakuna kinachoweza kukuzuia,
kufanya unachotaka kufanya kwa mafanikio,
bila kuwa na hofu yoyote.
Mtazamo ulionao juu yako wewe,
una nguvu kubwa katika matokeo ya kitu chochote utakachofanya.
Mtazamo wako utaleta uhalisia wa ama ufanikiwe au ushindwe katika vitu unavyofanya.
Sasa tungalie vitu ambavyo vinaweza kukusaidia wewe kujenga kujiamini:
1.VAA VIZURI UPENDEZE:
Japo mavazi si yanayounda utu wako, lakini yanachangia kwa kiasi kikubwa namna unavyojisikia katika nafsi yako.
Hakuna mwenye hisia za karibu na nafsi yako kama wewe mwenyewe,
na unapojua wazi kwamba hujapendeza inaleta tofauti namna utakavyojichanganya na watu wengine.
Ukivaa vizuri na kupendeza utaifanya nafsi yako ijiamini hata kusimama mbele za watu na kufanya mambo ya msingi.
2.TEMBEA KWA KUJIAMINI:
Njia rahisi kabisa ya kujua kama mtu anajiamini au la ni ya kuangalia jinsi anavyotembea.
Je, anatembea taratibu sana, kwa uchovu, kwa maumivu au anatembea kwa kasi?
Watu wenye kujiamini huwa wanatembea kwa kasi;
kwasababu wanajua wana sehemu ya kwenda, kuna watu wa kukutana nao, na kazi za msingi za kufanya.
Yawezekana hauna haraka na eneo unaloenda lakini ongeza nguvu kidogo katika mwendo utaufanya ubongo ushughulike vizuri.
3.ANGALIA WATU MACHONI:
Mtu anayejiamini anapoongea na watu wengine hawezi kutoa macho yake
kwa anayeongea naye.
Kwasababu wanaipa umuhimu taarifa yoyote inayotoka kwa mwengine wakiamini kuna jambo la kujifunza,
na utamfanya anayekupa taarifa asilete masihara.
4.FANYA TENDO LA UPENDO:
Watu wanaojiamini mara nyingi wanaguswa na hali za watu wengine,
na siku zote wanajiona wana nafasi ya kuwa sehemu ya utatuzi wa mtatizo.
Ukifanya tendo lolote la kumuonyesha mwengine upendo litakufanya ujisikie vizuri na kujiamini.
5.SHUKURU:
Unapoweka akili yako yote katika vitu unavyotaka tu,
unatengeneza mazingira ya akili pia kuhisi unaweza ukavikosa.
Na hali hii itakufanya ufikirie sababu zitakazokufanya ushindwe.
Njia pekee ya kuondokana na tatizo kama hili ni kuelekeza fikra zako katika shukrani za uliyoyapata.
Unaweza ukakaa chini na kuorodhesha vitu vyote ambavyo umeweza kuvipata,
shukuru na jipongeze.
Shukuru kwa mafanikio uliyopata katika masomo, ujuzi, na mahusiano.
6.SIFIA WENGINE:
Kama una mtazamo hasi juu yako mwenyewe, kumsifia mwengine inakuwa ngumu.
Utabaki kusema umbea, na kuwasemea uongo wenzako.
Ili kuepuka jili ni heri uwe na tabia ya kuwasifia wenzako pale unapoona wamejitahidi kufanya jambo zuri.
Hii itawafanya unaowasifia kujisikia vizuri na wakupende,
na hapo ndio na wewe kujiamini kunajengeka zaidi.
Kwa kujali na kuunga mkono mazuri ya wenzako inakusaidia wewe pia mazuri yako yajitokeze.
7.KUWA MBELE:
Ukijijengea tabia ya kukaa nyuma kila sehemu kwa mfano darasani, ofisini, na katika mikusanyiko ya watu.
Hii inaonyesha kabisa huna cha maana kwako unachotaka kionekane kama mfano kwa wenzako.
8.CHANGIA WAZO MBELE ZA WATU:
Wengi wanasita kutoa maoni yao mbele za wengine eti kwa kuhofia
kuzungumza kitu cha ajabu na kuchekwa na wengine.
Unapoweka mkakati wa kuwa unachangia mawazo yako mbele za wenzako
itakujengea hali ya kuona una mchango kwa wengine.
9.MALIZA KAZI MPAKA MWISHO:
Raha ya kufanya kazi ni kuimaliza ikiwa kamili kama ilivyotakiwa,
hali ya kuwa umemaliza kazi kwa mafanikio itakufanya ujenge kujiamini sana.
Ukiwa unaacha viporo vya kazi kila siku utaanza kujenga hisia za kushindwa moyoni mwako.
10.SAIDIA WENGINE:
Mara nyingi tuunakuwa watu wa kufikiria namna ya kutatua shida zetu wenyewe,
lakini ukiwekeza muda wako katika kutatua shida za watu wengine
itasaidia kujenga kujiamini.
KUTOJIAMINI SI TABIA YA KUIFURAHIA KUWA NAYO KATIKA MAISHA YAKO.
KILA MARA UTAKUWA UNAPOTEZA NAFASI ZA KUFANIKIWA KWA KUENDEKEZA TABIA YA KUTOJIAMINI.
ANZA SASA KUFANYA MABADILIKO KATIKA MAISHA YAKO KWA KUJENGA KUJIAMINI NA UTAONA JINSI DUNIA ITAKAVYOFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO KWA AJILI YAKO.
1 comments:
Thank
Post a Comment