11.WASIFU WAKO UNAONYESHA NAFASI UNAYOOMBA NI YA CHINI KULIKO UWEZO ULIONAO. UNA MAONI GANI?
Hapa elezea kwamba nia yako ni kujenga mahusiano mazuri na kampuni yao na pia unatumaini uhodari wako utafungua fursa nyingine kwako.
Waambie kwamba kampuni kubwa kama yao inapaswa iwe na watu wenye uwezo mkubwa kama wako.
Na kwamba kwa kampuni kuwekeza kwako kutaifanya ipate ufanisi wa haraka katika utendaji wake.

12.MFUMO GANI WA UONGOZI UNAUPENDA?
Unatakiwa uwe unaufahamu vya kutosha mfumo wa uongozi unaotumiwa na kampuni yao, ili ule utakao utaja wewe uendane na wa kwao.

13.JE, WEWE NI KIONGOZI MZURI? UNAWEZA KUTUPATIA MFANO?
Hapa elezea zaidi mafanikio yako uliyoyapata wakati unaongoza na kazi ulizofanikiwa kuzifanikisha.

14.UTAKAPOPEWA NAFASI YA KUAJILI MTU UTAANGALIA NINI?
Waambie utaangalia ujuzi wake, juhudi na uwezo wake wa kushirikiana na wafanyakazi wengine.
Waambie kwamba utaajiri mtu ambaye anaonekana ataweza kuboresha utendaji kazi wa kampuni na kuipeleka hatua nyingine. 

15.ULISHAWAHI KUMFUKUZA MTU KAZI? NINI ILIKUWA SABABU NA ULIKABILIANA VIPI NA TUKIO HILO?

Kama uliwahi kiri kwamba haikuwa rahisi, na waambie kwamba ilisaidia kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi, kwa kuendeleza maelewano mazuri na wafanyakazi wengine.
Waambie kwamba unatumia mfumo wa kibinadamu kutatua tatizo kama hilo.


LEO NIMEWALETEA TENA HATUA HIZI TANO, NA ZITABAKI 10 AMBAZO ENDELEA KUFUATILIA BLOG HII ILI TUZIMALIZE ZOTE.







Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

1 comments:

frank Victor

Guys your welcome to comment on this...

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz