Matumizi ya kitu yanayozidi kiwango cha kawaida(Addiction) ni tabia ambayo siku hizi imekithiri katika jamii yetu.
Mtu anayekuwa mtuhumiwa wa tabia hii mara nyingi anakabiliwa na hali ya kuukimbia ukweli wa jambo linalotokea katika maisha yake na hivyo analikwepa kwa namna hiyo akihisi hawezi kulikabili.
Yawezekana mtuhumiwa wa tabia hii akatokea katika hali ya kuwa na kosa na anakwepa kuwajibika, msongo wa mawazo, tamaa, hofu, kutojikubali, kutojiamini, hasira, upweke hivyo kuchangia yeye kukosa furaha.
Hali hii umpelekea yeye kutafuta kitu mbadala kitakachoweza kuchukua nafasi ya kile anachokosa.
Hebu leo tujuzane vitu kumi vinavyoongoza kwa kutumiwa kuliko pitiliza katika jamii yetu.

1.POMBE(ALCOHOL):
*Mtu huyu analewa akihisi itamsaidia kukimbia tatizo linalomkabili, lakini pombe inapoisha anakumbana nalo tena na inambidi akanywe tena ili asahau.

2.UVUTAJI SIGARA(SMOKING):
*Tabia hii mara nyingi huanza katika rika la kubarehe ambapo kijana anataka aonekane mtu mzima ili asidharauliwe, asionekane mshamba na rafiki zake wanaovuta au alikuwa anajaribu tu aone ikoje baadaye kuacha anashindwa.

3.DAWA ZA KULEVYA(DRUGS):
*Sababu zake hazitofautiani sana na za mvutaji wa sigara anavyoanza lakini zina matokeo tofauti katika utumiaji.

4.UCHEZAJI KAMALI(GAMBLING):
*Wachezaji wengi wa kamali huanza kwa kuvutiwa kuona wengine wamepata pesa za haraka na hivyo na wao wakicheza wanaweza kupata.
Akianza kucheza hata akipata siku ya kwanza anahisi anaweza kupata zaidi, siku hadi siku anakuwa mzoefu  na anashindwa kuacha hadi afilisike kabisa kwani wengine huweka mali zao zote.

5.MEDIA ZA KIJAMII(SOCIAL MEDIA): 
*Tabia hii huanza kama jambo muhimu kuwasiliana na watu wanaokufahamu kwa muda fulani wa siku lakini baadaye unapoteza ratiba.
Utakutana na mtuhumiwa wa hili anaanza kuchati kutoka nyumbani anaendelea hadi akiingia katika usafiri na hata anapotembea njiani bado anaendelea kuchati na pengine hata akiwa kitandani anaendeleza.

6.MICHEZO YA VIDEO(VIDEO GAMES):
*Wengi wanaonasa katika mchezo huu hujikuta akili yote inahamia hapa kwani kila anapopata muda wa wazi shughuli kubwa huwa ni hii.
Wengi wao wanapata muda mchache sana wa kulala.

7.MTANDAO WA INTANETI(INTERNET):
*Hapa ndipo dunia kwa sasa imekamatwa, kwani binadamu  siku hizi tunatumia muda mwingi sana hapa.
Inachukua muda mwingi  wa watu kwa kuchati facebook na kuangalia  picha za ngono ambapo eneo hili limeshika vijana wengi na kuacha wanaona ngumu.

8.NGONO(SEX):
*Unaweza ukaanza na swali je, tuko wangapi?
Hapa watu wengi wanapoingia, kutoka inakuwa ngumu hasa kama alishaanza kujihusisha na wapenzi wengi.
Tabia inajijenga na kinachotokea baadaye ni kuona haiwezekani kuishi bila kushiriki tendo hilo na zaidi ya rafiki mmoja.

9.MANUNUZI(SHOPPING):
*Eneo hili limewashika zaidi jinsia ya kike kwani hufikia hatua kila siku lazima anunue kama ni nguo, vipodozi au hata mawigi. 
 Huwa anapoziona bidhaa hizo anashindwa kujizuia kuacha kununua hata ikibidi kukopa ili awe nayo.

10.KULA HOVYO(ROUGH EATING):
*Hapa sina la kuongeza!!!!!

Kwa hayo tuliyaona hapa juu hebu jichunguze kwa makini upo katika kipengele kipi ili uwaone wataalamu wakusaidie namna ya kuondokana nalo.
Huo si ugonjwa bali unahitaji kubadilisha tu tabia za aina fulani, na kwa msaada wa mtaalamu wa saikolojia utaweza kushinda kabla haijakuletea madhara makubwa.

UKIAMUA UNAWEZA KUTOKA KATIKA HIKI KIFUNGO:
USIJARIBU KUUFUNGUA HUU MNYORORO MWENYEWE, UTAKUUMIZA, SHIRIKISHA WATU UNAOWAAMINI. 







Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz