Kompyuta mawinguni ni mfumo unaomuwezesha mtumiaji wa huduma hii kuhifadhi taarifa zake katika mfumo wa digitali katika hifadhi  inayotolewa na kampuni atakayoomba.

Kuna kampuni mbali mbali zinazojihusisha na utoaji wa huduma hii kwa wateja wanaoomba.
Kampuni nyingi zina utaratibu wa kutoa hifadhi ndogo ya bure kama majaribio kwa wateja wanaoomba huduma yao. 


Mfumo huu unamfanya mtumiaji wa hii huduma aweze kutumia huduma za mfumo wa kompyuta bila kumiliki, kutunza, au kuhifadhi programu za kompyuta anachokuwa anamiliki yeye ni taarifa zake tu.

Wewe unayetaka kutumia hii huduma, ili ufanikiwe kuitumia mahali popote duniani ni lazima uwe una uwezo kufikia mawimbi ya intaneti.

Huu mfumo unaundwa na vitu vitatu vikuu ambavyo ni mtumiaji, mtandao wa intaneti, na kampuni inayotoa hiyo huduma.

1.MTUMIAJI:
Ni mtumiaji wa mwisho ambaye anataka kutumia taarifa zake katika vifaa vyake vyenye uwezo wa kupata mawimbi ya intaneti, na kuzivuta taarifa hizo kutoka katika kampuni iliyompatia hifadhi.

2.MTANDAO WA INTANETI:
Mtandao wa intaneti huwaunganisha mtumiaji na kampuni inayotoa huduma ya hifadhi za taarifa kwa mteja wake.

3.MTOA HUDUMA:
Ni kampuni zenye kompyuta zilizounganishwa kwa mtandao wa intaneti ambazo zinaruhusu kufikiwa  kwa programu,taarifa na hifadhi zake.
Endapo mteja atahitaji huduma ya hifadhi kubwa, kampuni humtoza kiasi cha pesa kulipia huduma hiyo.

Hebu tuyaorodheshe baadhi ya makampuni yanayotoa huduma ya kompyuta mawinguni, na kiasi cha hifadhi ya bure wanayotoa ili kwa anayehitaji ajiunge na kuanza kutumia haduma yao.


Google.....http://docs.google.com 5GB FREE
Drop Box.....http://dropbox.com 2GB FREE
Microsoft.....http://skydrive.com 7GB FREE
Apple.....http://iCloud.com 5GB FREE
Media Fire.....http://mediafire.com 50GB FREE
Sugar Sync.....http://sugarsync.com 5GB FREE
Ubuntu....http://ubuntu1.com 5GB FREE 

HUJACHELEWA KUTUMIA TEKNOLOJIA HII KWANI KAMPUNI HIZI ZIMEFUNGUA MILANGO KWA YEYOTE ANAYEHITAJI KUTUMIA HUDUMA ZAO.
ANZA SASA KUFAIDI MFUMO HUU.



Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz