Utume wa kidiplomasia(Diplomatic mission), ni ujumbe wa watu unaotumwa kutoka nchi moja kwenda kuweka makazi ya
kudumu katika nchi nyingine na kuwa muwakilishi pekee
wa nchi aliyotoka.
Ubalozi(Embassy), ndio jina linalotumika kuitwa makazi ya wawakilishi hao,
ambayo yanatakiwa yawe katika mji mkuu wa nchi hiyo iliyowapokea.
Makazi haya yanaongozwa na mtu anayeitwa balozi na eneo analofanyia kazi huyu kiongozi linaitwa kanseli na anapewa ulinzi na nchi iliyompokea.
Kuna mabalozi wengine wanalala hapo hapo katika kanseli na wengine
wanalala nje ya kanseli lakini bado hata kama halali hapo,
bado eneo analoenda kulala linapewa ulinzi na nchi iliyompokea.
Utume wowote wa umoja wa mataifa unaitwa utume wa kudumu(permanent mission)
katika nchi husika na utume wa nchi za jumuiya ya Ulaya huitwa
uwakilishi wa kudumu(permanent representation) zinaongozwa na muwakilishi
wa kudumu(permanent representative) na balozi.
Tume ya juu(High commission), ni jina linalopewa makazi ya wawakilishi wa nchi za jumuiya ya madola zikiongozwa na mtu anayeitwa kamishna.
Ubalozi mdogo(Consulate),hauna tofauti kubwa kiutendaji na
ubalozi mkubwa japo wenyewe unawekwa nje ya mji mkuu wa nchi husika.
Na wenyewe unajukumu la kushghulika na maslahi ya raia wao na
biashara wanazofanya kwa
ukaribu na unaongozwa na balozi mdogo.
Nchi moja yenye ubalozi
katika nchi fulani, inaweza ikawa na balozi
ndogo ndogo nyingi
katika miji tofauti ikiwa imeona raia wa nchi yake wapo wengi katika miji hiyo.
Ubalozi wa nchi yeyote unapewa kinga ya kutobanwa na sheria za mitaa iliyopo.
Na kutokana na agano la masuala ya kidiplomasia
lililoafikiwa Viennna na nchi zinazopokea mabalozi,
serikali ya nchi husika haziruhusiwi kuingia katika makazi ya ubalozi
mpaka wapokee ruhusa kutoka kwa nchi yenye ubalozi wake.
Na hii ndio nafasi pekee wanayoipata baadhi ya raia au wakimbizi
wanapotakiwa kukamatwa na mamlaka ya nchi hizo,
wakikimbilia ubalozini hawawezi kukatwa mpaka kwa ruhusa maalumu kutoka
katika nchi yake.
Nchi za jumuiya ya madola zina kawaida ya kushirikiana
shughuli za kibalozi,
kwani kama nchi mojawapo yenye uanachama wa jumuiya madola
ikiwa na ubalozi mahali utahusika kuhudumia pia raia wa nchi
nyingine za jumuiya ya madola ambazo hazina ubalozi katika nchi hiyo.
Nchi zilizopokeana mabalozi zinapogombana hatua ya kwanza kuonyesha
kwamba imechukizwa na
jambo lolote liliofanywa
na mmoja wao ni kumwita
balozi wake nyumbani mpaka watakapofikia muafaka.
Ubalozi una fanya kazi kama zifuatazo:
1.Raia wa nchi yake amepatwa na matatizo ya pasipoti, iwe imeibiwa au kupotea wanahusika kumsaidia namna ya kupata nyingine.
2.Kumsaidia raia wa nchi yake anayetaka kwenda nchi nyingine kupata viza.
3.Kuisaidia nchi yake katika nyanja ya uchumi kwa kuwakutanisha wafanyabishara wa nchi yake na wa nchi uliyopo ili kufungua fursa za kiuchumi.
4.Unakuwa kama mpeleka ujumbe wa taarifa kubwa kutoka kwa kiongozi wa nchini kwake kwenda kwa kiongozi wa nchi uliyopo.
Na endapo umepatwa na tatizo unataka kukamatwa sehemu pekee ambayo ukiwa tu ndani ya uzio wake
hakuna askari anayeruhusiwa kukukamata mpaka ruhusa itoke kwa
balozi ni ubalozini.
Ndio sehemu pekee ambayo inaweza kukupa hifadhi hata mwezi mzima
ili usikamatwe na pia unaweza
ukakutorosha na kukurudisha nchini kwako.
0 comments:
Post a Comment