UNAZIFAHAMU KAZI ZA BENKI KUU ZA NCHI(CENTRAL BANKS). JIELIMISHE HAPA KWA UFUPI.

Hii ni taasisi ya jamii inayosimamia pesa ya nchi(Manage state's currency),ugavi(mtawanyiko )wa pesa(Money Supply), na viwango vya riba(Interest rates).
Ndio taasisi inayosimamia benki zote za kibiashara zinazofanya shughuli zake nchini.
Taasisi hii imepewa mamlaka ya kutoa chapa ya pesa mpya za nchi na kusimamia mtawanyiko wake.
Kazi kuu kabisa inayofanywa na taasisi hii ni kusimamia ugavi(mtawanyiko) wa pesa za nchi kwa kutunga sera ya pesa ya nchi na kuisimamia(Monetary policy).
Sera hii inatekelezwa kwa kufanya mambo yafuatayo:
1.Kuelekeza viwango vya riba(Interest rates) kwa benki zote zinazokopesha.
2.Kupanga hitaji la hifadhi(Reserve requirement) kwa benki za biashara ambapo inazipangia benki hizo kiasi gani cha pesa kinachowekwa na wateja kitumike kukopesha na kiasi gani kipelekwe kwao Benki kuu kama hifadhi.
3.Kuziokoa benki za biashara kutoka katika dhoruba ya kifedha(Financial Crisis) pale zinapokumbwa na matatizo hayo kwa kuzikopesha.

Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz