CD ama Disk ni teknolojia ya kuhifadhi taarifa kama picha za digitali, video na hata mafaili ya maandishi inayotumika sana kwa siku hizi za karibuni. 
Taarifa hizo kila alama uhifadhiwa kwa kipimo kinachoitwa bytes na kwa kuwa taarifa huwa nyingi  kipimo huitwa MegaBytes(MB) kama hazijavuka MB 1000 na endapo zikiwa MB 1000 na kuendelea huitwa GigaBytes(GB).
Katika kifaa hiki cha duara taarifa huweza kuhifadhi na kusomwa kwa njia ya teknolojia ya mwanga(Laser technology).
Kwa leo tutaelezana kwa ufupi tu kuhusu tofauti ya Diski hizi ambazo tunazitumia kila siku katika shughuli zetu.
Kuna aina tofauti tofauti za Diski na nitazielezea kama ifuatavyo:

1.CD(Compact Disc)
Hizi huwa na uwezo wa kubeba taarifa za kuanzia ukubwa wa MB 700 hadi GB 1. Zipo za aina tatu ambazo ni:
     CD-ROM(Cmpact Disc Read-Only-Memory): Taarifa katika aina hii zinapoingizwa haziwezwi kufutwa wala kuongezwa ila zitasomwa tu na mtumiaji. Watengenezaji wakuu wakiwa ni Sony na Philips.
     CD-R(Compact Disc Recordable): Aina hii hutumika sana katika kuchoma nyimbo na video(CD Burning).
     CD-RW(Compact Disk Rewritable): Katika aina hii taarifa zinawezwa kuingizwa na kufutwa na kuandikwa upya hata mara 100,000.

2.DVD(Digital Versatile/Video Discs ): Hii huwa na uwezo mkubwa zaidi wa hadi kubeba taarifa za kuanzia GB 4.7 mpaka GB 17 katika mfumo video na picha.
Kuna aina tatu za DVD:
    DVD-ROM: Aina hii ikishaingizwa taarifa mtumiaji ataweza kuziangalia tu na hatoweza kuzifuta au kuziongeza.
    DVD Players(DVD+R na DVD-R): Hizi pia hutumika katika kuchoma movies kubwa na video nyingi zinazohitaji nafasi kubwa.
    DVD-RAM(DVD+RW na DVD-RW): Aina hii unaweza ukaingiza taarifa na ukitaka kufuta unaweza na kuingiza upya.


3. Blu-Ray: Hii ndio teknolojia mpya ambayo inahifadhi taarifa katika muono wa hali ya juu(High Definition).
   Blu-Ray diski inaweza kuhifadhi taarifa za kuanzia ukubwa wa GB 30 hadi GB 100. Na inatumia kisomeo(Deck) maalumu kilichopewa uwezo wa kusoma taarifa katika kifaa hiki na si zote zinaweza kusoma taarifa katika blu ray DVD.
  Hata hii yenyewe inakuja katika aina tatu kama zilizotangulia.(Blu Ray-ROM, Blu Ray-R na Blu Ray-RW).

Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz