Euthanasia neno lililokopwa kutoka katika lugha ya Kigiriki Euthanatos(Kifo kizuri).
Huu ni mfumo unaotumika kukatisha maisha ya mgonjwa anayeonekana anateseka kwa maumivu na hakuna uwezekano wa kitabibu wa yeye kupona au kupunguza maumivu yake.

Kuna kipindi ni mgonjwa mwenyewe ndiye anayeomba auawe kwa sababu zake binafsi lakini kama yeye yupo mahututi ndugu wa karibu wanaweza kuamua badala yake. 
Wakati mwengine ni Madaktari huamua kumpumzisha mgonjwa wao na maumivu au hata uamuzi wa mahakama.
Kuna nchi chache sana duniani zinazoruhusu jambo kama hili kufanyika kwa raia wake na nyingine ni kosa la jinai ukigundulika umemfanyia hivyo mgonjwa.
Uingereza kosa kama hili ukikutwa nalo unahukumiwa miaka hadi 14 jela.
Lakini hii ni tofauti sana na Marekani ambako mgonjwa, ndugu au mahakama inapoamua jambo hili linatekelezwa.
Hapo juu ni ushahidi wa tukio ambalo liliwahi kumpata mwanamke mmoja aliyeitwa Terri ambapo alikuwa mahututi na ikaamuriwa asitishiwe chakula na maji kwa njia ya mpira. 
Na baada ya kuondolewa huduma hizo aliishi hapo kitandani hospitali kwa muda wa siku tatu bila ya hizo huduma  mpaka alipofariki.

Wanaharakati wengi wanapouangalia mfumo huu wanapatwa na maswali tata vichwani:
1.Je, ni sahihi kukatisha maisha ya mgonjwa anayeteseka kwa maumivu yasiyopona?
2.Je, kuna mazingira yoyote ambayo yanaweza kuruhusu mfumo huu kutumika?
3.Kuna tofauti yoyote ya kimaadili, kati ya kumuua mtu anayeteseka au kumuacha afe?

Msingi wa maswali yote haya unaangukia kwenye swali moja kuu: Je, Kuna binadamu amepewa mamlaka ya kukatisha uhai wa binadamu mwenzake?
Pamoja na hayo kuna utafiti ulifanyika katika nchi amabazo mfumo huu unatumika mara kwa mara ambazo ni Marekani na Uholanzi.
Watafiti waligundua theruthi tatu ya watu waliofanyiwa mfumo huu ni wagonjwa wenyewe ndio waliomba.
Pia walichunguza chanzo kwanini wagonjwa hao mara nyingi wanaomba kufanyiwa hivyo.
 Jibu likaja ni kutokana na matatizo ya kisaikolojia kama msongo wa mawazo(Unyogovu), kujihisi amepoteza utu, Kujihisi ni mzigo kwa watu, na pia wengine walikuwa wanachukizwa na wao kuwa tegemezi.

Je, wewe unauonaje mfumo kama huu, unastahili kuruhusiwa pale ndugu, madaktari au mahakama ikiruhusu mgonjwa akatishiwe maisha?

Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz