Ukamilifu ni uzuri, wazimu ni fikra na ni heri kuwa na kejeli kuliko kuchosha watu.
WEWE, rafiki yangu ni mtu kamili na mwenye uwezo binafsi wenye kushangaza watu wengine.
Je, umeshasahau wewe ni nani?
Ikiwa umejisahau kutokana na mihangaiko ya dunia hii, basi ngoja nikukumbushe mambo ya ukweli ambayo unapaswa uanze kuiambia nafsi yako.

1."Sina muda wa kutulia"

Katika hali ya kawaida unaweza ukawa ulikutana na mambo yaliyokufanya uache kuwa mchakalikaji, mbishi na usiyekubali kushindwa katika kupigania mafanikio.
Nakuambia anza sasa kuamsha upya hisia za kupambana na vikwazo vyote vinavyokuzuia wewe kutimiza malengo yako na ukizingatia muda haukusubiri wewe.

2."Nina kila sababu ya kuiamini nafsi yangu"

Umeishi muda mrefu kwa kusikiliza sauti za watu wakikuambia wewe unapaswa uweje kulingana na mitazamo yao.
Unapaswa ujue kuwa unapotaka kufanya jambo lolote mtu wa kwanza kumsikiliza ni nafsi yako ambayo siku zote haina muda wa kukudanganya.
Si kwamba usisikilize ushauri kutoka kwa watu wengine, rahasha, ila unapaswa utangulize nafsi yako kwanza.

3."Upekee wangu ndio nguvu yangu kuu"

Ndio hujakosea, upekee wako ndio utakao kutofautisha wewe na mtu mwengine.
Yawezekana mazingira yalikuwa yanakufanya utake kuwa na tabia kama za fulani na hivyo ukajikuta unapoteza uhalisia wako.
Anza sasa kuishi wewe na sio mtu mwengine.

4. "Nitatumia changamoto zangu kujiimarisha na sio kuniangusha"

Hakuna mafanikio yasiyo na changamoto na ukiona changamoto inakuwa kubwa basi ukkishinda na mafanikio 
yake yanakuwa makubwa.
Yawezekana watu walikutendea uovu lakini wewe ukashikiria upendo dhidi yao.
Badala ya kufunga mlango kuzuia changamoto katika maisha yako fungua ili ukutane nazo zikuimarishe.

5."Bado nina nafasi ya kujifunza zaidi hata kama nimeshindwa baadhi"


Kitu kizuri kwako ni kuwa na moyo wa kutoruhusu anguko la mambo yaliyopita yaendelee kuzuia inuko la mambo yajayo.
Dunia ina fursa nyingi za kujifunza moja, mbili au tatu zinaposhindikana inuka angalia nyingine zaidi na zaidi.
Hakuna jambo kubwa linaweza kukamilika kwa siku chache tu unapaswa uangalie njia mbadala bila kuchoka.

ANZA SASA KUIAMBIA NAFSI YAKO MANENO HAYO
 NAWE UTAONA MABADILIKO UTAKAYO TENGENEZA KATIKA MAISHA YAKO.

NASHUKURU SANA WAFUATILIAJI WA MAKALA ZANGU SABABU MMEKUWA WAVUMILIVU SANA KATIKA KIPINDI CHOTE AMBACHO SIKUWA NA NAFASI YA KUANDIKA NA KUWALETEA MAKALA MPYA LAKINI MMEONYESHA MOYO WA DHATI WA KUTOACHA KUITEMBELEA BLOG YENU.
TUENDELEE KUWA PAMOJA KUELIMISHANA.

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz