Katika maisha fumbo kubwa ni kutojua kesho kitatokea kitu gani katika maisha yetu.
Lakini wote mioyoni tunaombea tuwe na maisha ya furaha kuanzia wakati tuliopo mpaka kesho itakapofika.
Kwani maamuzi tunayoyafanya leo ndio yanaamua kesho tutakuwa na kitu gani.

Hebu tujaribu kuangalia hatua fupi ambazo tunaweza kuzitumia ili kujiandalia mazingira ya furaha siku zijazo:
1.THAMINI WATU NA VITU KATIKA MAISHA:

Mara nyingi unashindwa kutambua mchango wa watu wanaokufanyia mema katika maisha yako mpaka pale wanapoacha kufanya hivyo.
Haupaswi kuwa hivyo, inabidi uwe na shukrani kwa kile unachopata, kwa wale wanaokupenda, na wale wanaokujali.

2.USITILIE MAANANI MAMBO HASI KUKUHUSU WEWE:

Ukiwaruhusu watu wakutoe kasoro kila wakati, bila kukueleza mazuri yako, hautaweza kuwa imara kamwe.
Tupilia mbali maoni yasiyokujenga na ambayo yanakuumiza.
Hakuna mwenye haki ya kukuhukumu. Inawezekana walisikia historia yako na kuona matukio yako lakini wewe ndiye unayejua jinsi gani unaumizwa nayo.
Hauna uwezo wa kuzuia watu waseme nini kuhusu wewe, ila una uwezo wa kuzuia mtu asikwambie maneno yake ya sumu.

3.WASAMEHE WALIOKUUMIZA:

Kuna misemo inayosema; mtu wa kwanza kuomba msamaha ni shujaa na mtu wa kwanza kusamehe ni  jasiri.
Ukifanya hili unayafanya maisha yako yawe huru pasipo kuwa na mashaka.
Anza sasa kuwa shujaa, jasiri, huru, na furaha  katika maisha yako.

4.ISHI KAMA ULIVYO:

Ukifanikiwa kutambua kwamba una vitu fulani ambavyo ni tofauti na wengine usijaribu kujibadili ili uwe kama wao.
Kuwa wewe hakuhitaji gharama yoyote lakini kuwa mtu mwengine ni gharama kubwa.
Watu wakikucheka kwa kuwa wewe ni tofauti na wao, usihuzunike kwa kuwa na wao pia ni tofauti na wewe.

5.CHAGUA KUISIKILIZA SAUTI YAKO YA NDANI:

Usiwe mtu wa kusikiliza maelezo ya kila mtu, yachuje kwanza pale unapotaka kufanya maamuzi ila sikiliza zaidi moyo wako unakwambia nini.

6.BADILI TABIA ZAKO MBAYA:

Ni jambo gumu sana kuacha kitu ambacho kimekuwa ni sehemu ya maisha yako,na itakubidi uanze kuishi bila hicho kitu.

7.CHAGUA MAHUSIANO KWA MAKINI:

Ukifanya kosa katika kuchagua mahusiano yako utakuwa unajitengenezea mazingira ya kukosa furaha.
Kumpenda mtu si tu kumwambia unampenda kila siku bali kumtendea upendo kila siku.
Uhusiano unatakiwa uchaguliwe kwa hekima, usikurupukie kuwa na mtu kwa kuwa uko na upweke bali mpaka uwe tayari.

KATIKA HATUA TULIZOONA HAPO JUU TUNAWEZA KUZITUMIA KUJIANDALIA MAZINGIRA YA FURAHA SIKU ZIJAZO.
ZITUMIE NA UTAONA MATUNDA YAKE SIKU ZIJAZO.





Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz