DNA(Deoxyribonucleic acid) ni chembe hai za binadamu ambazo zinarithishwa kutoka kizazi hadi kizazi.
Chembe hizi za DNA hupatikana kutoka katika chembe hai nyeupe za damu. Mtu anayepimwa hutolewa sampuli ya damu au muda mwengine sampuli hutolewa ndani ya chembe za shavuni.
Kipimo hiki hufanyika katika maabara maalum na huchukua siku saba au zaidi kutoa majibu.
Kuna sababu au matumizi mbali mbali ya kipimo hiki cha DNA. Baadhi ya sababu hizo ni:
1.Kutambua matatizo ya kimaumbile(Genetic Disorder testing)
2.Kutambua kama mwanafamilia amebeba virithishi kwenda kwa mtoto(Carrier testing)
3.Kutambua mzazi halisi(Paternity testing)

4. Kuhakiki ushahidi wa uhalifu(Crime scene investigation) Hapa timu maalumu ya uchunguzi huchukua vitu kama damu iliyomwagika, mbegu za kiume au chembe nyingine kutoka katika nywele au mate.
5.Kutambua ubora wa kiini tete(Preimplantation DNA test) Hii hufanywa na watu wanaotaka kufanya uzazi wa kupandikiza mbegu.
Kipimo cha DNA kinabaki kuwa moja ya vipimo ghali sana kufanyika kwani kwa kipimo rahisi kabisa cha kutambua mzazi halisi hugharimu shilingi laki 3 za Tanzania au dola mia 200 za kimarekani.




Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz