VIZA 
             Viza ni cheti au muhuri maalumu unaowekwa 
(katika hati ya kusafiria ya mwombaji) na mamlaka ya uhamiaji ya            nchi husika ambayo mwombaji anataka kutembelea,
alama hii ina maanisha mwombaji amepewa ruhusa ya kuingia nchi                           husika kwa muda maalumu.
Kuna viza ambazo zinaweza kukuruhusu uingie mara moja na kutoka                         (Single entry visa) na 
kuna viza nyingine zinakuruhusu kuingia na kurudi zaidi ya mara             mpaka pale muda uliopangwa kuisha matumizi ufike 
                     (multiple entry visa).


                             Viza za muda
Kuna aina mbali mbali za viza za muda zinazotolewa na ubalozi wa Marekani. Aina hizi za viza zinatambulika na sheria ya Uhamiaji ya Marekani(Immigration Law)na inaenda sambamba na dhumuni la kusafiri mwombaji.

Viza hizi zimewekwa kwa ajiri ya wasafiri ambao wana nia ya kukaa Marekani kwa muda na kurudi nchini kwao.
             Aina za Viza za muda ni pamoja na:
               .       Biashara na Utalii (Mapumziko)
2              .       Matibabu
               .       Wanafunzi
     .       Mwanadiplomasia, Maofisa wa serikali, na Wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa 
               .       Wageni wa kubadilishana.
               .       Wafanyakazi wa muda
7              .       Waandishi wa habari
8              .       Wafanyakazi wa mashirika ya dini

         A.      Biashara na Utalii (Mapumziko)

Kutokana na dhumuni lako hili la kwenda Marekani, Unahitaji aina hizi za Visa B1, B2 au B1/B2 viza.

                  B1-Waingiaji wa muda Kibiashara
Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina gani ili uweze kufanya biashara Marekani?
Kama unataka kuingia Marekani kwa dhumuni la biashara unahitaji aina hii ya viza. Viza hii haitakuruhusu ukubali ajira Marekani,lakini unaweza kukubaliana mkataba, mashauriano na washirika wa kibiashara,kukutana na wateja,kushiriki makongamano na semina na kuchukua oda za wateja.
                           
       
              B2-Waingiaji wa muda Utalii (Mapumziko)
 Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina gani ili uweze kufanya utalii au kutembelea marafiki Marekani? 
Unahitaji viza hii kama una dhumuni la kuingia marekani kwa ajiri ya mapumziko, au kuitembelea familia na marafiki.

     B1/B2- Waingiaji wa muda wa biashara au utalii (Mapumziko)

Umewahi kujiuliza kama unataka kutembelea maonyesho ya biashara halafu ukitoka hapo ukashangae shangae kidogo mambo mengine?
Unahitaji viza aina ya B1/B2 kama unataka kwenda Marekani kwa dhumuni la ama biashara au mapumziko au kwa shughuli maalumu,elimu, dini, makongamano ya kitaaluma,kozi za muda mfupi, kushauriana na washirika wa kibiashara au wataalamu,kutibiwa, kushiriki katika shughuli za kujitolea katika mashirika ya misaada au kushiriki katika michezo.


                      B.      Matibabu

Ili hali yako ya ugonjwa ipewe kipaumbele unapoomba viza unatakiwa                        uwe na taarifa zifuatavyo:                       
   a) Barua iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kutoka kwa daktari wako wa hapa Tanzania:
-          Ikielezea hali yako ya ugonjwa;
-          Inayofafanua chanzo cha ugonjwa na sababu za kuhitaji matibabu Marekani.

   b)      Ushahidi wa fedha ya kutosha kwa matibabu:
-          Ushahidi wa ufadhili wa kifedha au hati ya kiapo cha ufadhili (Fomu 1-134) kutoka kwa mfadhili. Zinatakiwa hati halisi tu-faksi na nukushi hazikubaliwi.
-          Uhakika kutoka kwa mfadhili kwamba mgonjwa atakuwa na tiketi ya kurudi.
-          Barua kutoka kwa mwajiri wa mfadhili  ikiwa na anuani ya kampuni ikieleza cheo chake kazini, mshahara, na mwisho wa ajira yake.
-          Barua kutoka benki ya mfadhili ikiwa na anuani ya benki  na ikiwa imesainiwa na ofisa wa benki.
-          Ripoti ya ulipaji kodi wa mfadhili kwa mwaka uliopita.


    c)       Barua binafsi ya mfadhili kwenda ubalozi wa Marekani
-          Ikieleza wapi hasa mgonjwa atafikia wakati wote ambao atakuwa anahudhuria matibabu.
-          Ikielezea kwa nini ameamua kumfadhili mgonjwa (mwombaji wa viza), Historia kamili ya uhusiano wao, ni wa vipi na ulianza linin a anatarajia kupata nini kutokana na ufadhili wake.

    d)      Barua kutoka kwa daktari wa Marekani:
-          Ikieleza hali ya mgonjwa na utayari wa kumtibu.
-          Makadirio ya juu na ya chini ya kipindi atakachokuwa         anamtibu mgonjwa
-          Makadirio ya juu na ya chini ya gharama za matibabu (Ada       ya daktari, ada ya hospitali, gharama za vipimo,        gharama za dawa na gharama zote zitakazohusiana matibabu)
-          Uhakika kwamba gharama za matibabu zitalipwa na fungu       lipo tayari kwa ajili ya kugharamia.
-          Tarehe maalumu ya ahadi.

Sheria ya uhamiaji ya taifa la Marekani imeweka dhahania kuwa       waombaji wote wa viza za muda wana nia ya kukaa Marekani moja kwa moja. 
Kwahiyo kuwa na vigezo vya kupata aina hizi za viza za muda unahitaji kuwathibitishia kuwa dhahania yao si sawa kwako na hauna   nia ya kukaa moja kwa moja.

Unaweza kuishinda hii dhahania yao kwa kuwapa ushahidi kuwa wewe una mambo ya msingi yatakayo kurudisha nyumbani na wala huna nia ya     kuikimbia nchi yako.

Itaendelea.....

Majanga ya asili(Natural Disasters) ni matukio yanayotokea kwa wingi duniani hutumia muda mfupi lakini madhara yake huwa ni makubwa.
Katika muda mfupi yanayotumia huondoa maisha na kujeruhi watu pamoja na uharibu wa mali.
Majanga haya huwa hayana eneo maalumu popote yanaweza kutokea japo kuna baadhi ya maeneo huwa ni mara kwa mara yanajirudia.

Mara nyingi unapowauliza mashuhuda wa matukio haya ya majanga ya asili hukosa jibu kamili la kilichotokea, kwa mfano mashuhuda wengi wa kimbunga watakwambia "Niliona joka kubwa likitua juu ya nyumba na kuibomoa yote!!"
  
Hii inaashiria wakati majanga haya yanatokea taswira ya dunia huwa ni tofauti kabisa, ni kama ya mtu aliyekasirika na kukunja uso.
Hebu tujaribu kuyajua majanga 5 makubwa ambayo yanapotokea uharibifu wake huwa ni mkubwa sana.
1.UMEME(lightning):
Umeme hutokea pale ambapo kunakosekana ulingani wa chaji za umeme katika anga(Electric charge unbalance).
Kitendo hiki husababisha eneo moja la mawingu lenye chaji nyingi, kuachilia chaji zake(Electrostatic Discharge),ili kwenda kujaza eneo lililopungukiwa na hivyo chaji hizo zinapokutana na chaji za mawingu mengine zinazolingana husababisha kusukumana na kuanguka na kuambatana na sauti kubwa ya radi(Thunder).

2.MOTO WA MSITUNI(WILD FIRE)
Nyasi ndogo za msituni zinapopigwa na jua kwa muda mrefuhukauka kabisa na kuanza kushika moto.
Matukio ya moto wa msituni hutokea zaidi katika majira ya kiangazi na kipupwe ambapo huchangia kusambaa kwa kasi kwani matawi mengi ya miti huwa yamekauka hivyo kushika haraka moto huo na unachagizwa zaidi na upepo mkali.

3.MLIPUKO WA VOLKANO(VOLCANIC ERUPTION):
Magma iliyoyeyuka chini ya miamba husababisha mlipuko wa miamba pale inapopigwa presha kupita katika njia ndogo na hivyo huruka juu na kuanza kusambaa juu ya ardhi.

4.BANGUKO(AVALANCHE):
Huu ni muanguko wa mapande makubwa ya barafu kutoka juu milimani na kushuka chini kwa kasi kubwa na kuleta uharibifu kwa wakazi wa karibu na eneo husika.

5.MAJIVU YA VOLKANO(VOLCANIC ASH):
Janga hutokea pale ambapo volkano imelipuka na kutoa majivu mazito ya miamba iliyosagwa angani.
Wataalamu wanasema moshi huu ndio huchangia kuua watu wengi kwani huwa na sumu. 
Kwa mfano Mlima mmoja Iceland mwaka 2011 ulipo lipuka na kutoa hayo majivu mazito yalisukumwa na upepo na kusababisha nchi nyingi za ulaya kusitisha safari zao za ndege.

 6.KIMBUNGA(HURRICANES):
Ni dhoruba kubwa inayoweza kuchukua eneo la umbali hadi wa maili 600 ikiambatana na upepo mkali unaozunguka na kuelekea juu kwa kasi ya maili 75 mpaka 200 kwa saa.

7.DHORUBA YA MCHANGA(SANDSTORMS):
Dhoruba hii hutokea pale ambapo upepo mkali unapovuma eneo ambalo lina mchanga mwingi ulioachana na kuunyanyua kuelekea unapoelekea wenyewe.

8.TSUNAMI

Hili ni dhoruba linaloanzia katika kina cha bahari ambapo miamba iliyoshikamana, inapoachana huku mmoja unaelekea chini na mwengine juu unasababisha kunyanyuka na maji kuelekea ufukweni.
Hali hiyo husababisha maji kuingia kwa kasi maeneo ya kuishi watu na kufanya uharibifu.

9.TORNADO(KIMBUNGA CHA NCHI KAVU):
Huu ni mkusanyiko mkubwa wa hewa inayozunguka ikiwa imeshuka hadi kugusana na ardhi ambayo inaweza kuanzishwa na umeme unavyotokea.
Kuzunguka huko kwa hewa iliyo kwenye kasi kubwa husababisha kuzoa na kuharibu kitu chochote itakachokutana nacho.

10.TETEMEKO LA ARDHI(EARTHQUAKES):
Hili janga husababishwa na mpasuko miamba wa chini ya ardhi ambapo hupelekea nguvu ya mawimbi ya seismic(Seismic waves) kuzalishwa na kusababisha ardhi kutikisika.
Haya majanga yote yana madhara makubwa pindi yanapotokea eneo lolote juu ya uso wa dunia.









 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz