Kula chakula chenye virutubisho sahihi ni jukumu la lazima la binadamu kama anahitaji kuwa na afya njema.
Dunia ina vyakula vya asili ambavyo ndani yake kuna virutubisho muhimu vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa.
Na vyakula hivyo si vingine bali ni vile vya kijani vyenye uwezo hadi wa kuponya magonjwa.

Hapa nawaletea vyakula vya aina saba ambavyo vinapatikana kwa urahisi katika mazingira yetu na kazi zake:
1.MCHICHA(SPINACH):
Hii ni mboga inayolimwa sana katika maeneo yetu, kwani huwa haichagui hali ya hewa maalumu.
Wewe ukiweza kuandaa kitalu kidogo maeneo unayoishi na kukiwekea mbolea, ukiotesha mchicha siku chache tu unaanza kuula.
Mchicha una:
1.Vitamini(A,C,E,K na B6)
2.Madini(Manganese,calcium,Selenium,riboflavin,iron, niacin, na zinc)
Mchicha unasaidia sana kuupa mwili nguvu ya kupambana na kansa ya ngozi na matiti.

2.KAROTI(CARROTS):
Karoti pia zinapatikana kwa wingi sana maeneo yetu tunayoishi.
Zinasaidia kuimarisha kinga ya mwili, ina kalori 52 ya kipimo cha nishati ya mwili, mafuta kidogo na hazina kolesto.
Zina nguvu ya kuua seli za mwanzo za kansa katika mwili wa binadamu kama kansa za mapafu, ngozi, na ya koo.
Ukiila ikiwa imepikwa au mbichi bado inabaki ni chakula muhimu kutumiwa kila siku.

3.MAPERA(GUAVAS):
Hupatikana sana maeneo yetu tunayoishi na ni tunda ambalo si gharama kulipata.
Linasaidia sana kwa mtu anayetaka kupunguza uzito, kuondoa kiungulia, 
kansa, magonjwa ya moyo na huzuia matatizo ya ngozi.
Husaidia pia kuongeza uwezo wa kuzalisha wa mwanaume, ni tajiri wa vitamini C, na madini mbali mbali.

4.PARACHICHI(AVOCADO):
Hili pia linapatikana sana na bei yake sio kubwa mpaka imfanye mtu ashindwe kununua.
Linasaidia kuimarisha mfumo wa ufanyaji kazi wa moyo kwa kuchochea kolesto nzuri inayoboresha ufanyaji kazi wa moyo bila kuinyanyua kolesto mbaya inayoharibu ufanyaji kazi wa moyo.

5.TUFAA LA KIJANI(GREEN APPLE) NA PEASI:
Japo hili bei yake ni kubwa kidogo kuliko yaliyotangulia lakini upatikanaji wake sio mgumu.
Linasaidia kuzuia ugonjwa wa kiharusi kwa binadamu.
Binadamu anahitaji gramu 25 kila siku ili kuzuia uwezekano wa kupata kiharusi kwa asilimia 9 lakini hili tunda zima lina gramu 120.

6.CHAI YA KIJANI(GREEN TEA):
Hiki ni kinywaji ambacho hakina kalori hata moja ya nguvu za mwili na humsaidia mtumiaji kupunguza mwili.
Husaidia kuzuia kansa pia.

7.PILIPILI HOHO(GREEN PEPPER):
Hoho mara nyingi tunaitumia katika kachumbari na inapatikana sana katika maeneo yetu na bei yake ni ya kawaida.
Ina utajiri wa vitamini C na pia ina uwezo wa kusaidia kunyanyua kinga za mwili.
Sio mbaya kila unapoenda kula ukabeba pilipili hii ambayo sio kali na unaweza ukaitafuna bila matatizo yoyote.



BAADA YA MAELEZO HAYO MAFUPI YA VINAVYOPATIKANA KATIKA VYAKULA HIVI, NA MAGONJWA ZINAZOSAIDIA BINADAMU KUPAMBANA NAYO.

 NATEGEMEA  SASA MATUMIZI YETU KATIKA HIVI YATAKUWA MAKUBWA ILI KULINDA AFYA ZETU NA MAGONJWA.












Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz