Wingi wa watu sasa hivi duniani ni zaidi ya bilioni 7 na unaendelea kukuwa kwa kiwango cha watu milioni 82 kila mwaka.
Kutoka mwaka 1960 hadi 2010 wingi wa watu duniani uliongezeka kutoka bilioni 3 hadi bilioni 6.8 kutokana na takwimu za umoja wa mataifa.
Kwa maneno mengine unaweza ukasema katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita dunia imeshuhudia ongezeko kubwa la watu kuliko miaka milioni mbili watu wa kale waliyoishi.
Katika kipindi cha karibuni ongezeko la watu lilikuwa katika kiwango cha asilimia 1.2, hii ikimaanisha kuwa baada ya miaka 58 ongezeko litakuwa mara mbili ya hili la sasa.
Kutokana na takwimu za umoja wa mataifa za mwaka 2000 hadi 2005 ongezeko lifuatalo lilitokea katika mabara yafuatayo:
- 227,771,000 Bara la Asia;
- 92,293,000 Bara la Africa;
- 38,052,000 Bara la America ya kusini;
- 16,241,000 Bara la America ya Kaskazini;
- 3,264,000 Bara la Ulaya;
- 1,955,000 Bara la Australia ;
- 383,047,000 Jumla.
Hebu tuangalie Nchi kumi zinazoongoza katika kuchangia ongezeko la watu duniani kutoka mwaka 2000 mpaka 2011, na idadi wanayotarajiwa kuiongeza ikifika 2050:
Tanzania ipo nafasi ya thelathini(30) katika msimamo wa dunia wa nchi zenye idadi kubwa ya watu ikiwa na watu 43,188,000 kwa takwimu za mwaka Julai 1, 2010.
SWALI LA KUJIULIZA NI; JE, IDADI KUBWA YA WATU KATIKA NCHI INACHANGIA KUPATA MAENDELEO YA HARAKA AU INARUDISHA NYUMA?JARIBU KUANGALIA NCHI ZINAZOONGOZA MSIMAMO HUU ZINA MAENDELEO AU HAZINA?
0 comments:
Post a Comment