16.MIPANGO ISIZIDI MATENDO:

Acha kupanga sana bila kufanyia kazi mipango yako, 
inawezekana unaogopa kukosea lakini kukosea ni sehemu ya kujifunza.

17.TENGENEZA VIPAUMBELE:

Piga hesabu ya uzoefu wako wa nyuma, kazi,  na elimu.
Tengeneza orodha ya vitu vitano ambavyo ulikuwa unapenda kuvifanya na unavifurahia.
Kwa kutumia orodha hiyo 
jaribu kuchagua tatizo lililo katika jamii yako ambalo utaweza kulitatua kwa kutumia vitu unavyopenda kufanya.

18.JIFUNZE KUTOKATA TAMAA:

Unatakiwa ujitengenezee shauku ya kufanya biashara 
unayotaka kwa uvumilivu,
kwani katika baishara yeyote hakuna mteremko wa mafanikio ya bure 
bila kujitoa na kuwa mvumilivu.

19.TUMIA TEKNOLOJIA VIZURI:

Tumia fursa iliyopo katika mitandao ya kijamii katika kutafuta uzoefu zaidi wa biashara unayotaka kufanya.
Tumia nafasi yako ya kuwa katika mtandao wa twitter au facebook na 
mtu au kikundi cha watu wakufunzi wa biashara unayotaka kufanya na utaona msaada wataokupatia.

20.JIKUMBUSHE WAZO LAKO KILA WAKATI:

Ukilifanya wazo lako kuwa wimbo wa taifa kichwani mwako,
utajisaidia kulikuza na kulipenda.

21.USIOGOPE KUTUMIA GHARAMA:

Kuna kipindi utahitaji kukutana na watu ambao wanafanya ujasiliamali 
ili ujifunze kitu kutoka kwao.
Ukipata nafasi ya kumualika chai au chakula cha mchana mahali ili tu upate nafasi ya kuongea naye, 
usione umepoteza pesa yako kwani utakachotoka nacho hapo kitakuwa na thamani kubwa.

22.ANZA KWA KUFANYA KAZI ZA KUJITOLEA:

Katika kipindi ambacho unajiandaa kuingia katika ujasiliamali,
 kubali kujitolea kufanya shughuli mbali mbali bila malipo katika jamii yako.
Hapa ndipo utakapogundua 
kwa ukaribu kwamba katika shughuli unazojitolea ipi umeipenda zaidi kuifanya.

23.TAFUTA MTAJI WA KUTOSHA:

Yawezekana unataka kuingia katika biashara ambayo hata gharama
 ya kuendesha hujui ikoje.
Ni vyema ukajua biashara hiyo itahitaji mtaji kiasi gani na uanze 
kutafuta hicho kiasi kabla haujaanza ili usije ukaishia njiani,
tafuta mtaji wa kutosha ndio uanze.

24.KUWA MBUNIFU:

Hakutakuwa na maana ya wewe kuingia katika ujasilamali 
na kuja kuufanya vile vile ambavyo mwengine anayefanya shughuli kama 
yako anafanya hivyo.
Lazima utambue kuwa ubunifu katika bishara yoyote ndio unalipa.
Hakikisha unafanya unachokipenda na kinakulipa.

25.ANZA KWA KUTENGA MUDA KIDOGO:

Kama umeajiliwa mahali na unataka kufanya biashara, 
usiache kazi kabisa kwa kudhani utafanikiwa kwa haraka kwa kuwa tu una wazo zuri la biashara.
Anza kwa kutenga muda wako mfupi katika siku kufanya biashara unayotaka.
Kama ukiona unashindwa kutengeneza faida katika muda huo wa 
siku uliojitengea basi hiyo biashara sio ya kuingia kichwa kichwa.

HIZO NI BAADHI YA MUENDELEZO WA NJIA AMBAZO ZINAWEZA KUKUSAIDIA IKIWA UNATAKA KUJIAJIRI.
ENDELEA KUFUATILIA NYINGINE NYINGI ZINAKUJA.


Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz