Si mara moja tumewahi kusikia msemo unaosema;
"Usimuhukumu mtu kwa anachosema, bali kwa anachotenda".
Lakini katika biashara msemo huo unawekwa kando kabisa, 
ukikosea kitu cha kusema kwa mteja wako basi unamfanya akutafsiri anavyojua yeye,
 na unaweza ukampoteza kabisa.

Hebu tuangalie kauli 7 ambazo unatakiwa uzitumie kwa mteja wako:

1.TAJA JINA LAKE KWA USAHIHI:

Usije ukarogwa na kuropoka vibaya jina la mteja wako kama
 umeamua kulitaja.
Hakuna kitu kinachomkasirisha mteja kama jina lake kutajwa vibaya au umwite jina tofauti na lake.
Kwa wateja wengi hii huashiria kwamba haujali kuwafahamu na
 hana umuhimu.
Unatakiwa kama mteja umekutana naye kwa mara ya kwanza,
 ni vyema kumuuliza jina lake na kama unajijua ni mwepesi kusahau ni bora uandike mahali.

2.TAJA SAHIHI JINA LA KAMPUNI YAKE:

Hapa napo kama unafanya biashara na kampuni fulani kuwa makini
 kulifahamu jina lake.
Na unapotaka kuitaja hakikisha unajua namna ya kuitamka, 
kwani ukikosea tu inapunguza morali wa kampuni kufanya biashara na wewe.

3.TAJA BEI YA UHAKIKA:

Mara kwa mara unakutana na mfanyabiashara anakubaliana bei na mteja na anatumia kauli kama;
"bei yake ni kati ya....mpaka...".
Hii itamuonyesha mteja kuwa wewe unataka kumdhulumu, kwani kama unajua bei halisi uliyonunulia bidhaa yako,
 lazima utakuwa unajua kiwango kamili cha kutaja.

4.USIMDHANIE MTEJA WAKO:

Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanapenda kuwadhania wateja wao kwa nia ya kutaka kuwa karibu zaid nao.
Kwa mfano mteja anafika dukani na mtu pembeni;
yeye bila kuuliza anaanza kumwita yule wa pembeni shemeji au wifi,
 bila kufahamu uhusiano wao.
Hili linawakasirisha wateja wengi sana na kuona unaingilia maisha yao.

5.USIJIRAHISISHE KUPITILIZA:

Ikiwa unaelewana biashara na mteja wako, 
ni vyema usionyeshe 
kana kwamba usipopata tenda yake biashara yako itayumba.
Wateja wengi huwa hawapendi kufanya biashara na wafanyabishara ambao hawako imara.


6.USIKISIE HOVYO KAZI YA MTEJA:

Ukiwa unataka kufanya bishara na ama mtu au kampuni ni vyema 
ukauliza shughuli zake, kuliko wewe kujifanya mtabiri na kukosea.
Ni afadhali kama hujaijua shughuli yake umuulize,
na yeye akakutajia.

7.USIMDANGANYE WAZI WAZI:

Kuna baadhi ya wafanyabiashara anaongeza mbwe mbwe nyingi,
mpaka mteja anaingia shaka.
Kwa mfano, unamwambia mteja kuwa ikiwa atawapa tenda basi utamchagulia 
wafanyakazi wa kiwango cha juu kufanya shughuli yake.
Hii itatuma tafsiri kuwa inawezekana biashara yako ina matabaka ya wafanyakazi wanaojua na wasiojua, 
na atahisi wazi unamdanganya ili tu akupe tenda.

JAPO TABIA ZA BINADAMU ZINABADILIKA, LAKINI TABIA ZA WATEJA WENGI KATIKA BIASHARA HUWA ZINAFANANA.

NI VYEMA KUWA MAKINI NA NINI UNACHOONGEA MBELE YAKE KWA KUFUATA MIFANO HII MICHACHE.



Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz