Kuacha kutazama picha za ngono kunahitaji nidhamu, 
ujasiri na imani ndani yake.
Kwani bado madhara yake huwa hayaonekani mbele ya macho ya mtumiaji.
Je, kuangalia picha za ngono kuna madhara gani?

1.MAHUSIANO:

Si tu katika mahusiano yako na mchumba wako bali hata kwa marafiki,
 familia, wanafunzi wenzako, na hata wafanyakazi wenzako.
Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha wazi kuwa watu wanaoangalia picha za ngono,
 wana msongo mkubwa wa mawazo na kujihisi wapweke kuliko wasioangalia.

2.UBONGO:

Sehemu ya ubongo inaathirika na mihemko bandia inayotengenezwa  na anayeangalia,
 na hivyo kusababisha unalemaa na kushindwa kabisa kujibu mihemko halisi.
Picha hizi zitakufanya ujitenge na jamii yako, kwani kila muda utataka uwe peke, 
yako eneo unalokaa ili upate wasaa wa kuangalia vizuri kwa kujinafasi.
Maisha yanakosa shauku ikiwa ubongo utazoeshwa kujibu mihemko ya bandia
 kwa kiwango cha juu.

3.KUFURAHIA MATUKIO:

Unaweza ukajikuta kila kitu kwako kinachukiza kuangalia au kujihusisha nacho,
hata ukiangalia kitu kingine utaona bora kiishe ili uangalie picha zako.
Na hii ni hatari kubwa sana kwani utaufanya ubongo ukose taarifa za ziada na zile za ngono ndio zitatawala.

Fuata hatua zifuatazo kujiachisha na tabia hii:

1.AMUA KUACHA LEO USISEME KESHO:

Mara kwa mara watu ambao wamebobea katika uangaliaji wa picha hizi,
 wanapomaliza kuangalia hujipa ahadi kwamba kesho tu nitaacha kuangalia.
Baadaye wanajikuta kesho haifiki,
 kwani kila siku ina kesho yake.
Ukitaka kweli kuacha amua muda uliopo sasa usipange kesho ambayo hujaifikia.

2.USIKAE KARIBU NA MAZINGIRA YA PICHA HIZO:

Ukitaka kujisaidia kuondokana na tatizo hili, hakikisha una kaa mazingira
 ambayo hayajatawaliwa 
na picha za ngono.
Kama unatumia kompyuta, simu au 
hata iPad ambayo 
ndani yake umehifadhi picha hizo zifute sasa,
na ikiwa unatumuia 
DVD au CD ziharibu usikae nazo ndani,
 na hata katika 
historia ya anwani ya 
mitandao uliyotembelea,
 kama zipo zifute kabisa kwani ukiziona utarudi kule kule.

3.USIHESABU SIKU AMBAZO HUJAANGALIA:

Mara nyingi kama umebobea kuangalia huwa haipiti siku bila 
kutupia jicho picha hizo.
Na kuna muda mwingine unabanwa na shughuli nyingi kukupelekea 
kufikisha siku kadhaa hujaangalia,
sasa usikae chini kuanza 
kuhesabu siku ambazo hujaangalia utajikuta unajipa kibali cha 
kutaka kuziangalia haraka iwezekanavyo.

4.USIKAE MAZINGIRA YA PEKE YAKO:

Mara nyingi kama uliwahi kuangalia picha za ngono na ukajikuta uko 
mazingira ya peke yako,
 ya ama unaangalia tamthilia au 
kusoma kitabu chochote kitakachokuwa na habari ya masuala ya watu 
kujamiana itakukumbusha kamchezo kako.
Usichague pia kuangalia
 peke yako picha ziliwekwa
 alama ya miaka 18 zitakuchochea urudi ulipotoka.

5.EPUKA MAZUNGUMZO MACHAFU NA MARAFIKI:

Mara nyingi tunapokaa na marafiki zako ambao wanapenda kuhadithia 
masuala ya ngono tu watakuchochea.
Maana kuna wengine ni mafundi wa kuhadithia hizo vitu,
 kana kwamba wao ndiyo watengenezaji,
sasa unapoona wanaanzisha hizo habari kama huwezi kuwasimamisha basi ni heri ujitenge nao.

6.EPUKA HISIA CHOCHEZI ZA NDANI:

Siri kubwa katika hizi picha zinampa hisia nzuri mtazamaji,
 na kuona hakuna chenye thamani yoyote muda huo.
Kwa hiyo epuka hisia za hasira, 
upweke, na huzuni kwani 
zitakufanya uone eneo pekee la kwenda kujipumzisha ni kuangalia picha hizo.

7.FUTA FIKRA POTOFU:

Achana na fikra potofu za mtaani kuwa kuangalia picha za
 ngono ni kujifurahisha nafsi na hazina madhara.
Lakini kiuhalisia madhara yanayoambatana na tukio lake utayaona baadaye.
Kuna wengine watakwambia kuwa usipoangalia hizo picha utakuwa mshamba na hauendi na wakati.

8.USIJISEMESHE KUWA HUWEZI KUACHA:

Unapokuwa unaangalia hizi picha mara nyingi akili yako inajizoesha,
 na kuona ni utaratibu 
wake wa kila siku.
Kwa hiyo moyoni utakuwa unajisemesha kuwa kuacha kitendo hiki 
hautaweza kamwe,
kitu ambacho kitakufanya uwe dhaifu wa kujitawala.

9.ACHA KUJIKUMBUSHA PICHA ULIZOANGALIA:

Mara nyingi unapokuwa mazingira fulani ya kuwaza mambo mbali mbali, 
mawazo ya picha ulizoangalia ukiyatanguliza kwanza utajifanya 
uwe na shauku ya kwenda kuangalia upya.
ukiona kuna kazi unafanya kazi
 katika kompyuta au umeshika kifaa chochote chenye uwezo wa kukuonesha 
picha hizo ni heri ukizime 
kwa muda huo halafu fikiria kitu kingine kwa haraka.

LINAPOKUJA SUALA LA KUACHA TABIA,
 HII NI VYEMA UKAFIKIRIA ZAIDI KAMA KUNA FAIDA YOYOTE UNAYOPATA.
 NA JE KUNA SIKU UTAKAYOKAA CHINI KUJIVUNIA ULICHOPATA KWA KUANGALIA HIZI PICHA? 

CHUKUA LEO HATUA YA KUACHA ILI KUEPUKA MADHARA YATAKAYOKUJA KUTOKEA SIKU ZIJAZO.


WEKA NIA, UNAWEZA.



Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

22 comments:

Unknown

ahsante kwa somo lako.. mana mm mdau sana hizo picha na huwa natamani kuacha ila kila siku kesho hadi afya yangu ya mwili inazidi kuzorota, nazidi kukonda.. kuanzia sasa naamua mm kama mm naacha rasmi kupitia njia ulozitaja

Unknown

Da!!! Vijan wenzangu tuache haka kamchezo wise...

Alex wambui

Naacha Sasa izi picha kiukweli nasema nita acha ila kila siku najikuta nazi tazama ila kwasasa naacha kwanjia ulizo nielekeza

Unknown

Asante Naminaacha leo Edu good

Unknown

Daah inahitaji kuomba Mungu sana pia...
Sema nimependa sana picha mlizotumia kwenye kila article asee zinasadifu kabisa kila mlichoongea๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†

kamlinzi

https://www.jw.org/sw/maktaba/magazeti/wp20130801/je-ponografia-ina-madhara/

Gazeti hili linahabari nyingine ambazo zinaweza kusaidia mtu kupambana na pronograpgy. Asante kwa makala yenu

kamlinzi

https://www.jw.org/sw/maktaba/magazeti/wp20130801/je-ponografia-ina-madhara/

Gazeti hili linahabari nyingine ambazo zinaweza kusaidia mtu kupambana na pronograpgy. Asante kwa makala yenu

Unknown

Duh Kuna utamu fulani husikika lakn kuanzia sasa sihusiki Teena na hii kitu ijapo mm wanawake wananikataa saana ndo maana nkachagua hii kama njia sahihi ya kupunguza hisia zangu kumbe sio nzr kwa Maisha yangu ya baadae,,!!Eee mungu baba Nisaidie naacha.

Anonymous

Change start now

Unknown

Kweli ata mm paka naumia nikuamua kurudi kwa mungu na kutubu

Unknown

Namshukuru Sana kwa ushauri wako Mana nilikuwa najiuliza nitatokaj

Unknown

Ebana munguh akubakubari Sana, jazakallahu khayra

Unknown

Ebhana mungu akubariki Sana jazakallahu khayrah๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™

Anonymous

Dah me kwng inakuwa shda sana mbona

Anonymous

Bro asante sana na mm naacha kuanzia leo … ewe mungu wangu niongoze ๐Ÿ™๐Ÿป

Anonymous

Mbn mm kila ciwez jmn kwann

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz