16.UNADHANI KITU GANI NI KIGUMU ZAIDI KUWA MTENDAJI MKUU?

Hapa jikite zaidi katika mipango, utekelezaji, na gharama za usimamizi.
Elezea kuwa kazi kubwa kwa mtendaji mkuu ni kuwafanya wafanyakazi wake kufanya kazi kulingana na mipango ya ofisi, kuitekeleza kazi hiyo katika muda uliopangwa na pia ikamilike ikiwa imetumia bajeti iliyopangwa.

17.UNAUONAJE MWENENDO WA SOKO LA SHUGHULI ZETU?

Jiandae na vitu viwili au vitatu kuhusiana na mwenendo wa soko, na uonyeshe jinsi gani unalifahamu soko vizuri.
Unaweza ukagusia suala la changamoto za teknolojia au fursa, hali ya uchumi na hata mahitaji ya mamlaka zinazosimamia soko ili kuonyesha ni wapi soko la shughuli zenu linapoelekea.

18.SABABU GANI ZIMEKUFANYA UIACHE KAZI YAKO NA KUJA KUTAFUTA MPYA?

Elezea kwa kifupi sababu zako, kuwa mwaminifu pia bila kujiumiza wewe mwenyewe.
Waeleze kuwa kuondoka huko ulikuwa ni uamuzi wako, na wewe ni mtu wa kupenda kutafuta changamoto mpya na umeona sehemu sahihi ya wewe kuzipata ni hapa kwao.
Usije ukaelezea matatizo yako binafsi hapa, kwani unaweza ukajiharibia. Wanacholenga wasaili katika hili swali ni kujua kama ulifukzwa au uliondoka mwenyewe.

19.UMEJISIKIAJE KUACHA FAIDA ZA MAKATO YAKO KWA KUACHA KAZI ULIKOTOKA?

Waambie kuwa kiuhalisia uliguswa, lakini hukuwa na hofu.
Waambie kwamba ulikuwa tayari kuacha faida zote ili ukapate mazingira sahihi ya kazi ili uonyeshe kuwa maslahi si kipaumbele cha wewe kuajiliwa na wao.

20.KITU GANI ULIKUWA UNAKIPENDA, NA ULICHOKUWA UKIPENDI KATIKA KAZI YAKO ILIYOPITA?

Kuwa mwangalifu wakati wa kujibu hili swali, uwe na mtazamo chanya zaidi kwa kuelezea vitu vingi ulivyokuwa unavipenda kuliko ulivyokuwa unachukia.
Ukijifanya unataka kukosoa sana kazi uliyokuwa unafanya kabla ya kuja kuomba kwao, itawashangaza na kukuuliza kwanini uliendelea kubaki mpaka leo ndio uje kwao?

21.ULIKUWA UNAMUONAJE MKUU WAKO WA KAZI?

Hapa pia kuwa na mtazamo chanya, kwani hata kama mkuu wako hakuwa mwema kwako,
 ila jinsi utakavyomzungumzia kwa kuponda ndivyo muajili wako mpya atahisi utamfanyia yeye siku zijazo.

22.KWANINI UNAHISI HAUJAVUNA SANA KATIKA UMRI WAKO HUU?

Hapa waambie sababu moja kuu, ya kuwa ndio maana umekuja kwao kutafuta kazi 
na kuwa unajua thamani yako itapanda kupitia wao.
Usianze kujitetea sana hapa mpaka ukawaonyesha kuwa huna mipango mizuri na maisha yako.

23.UNADHANI KWA NAFASI UNAYOOMBA ULIPWE KIASI GANI?

Huu ni mtego mkubwa sana kwa wewe unayeomba kazi, unatakiwa uwe unafahamu viwango vya mishahara ya majukumu kama yako.
Endapo huyajui majukumu ya kazi yako, unaweza ukawauliza hapo hapo ili ukishayafahamu ndio uwatajie kiwango unachotaka.
Usije kujirahisisha au kujipandisha sana hapa, kwani nao wanaangalia kama uko kimaslahi zaidi  kuliko majukumu utakayopewa.
Au kuwatega na wewe, kama uliacha ajira mahali unaweza ukawaambia kuwa ulikotoka ulikuwa unalipwa kiasi fulani na ungependa kuona kiwango kinapanda.

24.UNA MIPANGO GANI YAKO YA MUDA MREFU?

Hapa wala usijisumbue na maelezo mengi, gusia kwa kifupi malengo yako ukiyahusianisha na malengo ya kampuni unayoomba.

25.UMEFANIKIWA KWA KIASI GANI MPAKA SASA?

Waeleze kuwa unajivunia na jinsi ujuzi wako unavyokua siku hadi siku.
Waambie pamoja na changamoto za kupanda na kushuka katika maisha lakini huna malalamiko na hatua uliyopo.
Hapa jionyeshe ni jinsi gani unajiamini na unafurahia unachofanya katika maisha yako.

HAYA NDIO MASWALI KUMI YALIYOKUWA YAMEBAKI AMBAYO NDIO HUWA YANAPENDWA KUULIZWA SANA WAKATI WA USAILI.

YAWEZEKANA KUNA MENGINE MENGI MAPYA UTAKUTANA NAYO LAKINI UNACHOPASWA KUFANYA NI KUJIANDAA KWA KUTUMIA PICHA ULIYOPATA KUTOKA KATIKA HAYA MACHACHE YA MIFANO.




Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz