Kwa wale ambao bado mnasoma, au mmemaliza hatua moja ya elimu na mnataka kuingia hatua nyingine maneno haya si mageni kwenu kukutana nayo.
Hebu leo tujuzane kwa ufupi tofauti zake na kuona jinsi ufahamu huu utakavyo tusaidia siku za usoni.
1.Shahada ya kwanza(Undergraduate):
Ni mahususi kwa wanafunzi waliomaliza elimu ya kidato cha sita(A level) na ambao bado hawajapata shahada ya chuo.

2.Shahada ya pili(Graduate):
Ni mahususi kwa wanafunzi ambao wameshapata shahada ya kwanza na wanataka kusomea utaalamu wa fani waipendayo.

Mwanafunzi yeyote wa elimu ya juu anapohitimu masomo yake anatarajia apate vitu viwili muhimu, kama ushahidi wa yeye kuwa alisoma na kufaulu hiyo kozi.
Vitu hivi humsaidia pale anapotaka kuomba kazi au kutaka kuendelea na elimu ya juu zaidi.

1.Nakala(Transcript):
Ni nakala rasmi yenye mkusanyiko wa taarifa za mwanafunzi, kuanzia kozi aliyosoma mpaka idadi ya masomo na alama zake ulizopata.
Unapotaka kuendelea na elimu lazima utaombwa uwasilishe na nakala hii.
Nakala(Transcript) inayotambulika ni ile inayotoka moja kwa moja kutoka chuo ulichosoma na ikiwa imepigwa muhuli wa chuo husika.

2. Cheti(Certificate):
Ni hati inayothibitisha kwamba huyu mwanafunzi alisoma kozi fulani na alifaulu idadi fulani ya majaribio aliyojaribiwa.

Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

1 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz