*Hii ni moja ya kituo cha mabasi hayo kitakavyokuwa*
Barabara za mradi huu hatua ya kwanza zitakuwa na urefu wa kilometa 20.9, vituo vidogo 29 (ina maana wastani wa kituo kidogo kwa kila kilometa moja), Vituo vikuu 5 na sehemu za maegesho zitakuwa 2.
Ramani hii inaonyesha vituo vikuu vitakuwa ni Kimara(Mwisho), Ubungo, Kariakoo, Ferry(Kivukoni) na Morocco.
Katika vituo hivyo vikuu 5, vituo 2 kati ya hivyo, cha kutoka kimara hadi kariakoo na Ubungo hadi Kivukoni mabasi yatakuwa hayarembi mwendo(Express) katika kupeleka watu kati kati ya jiji ambako ofisi ni nyingi.
Baada ya hatua ile ya kwanza ya kilometa 20.9 kukamilika wataingia hatua 5 zilizobaki ili kufanya jiji zima la Dar liwe na mradi huu wa mabasi yaendayo kasi kama ramani ya hapo juu inavyoonyesha.
Maeneo ambayo mabasi hayo yatakuwa yanaegeshwa ni Ubungo na Kariakoo.
Vituo vidogo vitakuwa Kimara Resort, Kimara Thomas, Kimara Baruti, Kibo, Chai Bora, Shekilango, Urafiki(Mahakama ya ndizi), Manzese Tip Top, Bakhresa, Argentina, Magomeni Kagera, Mwembe Chai, Usalama, Mapipa, Jangwani, Fire, Kariakoo Sokoni, Mtaa wa uhuru, Bibi Titi, City council, National bank,
Kinondoni A, Kanisani, Mwinyi Juma, Kinondoni Mjini, na Dunga.
Wewe mkazi wa Dar unahisi mpango huu utasaidia kupunguza foleni katika jiji la Dar es salaam lenye shughuli nyingi za kiuchumi?
0 comments:
Post a Comment