Haya ni makosa ambayo
tunayafanya bila kujua,
kwasababu
katika muda huo,
tunakuwa hatuna njia ya kumfanya aliyeondokewa na mali au mtu ajisikie tuko pamoja naye katika machungu.
Na kwakuwa
ni vigumu kwa muhusika kukueleza kwamba nataka kufanyiwa
au kuambiwa kitu fulani ndio nitajisikia vizuri,
inakubidi utumie ujuzi wako binafsi
kutafuta njia ya kumfanya
ajisikie vizuri.
Hapo sasa balaa ndio linaanza,
kwani mara nyingi
maneno tunayochagua kumwambia
aliyepotelewa hayamfanyi ajisikie poa
bali yanamfanya aanze kutafakari ulikuwa na maana gani.
Na hii inatokana
na si wote wana uwezo wa kutafakari
kauli zinazotolewa
na watu wengine katika
mtazamo chanya.
Hebu tuangalie maneno ambayo hupaswi kuyasema kwa muhusika:
1."Shukuru (ameishi/umeishi nacho) miaka mingi"
Unapoongea kauli kama hii inampa picha
mtu huyo,
kwamba jambo hilo
lilipaswa kutokea kwake,
na hivyo hapaswi kuhuzunika.
Yawezekana kuna ukweli ndani yake,
lakini
unapoongea mbele ya muhusika haitamfanya ajisikie vizuri.
2."Muda wake ulifika"
Hata kama umekosa la kuongea hii kauli
sio kabisa,
itamfanya akuone umefurahia
tukio hilo.
3."Alikosea/Ulikosea sana ku.... "
Ikiwa tukio lilikuwa la ajali,
hata kama liliempata alisababisha
usiongee kauli kama hii
kwa muhusika,
itaonekana kana kwamba alifanya uzembe na alistahili kupatwa na hilo.
4."Kuna sababu ya kila kitu"
Hii kauli kweli ina maana,
unapofikiria kwa kina lakini si nzuri kuizungumza
kwa mtu aliye kwenye
majonzi.
5."Usihofu utampata mwengine tu"
Ikiwa mtu amepoteza mtoto,
mume au mke,
kauli ya kumwambia kwamba
asihuzunike na kuwa
atapata mwengine tu,
itamfanya aone hukuwahi kuona umuhimu wa aliyeondokewa naye,
na ulikuwa unaombea hilo litokee.
Mara nyingi maneno haya yanapotamkwa na muhusika yanakuwa na
matumaini zaidi kuliko yanapotamkwa na mtu mwengine wa pembeni.
Ni heri utumie maneno kama:
1."Pole sana kwa yaliyotokea"
2."Natamani ningekuwa na maneno mazuri ya kukueleza ujisikie vizuri"
3."Niko pamoja nawe katika hili"
4."Niko pamoja nawe katika sala"
5."Tulimpenda wote"
6."Ukihitaji msaada, niko hapa kwa ajili yako"
TABIA YA KUWAFARIJI WENZETU WANAPOPATWA
NA MATATIZO,
NI NZURI SANA NA ITAWAFANYA
WAJISIKIE VIZURI.
KWELI YAWEZEKANA UNA TAFSIRI YAKO
MOYONI JUU YA TUKIO
LILILOTOKEA,
LAKINI IWEKE MOYONI UKIONA HAITAMFARIJI MUHUSIKA.
WOTE TUNAWEZA KUWA TUMAINI KWA WENGINE
PALE WANAPOPATWA NA
MATATIZO
KWA KUTUMIA MANENO NA NJIA SAHIHI
KUELEZEA HISIA ZETU PIA.
0 comments:
Post a Comment