Kitu pekee duniani, ni kuwa kila binadamu amepewa uwezo wa kufanya kitu cha pekee ndani yake,
lakini hautaambiwa unaweza kufanya nini mpaka wewe mwenyewe utafute.
Hautakuja kujua wewe ni
mzuri kwenye kitu gani kama huna tabia ya kujaribu vitu tofauti tofauti.
Ukichukua hatua ya kutafuta wewe unaweza kufanya kitu gani kwa ufanisi utajishangaa mwenyewe,
kwani utajikuta unaweza kufanya vitu ambavyo mwanzo ulikuwa unaona haiwezekani kwako.
Yawezekana kabisa kuna kitu huwa unatamani kufanya na unadhani hautaweza,
ukweli ni kuwa hautajua kama huwezi au unaweza mpaka ujaribu.
Watu wote waliofanikiwa katika maisha yao nao pia hawakuwa na uhakika kama wanachofanya watakiweza,
lakini kwa kujaribu wakajikuta wanaweza na kufurahia.
Unapofanikiwa kutambua kipaji chako ni nini,
ndio muda utakaoona utamu wa maisha yako ulipo,
kwani utafunguka macho na kuanza kuiona dunia katika mtazamo tofauti
na uliokuwa nao mwanzo.
Na hii inatokana na siku zote kitu unachoweza kukifanya vizuri ndio kitakuwa kinabeba furaha yako ya kila siku.
Sasa jaribu kufuata hizi hatua uone jinsi gani zitakusaidia kutambua kipaji chako:
1.CHUNGUZA UNAFURAHI SANA UKIFANYA NINI:
Sehemu nzuri ya kuanza kujitafuta ni kutafakari wewe mwenyewe kitu gani ukifanya unafurahia sana
huwa unaomba muda usiishe.
Lakini angalizo;
kiwe kinakubalika na jamii.
Kama unapenda kitu fulani sana acha kung'ang'ania kuwa shabiki,
hebu anza na wewe kufanya uone kitatokea nini.
Ushahidi upo wa watu wengi waliokuwa mashabiki wa muziki,
maigizo, na hata mpira walipoamua kujitoa katika ushabiki
walikuja kuwa na mafanikio makubwa kupitia fani hizo.
2.JIFUNZE KITU KIPYA:
Hata kama kwa sasa kuna kitu unajishughulisha nacho,
jaribu kufanya na shughuli nyingine ambayo utapata changamoto mpya na kuongeza ujuzi mwengine.
Hakuna ambaye anapenda afanye kitu katika mazingira magumu,
ukitoka katika mazingira hayo kutafuta mapya utaona mabadiliko yako.
Hautaweza kugundua kipaji chako kama utaendelea kun'gang'ania mazingira magumu na kuogopa kujaribu kitu kipya.
3.TEMBELEA MAENEO MAPYA:
Yawezekana maeneo unayoishi shughuli fulani ndio maarufu sana,
na wewe unajihusisha nayo kwa kuwa hakuna nyingine ya kufanya.
Kwahiyo unapoenda mazingira mapya utafanya akili yako ifunguke kuona fursa ya kujifunza vitu vipya.
4.SOMA HABARI MBALI MBALI:
Kusoma habari mbali mbali ziwe za mtu au mazingira fulani,
zitakufanya kupata uzoefu wa kutambua vitu vipya.
Vitu hivyo ambavyo mwanzo hukuwa na uelewa navyo.
Tabia hii itakujengea hamu ya kutaka kufahamu vitu zaidi,
na hivyo itakupunguzia uoga wa kujaribu mambo mapya.
Hasa hapa www.lishaubongo.blogspot.com lazima utabadilika mtazamo na utajitambua.
5.HUDHURIA SEMINA FUPI FUPI:
Ukiwa una tabia ya kuhudhuria semina
utakuwa unafungua ubongo wako
kulishwa mambo mapya na kukujengea mazingira ya kujitambua.
Usiogope kuingia gharama kulipia semina
ambayo inaweza kukusaidia wewe
kuja kuishi maisha ya furaha siku zote.
6.ULIZA MARAFIKI:
Mara nyingi mwenye kipaji ni ngumu kukitambua yeye mwenyewe,
kwa kuwa siku zote yeye anaona anafanya kitu cha kawaida.
Lakini watu wa pembeni ndio wanaochizika na kile anachofanya.
Kama una marafiki ambao mna upendo kwa kila mmoja hawatokuficha kipi wanakifurahia kwako unapokifanya.
Shikiria hapo sasa.
7.CHAGUA MTU WAKO WA MFANO:
Katika maisha kama wewe unapenda kitu fulani kinachofanywa na binadamu,
lazima kuna mtu mmoja ambaye anapofanya hicho kitu wewe anakufurahishwa sana,
na unatamani kuwa kama yeye.
Angalizo,
siyo lazima uje kufanya anachofanya yeye lakini unaweza ukachukua
ari yake na juhudi ya ufanyaji ukawekeza katika shughuli unayopenda wewe.
9.JIUNGE KATIKA VIKUNDI:
Kuna vikundi mbali mbali vya vijana vinajishulisha na
shughuli tofauti tofauti unaweza ukajiingiza huko na kujifunza
vitu usivyoweza.
10.TAFAKARI KILA UNACHOANGALIA NA KUSIKIA:
Wengi wetu tumekuwa mashabiki wa filamu, muziki au hata habari za uchunguzi katika televisheni na redio.
Lakini si kila unachosikia na kuangalia hakuna cha kujifunza,
naamini mpaka umepata nafasi ya kusikiliza na kuona basi ujue kuna kitu
unatakiwa ujifunze.
Usikubali kuendelea kuishi na taarifa zile zile kila siku,
anza kujifunza mpya sasa.
NAJUA KUNA WENGI WETU TUNASEMA HATUNA KIPAJI CHOCHOTE,
LAKINI AMINI LEO KWAMBA HAKUNA AMBAYE HAJAUMBWA NA KITU CHA PEKEE CHA KUMFANYA AYAFURAHIE MAISHA YAKE.
HUJACHELEWA ANZA SASA KUJICHUNGUZA NA FANYIA KAZI UTAONA UPANDE SAHIHI WA MAISHA YAKO.
0 comments:
Post a Comment