1. MUDA GANI WA SIKU HUWA UNAJISIKIA VIZURI ZAIDI
a.Asubuhi
b.Muda wa mchana na mapema jioni
c.Usiku sana
2. MARA NYINGI UNATEMBEA...
a.Haraka na hatua kubwa
b.Haraka na hatua fupi
c.Taratibu huku umenyanyua uso juu
d.Taratibu na uso umeinamisha
e.Taratibu sana
3. UNAPOONGEA NA WATU HUWA...
a.Umesimama huku umekunja mikono
b.Mikono yako imeshikwa
c.Mkono wako mmoja au yote ipo mdomoni
d.Unamgusa au unamsukuma
e.Unachezea sikio, kidevu au nywele
4. UNAPOPUMZIKA, UNAKAA HUKU...
a.Umeikuchanjanisha miguu yako
b.Umekunja nne
c.Umenyoosha miguu
d.Umekunja mguu mmoja chini yako
5.UNAPOFURAHISHWA NA KITU UNA...
a.Cheka kwa sauti kubwa
b.Unacheka lakini si kwa sauti kubwa
c.Unacheka kwa ndani tu
d.Tabasamu la aibu
6. UNAPOHUDHURIA SHEREHE, AU KWENYE MKUSANYIKO WA WATU UNA...
a.Unaingia kwa sauti ili ujulikane
b.Unaingia kimya, halafu unamtafuta unayemjua
c.Unaingia kimya na hutaki ujulikane
7. UNAFANYA KAZI NA UMEWEKA MAWAZO YAKO YOTE HAPO HALAFU MTU ANAKUJA KUKUSUMBUA
a.Unakatisha kazi
b.Unachukia
c.Inabadilika kati ya hali hizo juu
8.AINA IPI YA RANGI UNAIPENDA SANA KATI YA HIZI
a.Nyekundu au machungwa
b.Nyeusi
c.Njano au blue mpauko
d.Kijani
e.Blue iliyo koza au zambarau
f.Nyeupe
g.Kahawia au kijivu
9.UNAPOKUWA KITANDANI USIKU, KABLA HAUJAPITIWA NA USINGIZI HUWA UNA...
a.Unalalia mgongo huku umejinyoosha
b.Unalalia tumbo
c.Kiupande upande halafu umejikunja
d.Umelalia mgongo kichwa juu ya mkono mmoja
e.Kichwa unakifunika na shuka
10. MARA KWA MARA UNAOTA...
a.Unaanguka
b.Unapigana au unahangaika
c.Unatafuta kitu au mtu
d.Unapaa au unaelea
e.Huwa hauoti kabisa
f.Una ndoto za furaha tu
ALAMA KWA KILA JIBU(UKITAKA USAHIHI WA SIFA YAKO USIBADILI MAJIBU ACHA KILE ULICHOCHAGUA)
1.(a)2(b)4(c)6
2.(a)6(b)4(c)7(d)2(e)1
3.(a)4(b)2(c)5(d)7(e)6
4.(a)4(b)6(c)2(d)1
5.(a)6(b)4(c)3(d)5(e)2
6.(a)6(b)4(c)2
7.(a)6(b)2(c)4
8.(a)6(b)7(c)5(d)4(e)3(f)2(g)1
9.(a)7(b)6(c)4(d)2(e)1
10.(a)4(b)2(c)3(d)5(e)6(f)1
Sasa jumlisha idadi ya alama zako halafu angalia jumla yake inaangukia katika sifa ipi kati ya zifuatazo:
JUU YA ALAMA 60:Wengine wanakuona kuwa mtu wa kukuchukulia tahadhari sana,wanakuona unajikubali sana, wengi wanapendezwa na wewe na wanatamani kuwa kama wewe lakini hawakuamini, wanasita kujihusisha na wewe moja kwa moja.
ALAMA 51 MPAKA 60:Wengine wanakuona mtu uliyejawa na shauku, unayebadilika ghafla na kukurupuka bila kufikiri; kiongozi wa asili, uko haraka kufanya maamuzi japo mara nyingi siyo sahihi. Wanakuona unajiamini sana na sio wa kawaida, usiyeogopa kujaribu kitu kwa mara ya kwanza, unayechukua nafasi na kufurahia ujasili wako. Watu wanafurahi kuwa sehemu ya maisha yako kwasababu ya furaha unayowaletea.
ALAMA 41 MPAKA 50:Watu wengine wanakuona kama mtu mpya, mwenye uhai, mcheshi, unayefurahi, mtu wa vitendo, na mara nyingi ni mtu wa kushangaza; mtu ambaye mara nyingi unavuta usikivu wa watu na hupendi wajue kwamba huwa unavuta usikivu wao. Pia wanakuona mkarimu sana , unayejali na unayeelewa wengine; mtu ambaye mara zote unawafurahisha na kuwasaidia.
ALAMA 31 MPAKA 40:Wengine wanakuona mjanja, muangalifu, makini na mtu wa vitendo. Wanakuona una akili sana, una kipaji, na usiyejisifia. Siye mtu anayetengeneza marafiki kwa haraka au kwa urahisi,lakini wanakuona kama mtu unayekuwa muaminifu katika urafiki na unayependelea pia uaminiwe. Watu wengi wanaobahatika kuwa na urafiki na wewe wanagundua ni ngumu sana kuondoa uaminifu wako kwao, na hivyo hivyo huwa ngumu kwako kuurudisha uaminifu uliovunjika.
ALAMA 21 MPAKA 30:Marafiki zako wanakuona kama mtu jasili na pia ni mgumu kufurahishwa. Wanakuona mtu wa tahadhari sana, muangalifu kupitiliza, mtaratibu lakini mwenye vishindo vizito. Inawashangaza sana unapofanya vurugu za kushtukiza, wakitarajia utakaa kufikiri kabla hujachukua maamuzi juu ya tukio husika.
ALAMA CHINI YA 20:Watu wanakuona ni mtu wa aibu sana, mwenye hofu nyingi, unayepaswa kuangaliwa kwa karibu, ambaye mara nyingi unategemea watu wengine wafanye maamuzi kwa ajili yako na ambaye hutaki kujihusisha na kitu au mambo ya mtu mwengine.Wanakuona kama mtu muoga unayeogopa vitu visivyokuwepo. Watu wengine hukuona unachosha sana.
1 comments:
kuna ukweli sana tu
Post a Comment