Mtandao wa kijamii wa Facebook,
 ndio umetokea kuwa mtandao wa kijamii wenye mashabiki wengi kuliko wowote uliowahi kuanzishwa.

Wewe uliyejiunga,
 katika mtandao huu utajikuta unakutana na watu uliopotezana nao
 miaka mingi iliyopita,
 na wengine wapya ambao haungezani kama utawahi kuwasiliana nao.

Kati ya watu hawa utakao kutana nao wengine wanakuwa na tabia za ajabu mpaka muda mwengine wanaumiza kichwa.

Hebu soma hapa uzijue hizo tabia kama haujakumbwa na balaa hizo basi ujipange.

1.KUWEKA UJUMBE WA AINA MOJA MARA NYINGI KATIKA UKURASA WA MTU
Kitu chochote kinapozidi kiwango huwa kinachefua hata kuangalia, 
hata kama unamjali mtu 
huwezi kuweka ujumbe mmoja 
mara kibao utakuwa unamfanya apoteze 
ladha ya ujumbe.
We mtu anaposti"duh!"x10 hadi inachosha kusoma.

2.KU'LIKE' STATUS ZA HUZUNI

Yaani hata kama unashindwa kutofautisha habari za huzuni na furaha 
basi fikiria kabla huja'like'.
We mtu amepost picha ya
 marehemu ndugu au mzazi
 halafu wewe una'like',
ni heri uandike kitu kuliko 'like'

3.KUPOSTI KILA DAKIKA KITU UNACHOFANYA

Utakuta mtu anapoamka asubuhi anaanza kuposti:
"Ndio naamka sasa wadau/marafiki"
baada ya muda kidogo;
"Napiga chai na chapati hapa karibuni waungwana"
tena;
"Nasubiria basi pande hizi kwa manyanya teja ana kelele huyo"
halafu;
"Dah! naingia ofisini hakuna hata mtu"
halafu;
"Natamani muda wa chakula ufike nina njaa kinoma"
Nadhani watu aina hii ushakutana nao sana tu na wanachosha kwa kweli.

4.KUWEKA VITU BINAFSI KATIKA UKURASA WAKE
Lazima,
 utambue kuwa facebook ni mtandao wa kijamii kwa hiyo kila mtu 
anayefungua ukurasa wako awe rafiki asiwe rafiki ataona tu.
Sasa wewe,
 unaweka mapicha yako ya chumbani tena ukiwa umelala!! 
jaribu kutofautisha vitu gani vya kushirikisha kila mtu na vitu gani unapaswa kushirikisha watu wako wachache.

5.KUWEKA LUGHA ZA MATUSI
Lazima utambue,
 kuwa si kila mtu anapendelea kukutana na lugha za matusi juu
 ya ukurasa wako.
Yawezekana unataka kufikisha hisia zako kwa mtu fulani ni heri 
utumie njia nyingine lakini si 
kuweka matusi ya wazi juu.


6.KUWA'TAG' MARAFIKI PICHA CHAFU

Utakuta mtu anamtag rafiki yake,
 picha chafu zisizofaa katika ukurasa wake,
hata kama wewe
 hakuna watu wa heshima wanaofungua ukurasa wako,
 jua kuna wengine wazazi wao wanafungua kurasa zao wanapokutana 
na hizo picha unafikiri
 wanapata picha gani?

7.KUPOSTI KATIKA UKURASA WAKO STATUS NDEFU KINOMA

Ni heri hata kama unaichukua mahali hiyo status,
 jua kuichuja basi kuliko unaposti status kama insha'
 unategemea nani anamuda wa kusoma status ndefu hivyo 
jali muda wa wenzako.
Ndio maana mwengine kabla haijamliza kujua maana yake analike tu bila kujua maana yake,
eeh!eeh! ushamchosa hivyo.

8.KUTAKA KUCHAT NA MTU KILA UNAPOMUONA HEWANI

Si kila wakati,
 mtu anaingia facebook kutaka kuchat na watu, kuna muda, 
anakuja kuchati na mtu maalumu,
 lakini wewe unalazimisha kuchati 
naye kila wakati,
 unaandika 
tu maujumbe mengi 
ukiona hakujibu.


JAMANI  HUU NI MTAZAMO,
 TU JARIBU KUCHUJA VITU VYA KUFANYA KATIKA UKURASA WAKO NA WA WATU WENGINE.
  ILI USIPOTEZE MARAFIKI KWANI RAHA YA MTANDAO WA KIJAMII NI KUWASILIANA NA WATU.

WATU WENGI TUPO KATIKA MKUMBO HUU, TUJIREKEBISHE BASI ILI MAISHA YA FACEBOOK YAWE MAZURI KWA KILA MMOJA WETU.

Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz