Mtu wa mfano,
ni yule ambaye tabia yake mbele ya jamii husika inakubalika na
wengi wanatamani
kuwa kama yeye.
Mtu huyu,
huwa anaangaliwa kama mfano pale watu mwengine wanapotaka
kufanya majukumu fulani;
iwe ya uwanafunzi, urafiki, ujirani,
kazini, au sanaa na
hata michezo.
Yawezekana kila mmoja wetu
ana mtu wake anayemuangalia
kama mtu wake wa mfano.
Hasa mtu anapokuwa katika rika
la kuanza kujitambua,
mara nyingi
huanza kwanza kuvutiwa na sifa za watu wengine anaowaona
kila siku.
Na ndio maana,
unatakiwa kuwa makini sana
mtoto wako kipindi cha ukuaji,
anachangamana au kuwaangalia watu wa aina gani.
Kwa mtoto,
haitajalisha huyo mtu aliyevutiwa naye anafanya jambo jema au baya.
Kama amevutiwa jinsi anavyofanya
na yeye
atataka kuwa kama huyo mtu
kwa kufuata njia zake.
Unapobahatika kuvutiwa na mtu,
na ukamchagua kuwa
mtu wako wa mfano,
anaweza kuwa
chanzo cha wewe kufikia mafanikio
fulani unayotamani
kuwa nayo.
Ikiwa mtu wako wa mfano yuko
karibu na mazingira yako
unaweza ukafanya hili:
1.TAFUTA NAFASI YA KUZUNGUMZA NAYE
Hii ni hatua ya kwanza,
unaweza kuitumia
kumfahamu mtu wako wa
mfano kiundani njia alizopitia
kuwa hapo alipo.
Usifiche hisia zako kumueleza jinsi gani unavutiwa na tabia yake na
ungependa kuwa
kama yeye.
Hiyo itamfanya ajisikie vizuri,
na akupe ushirikiano,
kwa kuwa kila binadamu anapenda
awe anavutia wengine.
*USIMUULIZE MASWALI MAGUMU
Unapopata nafasi,
ya kuzungumza na mtu wako
wa mfano haina maana kwamba,
amekuamini vya kutosha
kukuelezea kila kitu
kuhusu njia alizopitia.
Ila,
kuwa na maswali mepesi
ambayo yatamfanya yeye wakati anakuelezea aguse
eneo ambalo wewe haungeweza
kumuuliza kwa urahisi.
Hata kama haujakutana naye
uso kwa uso lakini umeweza kuwasiliana naye kwa njia nyingine
za kieletroniki,
kuwa makini katika
kuuliza maswali.
*JENGA SHAUKU
Njia yoyote ya kujifunza jambo,
kwa ufanisi ni kuweka shauku ya
kutaka kujua zaidi,
wakati unazungumza naye hata kama kuna kipengele unaona hakija
kuvutia tengeneza shauku ili upate
kujifunza zaidi
kutoka kwake.
Yafuatayo ndio unapaswa kufanya baada ya kuchagua mtu wako wa mfano:
1.IGA MEMA ANAYOFANYA/ALIYOFANYA
Usitarajie kwamba,
kila tendo analotenda mtu wako wa mfano ukilifanya wewe pia
litakuwa jema.
Yawezekana
mtu wako wa mfano umesoma
njia zake alizopitia kupitia
maandishi na wala sio
kutoka mdomoni mwake,
unapaswa utambue
jamii zinatofauti ya kutafsiri
matendo.
Kama ni rafiki kwa kila mtu,
na wewe kuwa hivyo,
kama ni mtu wa kutabasamu,
nawe fanya hivyo,
na kama anasaidia watu na wewe usisite
kufanya hivyo pale
unapokuwa na uwezo huo.
2.SOMA WASIFU WAKE MARA KWA MARA
Unapokuwa na tabia ya kusoma
wasifu wa
mtu wako wa mfano,
itakusaidia kufahamu kwa nini
aliweza kufanya
anachofanya sasa.
3.TAFUTA MTU WAKE WA MFANO ALIKUWA NANI
Hii itakusaidia,
kujua kuwa yeye aliweza
kiasi gani kufanikiwa kupitia mtu
wake huyo wa mfano na
tofauti yao iko wapi.
Kila mmoja wetu anaweza kuwa mtu wa mfano katika jamii yake kwa kufanya yafuatayo:
1.JITAMBUE
Ukitaka kuwa mtu wa mfano,
katika jamii yako
ni lazima kwanza
uwe wewe umejitambua.
Unataka kuwa nani na kwa nini.
Hii itakupelekea ufanikiwe katika yule unayetamani kuwa.
Hii itawafanya wanaokuangalia wapate
shauku ya kutaka kujifunza
zaidi kupitia wewe.
2.KUWA NA MSIMAMO
Kama umechagua kufanya jambo fulani,
na jamii ikajua wazi
kwamba wewe unafanya hilo jambo
usiwe kigeu geu.
Utawachanganya watu
wasijue unataka nini hasa.
Kama ulichagua siasa
na ukakutana na ugumu
endelea kupambana mpaka upate suluhisho
sio ugumu kidogo tu
ushabadilisha msimamo.
Hakuna mtu atakaye tamani
kuwa na mtu wa mfano asiyejielewa.
3.ISHI NDOTO ZAKO
Kama ulitamani siku moja
ukipata kitu fulani ndio
roho yako itafurahia,
ukipata huo uwezo usisite
kufanya hilo.
Kwani
utawafanya watu
wengine waone wewe ni
mfanikishaji ndoto hivyo
unapaswa kuigwa.
4.SAIDIA WATU WENGINE
Chagua kuwa mtu mzuri,
na wa msaaada kwa watu wengine.
Wapokee wengine
maishani mwako.
Ukipokea watu vile walivyo
utawafanya wajione wana thamani
mbele yako nao pia watatamani
kuwa kama wewe.
5.TIMIZA MAJUKUMU YAKO
Kama ni mzazi,
fanya mazungumzo na watoto wako
na kufuatilia maendeleo yake/yao
ya kila siku na
pia
majukumu mengine ya familia
itawafanya watoto wako
wasiende nje kutafuta
watu wengine wa mfano bali
utakuwa wewe mzazi wao ndio mtu wao wanayetamani kuwa.
Kwani hulka ya binadamu siku zote ni kuwa shujaa.
HEBU TUANZE LEO KUWA AINA YA WATU AMBAO WENGINE WANAWEZA KUIGA
YALE TUNAYOYAFANYA.
USIKUBALI KUIACHA DUNIA HII HUKU WATU WAKISHUKURU KUONDOKA KWAKO.
0 comments:
Post a Comment