"Je, niko katika njia sahihi?"
Kama,
umewahi kujiuliza hili swali,
uko karibu
kuipata njia yako sahihi.
Wengi,
tunajihusisha katika shughuli mbali mbali bila kujua
kama njia tunayoifuata/tuliyochukua
ni sahihi au
si sahihi kwetu.
Ulishawahi kuamka usiku mnene,
huku ukijiuliza kama njia uliyaochagua ni sahihi kwako au la?
Wengi tunajiuliza,
kuwa njia sahihi maana yake ni nini?
Kujiuliza swali hili,
ni hatua kubwa sana
kupiga katika maisha yako ya
kutafuta shughuli sahihi ya kufanya.
Fahamu wazi,
kuwa unaanza kujitambua,
na ni ishara mojawapo ya kujua
mahitaji gani ni muhimu kwako.
Yawezekana,
ukawa unalipwa vizuri,
una mazingira mazuri ya kazi,
au una
vifaa vyote vya kufanyia kazi zako.
Linapokuja
suala la upo sehemu sahihi au
sio sahihi
masuala hayo niliyotaja hapo juu
huwekwa kando.
Ishara za kuangalia kama upo njia sahihi katika shughuli unayofanya:
1.MUDA HAUKUTOSHI
Unapokuwa unafanya hiyo shughuli,
unaona muda kama unapaa.
Kwa kuwa
kwako si kazi tu bali unafurahia
kila dakika ya
kitu unachofanya.
Na unapokuwa mbali
na shughuli yako au
hata ukiwa umelala unatamani asubuhi ifike ili urudi tena eneo lako la kazi.
2.UNAPOTEZA MUUNGANIKO NA MATUKIO YA NJE YA KAZI
Unapokuwa mzigoni unahisi kama unasafiri dunia ya kipekee,
na unapoteza mawasiliano na dunia inayokuzunguka.
Unaweza ukawa unaongeleshwa na watu na usiwasikie kabisa,
kwa kuwa akili yako yote imetekwa
kwa muda huo na muda mwengine hata kula unasahau.
3.UNA IMANI NAYO MOYONI
Moyoni una imani kuwa
hii ndiyo kazi uliyoumbwa kuifanya na hakuna
atakayeweza kukubadilisha mawazo
na imani yako
uliyonayo juu ya shughuli hiyo.
4.UNA MAONO NA SHUGHULI HIYO
Una maono ya wazi kabisa ,
ya nini
unataka kupata baada ya muda fulani,
na hata kama kuna
vikwazo vinajitokeza bado
unanguvu za kutaka kufikia
lengo lako.
5.HAUKATI TAMAA
Hata kama kuna watu,
au mazingira
yanataka kukurudisha nyuma
bado hutaki kukata tamaa na
shughuli yako.
6.UNAFURAHIA CHANGAMOTO
Pamoja na changamoto zinazojitokeza
mara kwa mara
unafurahia uwepo wake kwani zinakupa
uzoefu mpya ambao mwanzo
hukuwa nao.
7.WATU WANAKUUNGA MKONO
Watu kadhaa watachukua muda wao,
kuwasiliana na wewe
ili kukupa msaada na muongozo wa
shughuli yako.
Hata wewe mwenyewe huelewi watu hawa wanakujaje katika maisha yako
lakini
wanakuja na msaada mkubwa sana kwako.
8.UNACHOFANYA KINALETA MABADILIKO YA KWELI KATIKA MAISHA YA WENGINE
Wewe unaweza ukaona
unachofanya ni kitu kidogo lakini kuna
watu kinawasaidia sana,
na mrejesho wao
utakupa picha halisi ya jinsi unavyogusa maisha ya watu wengine.
NI VYEMA UKAANZA KUJITAFAKARI SASA,
KAMA NJIA UNAYOTAMANI
AU ULIYOCHUKUA
NI SAHIHI AU LA.
HII ITAKUSAIDIA KUKUEPUSHA NA UPEPO USIO SAHIHI.
NA KUANZIA LEO,
TAMBUA KUWA NJIA SAHIHI
NDIO ITAKAYOKUPA MAFANIKIO YA KWELI KATIKA MAISHA YAKO.
0 comments:
Post a Comment