Moja ya sababu ya kutokielewa kitu unachofundishwa au unachosoma
mwenyewe ni
kukosa umakini.
Ikiwa umakini wako hauko katika unachojifunza,
yaani unafundishwa au unajisomea lakini unawaza kitu kingine,
unachojifunza kitaingia katika
kumbu kumbu fupi
na baada ya muda
kitaondoka zake.
Unaweza ukawa unasoma muda mrefu kuliko
mtu yeyote
lakini umakini
kama haupo hautapata
matokeo unayoyahitaji.
Yafuatayo huchangia kukosa umakini wakati wa kujifunza:
1.KUTOKUWA TAYARI KIAKILI KUJIFUNZA
*Kuwa na mawazo lukuki,
ambayo hayaendani na kitu unachotaka kujifunza.
2.KUKOSA SHAUKU YA SOMO LENYEWE
*Kutovutiwa na namna linavyofundishwa au lina mambo mengi sana.
3.KUSOMA NYENZO NGUMU
*Kusoma somo lenye lugha ngumu kuielewa au maelezo mengi na ambayo mpangilio
wake huuelewi.
4.KUKOSA HAMASA
*Kutojua baada ya kujifunza hilo somo litakuja kukusaidia nini katika
maisha ya baadaye.
5.KUKOSA LENGO MAALUMU
*Kutojua katika hilo somo,
unatakiwa ujue nini hasa
baada ya
kumaliza kulisoma.
6.KUSOMA ENEO LISILO NA UTULIVU
*Kukosa utulivu wakati wa kujifunza
kwasababu ya kelele nyingi na
usumbufu wa watu.
7.MATATIZO YA HISIA
*Kuwa na maumivu ya kihisia yanayokuzuia kufikiria vizuri.
8.KUCHOKA
*Kuhisi uchovu wa mwili unaokufanya
utake kupumzika.
9.KUWA NA MLUNDIKANO WA KAZI
*Kuwa na mlundikano wa kazi nyingi za
kufanya na hivyo kukupotezea
hamu ya kujifunza.
10.KUWA NA HOFU YA KUSHINDWA
*Hofu ya kushindwa inapokuingia inashusha hamu yako ya
kujifunza kabisa.
Sababu,
kubwa ya kukosa umakini
katika unachojifunza,
sio
kukosa kuvutiwa na unachosoma
bali ukiwa
na nia ya kukijua
lazima
umakini wako utakuwa hapo tu.
Ndio maana,
sifa moja wapo ya mwanafunzi bora,
ni yule
anayesoma kitu hata kama
kwa mara ya kwanza hakijamvutia ila anachotafuta yeye ni
kujua taarifa mpya.
Lakini,
unaposoma kitu ambacho wewe mwenyewe
unasema moyoni kuwa kinakuchosha
lazima ukione kigumu.
Kama unajiona umechoka au
hauko sawa
kihisia kujifunza ni heri usiingie hicho kipindi au
usisome hilo somo kwa muda huo hadi utakapokuwa sawa.
Kwasababu,
ni heri utumie muda mwingi
kuweka akili yako tayari kwa kujifunza kuliko
kupoteza muda mwingi
kujifunza kitu ambacho hautakielewa.
Unapokuwa sawa kiakili,
unatumia muda mfupi kuelewa unajifunza kuliko unapokuwa hauko sawa.
Haya ndio unaweza ukaanza kuyafanya
ili kuongeza uwezo
wako wa umakini wakati wa kujifunza:
1.Chagua eneo ambalo umelipenda kusomea
na hakuna vitu au shughuli
zitakazo kuchanganya;
2.Tengeneza ratiba maalumu utakayoifuata
ili iwe inakukumbusha
kutimiza wajibu
wa somo husika;
3.Hakikisha una nyenzo zote muhimu
ambazo
zinatakiwa wakati wa
kujifunza.
Sio ushaingia darasani halafu kalamu
huna,
utaanza kuingia
uvivu mapema sana;
4.Weka mawazo ya kuifanya kazi
uliyonayo vizuri,
kama ni kazi ya darasa
au mitihani;
5.Jikumbushie malengo yako ya kusoma
ni nini halafu soma
kulijibu hilo swali;
6.Jiwekee mapumziko mafupi mafupi
wakati unajifunza sio kufululiza muda mrefu bila mapumziko;
7.Andika muhtasari wa yale unayojifunza
na jikumbushie
mara kwa mara;
8.Jiwekee vituo maalumu wakati wa
kujifunza wewe mwenyewe.
Kama unasoma mada ndefu
weka lengo kwamba utaishia sehemu fulani, halafu ukianza tena
unandelea ulipoishia.
UJINGA SI KITU CHA KUKIFURAHIA KABISA,
KAMA KUNA KITU UNAPASWA
UKIELEWE HALAFU HAUKIELEWI,
NI VYEMA UKAFANYIA KAZI MAZINGIRA YAKO YA KUJIFUNZA.
NA KITU PEKEE,
NI KUAMSHA HAMASA YAKO YA KUJIFUNZA ILI UFIKIE LENGO
ULILOJIWEKEA.
0 comments:
Post a Comment