Kila siku katika jamii yetu,
kuna maelfu ya wanafunzi wanaogopa
kwenda shule.
Uonevu,
limekuwa ni tatizo kubwa,
hasa maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi
kama shuleni, vyuoni,
na hata maeneo ya kutafuta mkate wa kila siku(kazini/kibaruani).
Linaonekana kutokuwa na mwisho,
kwani wazazi,
walimu, na hata wakuu wa eneo husika
bado hawajui kinachoendelea,
au hawafahamu madhara yake na
wanayafumbia macho
matukio kama hayo.
Uonevu ni kitendo cha mtu
kutendewa isivyostahili
na mtu au kikundi cha watu
mara kwa mara,
kutokana na hali yake ya kimaumbile,
nafasi yake,
au hali yake ya maisha.
Sababu hizi tatu,
ndio kuu kabisa zinazoongoza kuufanya
uonevu
uwepo katika jamii.
Mara nyingi wanaowafanyia wenzao,
uonevu huu
huwaona hao wanaowafanyia kuwa
hawaendani nao;
kwa kuwa tu wengine wana aibu,
kipato kidogo,
hawafanyi matukio wanayofanya wao,
rangi tofauti,
dini tofauti,
au hata jinsia tofauti na wao.
Waonevu,
wanaweza kutumia maneno
au vitendo
kwenda kwa wanaowaona
wanyonge wao
ambao hata wakiwaonea hawawezi
kuwafanya kitu.
Kuna njia mbali mbali ambazo waonevu wanazitumia kutimiza azma zao
kwa mnyonge wao.
Na uonevu ambao
madhara yake yanaonekana kwa haraka
ni wa kimwili
kwani wengine huwapiga
wanyonge wao na kuwaumiza,
na wengine huwanyanyasa
kwa kuwashika maungo.
Uonevu wa maneno unaonekana
kuathiri
zaidi saikolojia ya
anayefanyiwa na ni mgumu kuonekana na wanajamii wengine.
Hapa waonevu hutumia njia mbali mbali kuwasilisha kwa muhusika
kwa kumteta,
kumtumia ujumbe wa kuumiza,
kumuandika vibaya katika kuta/ubao,
au kumsambazia
maneno ya uongo.
Siku za karibuni njia inayoonekana imeshika kasi
kutumiwa na waonevu ni
mtandao wa kijamii na
meseji za elektroniki.
Hivi unadhani anayeonewa anajisikiaje?
Kitu kimoja kikuu,
ni kuwa uonevu huwa haupokeleki kwa
yeyote anayefanyiwa.
Anaweza akavumilia siku za mwanzo
lakini
hali inapozidi kuwa mbaya
inawajengea hofu kali.
Anaweza kuvumilia kuitwa jina baya
au unyanyasaji wa kijinsia
mbele za watu siku za mwanzoni
lakini
ikiendelea inamuumiza sana
na inamjengea hali ya kumuogoga
sana mtu anayemfanyia
kitendo hicho,
na huingia kuathiri hadi maendeleo
yake ya shule,
afya au kazi.
Uchunguzi unaonyesha,
watu wanaofanyiwa uonevu
na wenzao
wana hatari ya kupata
matatizo ya afya ya akili,
kama kutojiamini,
msongo wa mawazo,
unyogovu, hofu,
au wengine huishia kujiua wenyewe.
Wanao waonea wengine
pia wako katika hatari,
kwani
anapoanza tabia hiyo
tangu akiwa mdogo
anapokua mkubwa huwa katika
kiwango kibaya zaidi
cha uhalifu.
Utafiti unaonyesha kuwa
katika kila watoto 4
waliowahi kujihusisha
na uonevu walikuja kuwa wahalifu wakubwa katika jamii zao wanapokuwa
na umri mkubwa.
Wengine huishia kukataliwa na wenzao
na kupoteza marafiki wengi
wanavyoendelea kukua,
na wanakuwa katika hatari ya
kukosa maendeleo mazuri
shuleni na kazini.
Waonevu wengi huwa na sifa zinazofanana:
1.Wanapenda kuwatawala wengine;
2.Wanapenda kujizungumzia wao tu;
3.Sio wazuri katika kuwasiliana na wengine;
4.Wanatawaliwa na mawazo mabaya kuhusu wengine;
5.Hawajali hisia za wengine;
Hii inatokana na wao
kujiona bora sana
kushinda watu wengine,
na wanajiona wana haki ya kuwafanyia wengine
wanavyotaka wao.
muda mwingine wanawafanyia wenzao hivi
kwa kuwa
wanajiona hawako salama.
Kwahiyo
wanatumia njia hiyo
kuwashusha wengine chini
ili wao waonekane juu na
wana nguvu zaidi.
Na wengine wanawafanyia hivyo wenzao
kwa kuwa tu
wao waliwahi kufanyiwa kwa hiyo
wanalipiza kisasi.
Na wengine huwa wana matatizo ya akili na kushindwa kuwa hisia za hatia,
huruma,
uelewa au majuto.
Na njia pekee ya kuwasaidia
ni kuwapeleka kwa daktari wa saikolojia, mshauri,
daktari wa magonjwa ya akili au
mwana ustawi wa jamii.
Ufanye nini kama unakutwa na hili tatizo:
*Kwa watoto wadogo,
na vijana wanaweza kulitatua kwa
kuwaeleza watu wakubwa
wanaowaamini.
Ni heri,
ukatoa taarifa mapema
kabla uonevu haujafikia kiwango
cha kuumizwa mwili.
Na mara nyingine,
anayefanyiwa uonevu anaweza akapata
wazo la kulipa kisasi
na hivyo njia atakayotumia
siku zote huwa ni mbaya na
inaweza ikaleta madhara makubwa
eneo husika.
Hebu tuangalie njia mabazo unaweza kuzitumia kupambana na uonevu wa kisaikolojia na maneno:
1.WAEPUKE WAONEVU;
Ni heri,
uonekane mjinga
kuliko kuruhusu maneno yao
yakufanye upoteze utu wako.
Nia yao ni kukuona wewe ukiumizwa
na ujumbe wanaokutumia
na ukiondoka watajiona hawajafanya kitu
na wewe hukuwajali.
Ukiendelea hivyo watajiona wajinga na watachoka kukuchokoza.
Tena ukiweza ondoka kwa mbwe mbwe za kutabasamu na mwendo wa kishujaa kumuonyesha kwamba huumizwi
na maneno yake.
2.SHINDA HASIRA ZAKO:
Yawezekana kabisa,
wakawa wanakupa maneno makali
na yakakuumiza sana,
na kuondoka hilo eneo haiwezekani basi jitahidi usionyeshe hasira mbele yao.
Kwani utawapa ushindi kuwa wamefanikiwa kukuumiza.
Wanachotaka ni kuzitawala hisia zako
na kwamba
wao ndio waamue muda huu ucheke
au muda huu unune.
3.USIANZE KUPIGANA:
Yawezekana kabisa,
hasira zimevuka kiwango na unaona huyo mtu unamudu kuzipiga naye
lakini hujui aliyekuchokoza kajipanga
vipi na yeye.
Kwani mara nyingi
wenye tabia hizi huwa hawana cha kupoteza washajikatia tamaa na hivyo
wanatumia muda wao kuharibu
maisha ya wengine.
4.ONYESHA KUJIAMINI:
Muonyeshe anayekuonea,
kuwa anachotaka ujisikie hakitawezekana
kwani unajitambua na
unaelewa unafanya nini
katika maisha yako.
Hata kama anazungumzia kasoro ya kimwili onyesha wewe kuwa unajikubali
vile ulivyo na kuwa maneno
yake ni kazi bure.
5.JISAHAULISHE MANENO YAO:
Huwezi kuzuia watu
kuongea maneno usiyapenda dhidi yako,
lakini
unaweza kuzuia yasikae
kichwani mwako.
Kama unajijua unapenda sana kitu fulani elekeza mawazo yako
huko muda mwingi.
6.ZUNGUMZA NA WAKUBWA:
Unaweza ukatumia muda wako
kuzungumza suala hilo na watu kama
washauri, walimu,
marafiki,
au yeyote unayedhani atakupa msaada unaohitaji.
Itakusaidia kupunguza hisia ulizonazo juu ya tukio hilo ukimuelezea.
7.USIOGOPE KUBADILISHA MARAFIKI:
Ukiona marafiki ulionao
ni kawaida yao kukuzungumzia vibaya
kwa umbea
fanya uamuzi wa kuwaacha na
kutafuta marafiki wengine ambao unaona hawana tabia kama hizo.
IKIWA WEWE UNAYESOMA MAKALA HII,
UKO KATIKA MAZINGIRA HAYO YA UONEVU,
CHUKUA HATUA SASA KUPAMBANA NA HALI HIYO
KABLA HAIJAKULETEA
MADHARA SIKU ZIJAZO.
WAONE WANAOKUFANYIA UONEVU KUWA NI WAOGA NA WADHAIFU KWA HIYO WANAKUTUMIA WEWE KUJIONESHA NI MASHUJAA KUMBE SIO KWELI.
NA KWA SISI WENGINE
TUNAOSHUHUDIA MATUKIO HAYO,
TUWE TAYARI KUWASAIDIA WALE WANAOONEWA,
ILI NAO WAONE UTAMU WA KUWA KARIBU NA
WATU WENGINE.
0 comments:
Post a Comment