Mwanafunzi ni mtu yeyote
aliye katika mazingira ya
kujifunza kitu fulani
katika maisha,
iwe kazini,
shuleni au hata mtaani.
Lakini tabia za mwanafunzi mmoja zinatofautiana na tabia
za mwengine katika
namna wanavyopokea mafundisho
na kuyafanyia
kazi kwa vitendo.
Kuna sifa ambazo duniani kote
zinatumika kumtambulisha mwanafunzi
bora ni yupi.
Ni kitu kizuri ikiwa kila mtu
ambaye yupo katika
mazingira ya kujifunza akafahamu
sifa za mtu anayejifunza
ni zipi.
Uwe popote pale katika
mazingira ya dunia hii bado
kuna kitu cha
wewe kujifunza.
Jinsi utakavyokielewa na kukitumia
itatokana na wewe mwenyewe
utakavyoweka mawazo na
akili yako mahali hapo.
Sifa za mwanafunzi bora ni kama zifuatazo:
1.TABIA YA KUJIFUNZA VIPYA
Haina shaka yoyote kuwa
mwanafunzi bora ana tabia
ya kuwa tayari kujifunza
kitu kipya hata kama
hakijamvutia kwa mara ya kwanza.
2.UWEZO WA KUTENDA
Mwanafunzi bora ni yule mwenye
uwezo wa kuchukua
alichojifunza na kukiweka
katika matendo katika
hali ya ubunifu wake.
3.MTAZAMO CHANYA
Mwanafunzi bora ni yule mwenye
mtazamo chanya juu ya
mambo anayojifunza,
na ambaye anajijengea uwezo
mkubwa wa kutafsiri na
kuhoji mafundisho katika
namna ya kutaka
kuelewa zaidi.
4.NIDHAMU BINAFSI
Mwenye uwezo wa kutawala muda wake,
anakuwa na sifa ya
kuwasilisha kazi kwa
wakati uliopangwa.
5.KUTAKA KUELEWA
Mwanafunzi mzuri ni yule
anayejifunza na
kuelewa na
si kukariri maandishi na
maelezo tu.
Vitu gani ufanye ili uwe mwanafunzi bora:
1.TAFUTA VICHOCHEO
Ili uwe mwanafunzi mzuri
ni lazima utafute kitu
cha kukuchochea.
Na hii itakuja kichwani
mwako ikiwa utakuwa unajiuliza swali la
"ili iweje?"
Kama unasoma kwa bidii halafu
hujui unataka upate nini
baada ya hapo,
utakuwa unajiweka katika
wakati mgumu.
Na utakuwa katika mazingira
ya popote utakapoangukia
kwako ni sawa tu.
2.WEKA MKAZO
Kuweka mkazo kwenye kujifunza
kunatokana na shauku unayoweka
katika
katika
maisha yako.
Ukiweka mkazo katika
kile unachojifunza utakuwa
unajitengezea
mazingira ya
kutaka kujua zaidi.
3.TABIA
Moja kati ya vitu vitakavyoamua kesho
uwe wapi ni tabia
yako unayofanya leo.
Heshimu wakubwa,
na usiwe unanyanyasa wanafunzi au
watu wengine wa karibu.
Ukiwa na tabia ya kutowatendea wengine
vile ambavyo wewe
hupendi kutendewa utafanya mazingira yako ya kujifunza kuwa bora.
Kuwa msaada kwa wenzako pale wanapokwama kwani hilo ndilo
watakalo likumbuka kwako,
usifanye ili usifiwe
ila fanya ukijua unalomtenda
leo mwenzako na wewe utakuja
kutendewa hivyo hivyo.
KILA MMOJA WETU ANA NAFASI YA KUWA MWANAFUNZI BORA KATIKA YALE ANAYOJIFUNZA.
KINACHOTAKIWA NI UJUE TU UNATAKIWA UFANYE NINI NA KWA WAKATI GANI.
2 comments:
ahsante kwa makala nzuri
Asante sana mwandixhi
Post a Comment