Kila mwaka maelfu ya wanafunzi wanahitimu masomo yao ya elimu ya 
juu na kuingia katika mchakato wa kutafuta ajira.
Idadi ya wanafunzi wanaomaliza,
 ukiilinganisha nafasi za ajira huwa haviendani kabisa na 
unaweza ukajiuliza;
 je, ni wangapi watafanikiwa kuajiriwa?

Jibu,
 ni yule wa kwanza kuitafuta fursa,
 ndio atakaye kuwa 
wa kwanza kuajiriwa.

Kipindi hicho ndio vita ya kutafuta kazi inakuwa kali,
 baina ya wahitimu hawa.
Ushindani unakuwa mkubwa,
 kiasi kwamba kwa kila kazi moja inayotangazwa kuna waombaji zaidi ya mia wanaigombania.

wengine wakiwa na sifa,
 na kuna wengine ambao wamekosa sifa za kupata hiyo kazi,
 lakini wote wanakuwa na nafasi sawa.
Kujua tu,
 wapi kuna nafasi za kazi ni juhudi binafsi ya mhitimu 
mwenyewe kufanya mbinu zake.

Hebu leo tuangalie mbinu ambazo unaweza kuzitumia ili kupata ajira kwa haraka:

1.TENGENEZA MTANDAO NA WAHITIMU WENZAKO

Kubali usikubali,
 kati ya wahitimu wenzako wengine wanawahi sana kupata kazi.
Hawa ndio mara nyingi wanaitwa walio kwenye mfumo(System),
 na wengi wetu tunaonaga wanapendelewa
kwa kuwa wanajuana 
na watu katika soko.
Mtu kama huyu mng'ang'anie usimuache,
kwani wao mara nyingi wanauwezo wa kufahamu kwa haraka mahali ambapo wafanyakazi 
wapya wanahitajika.
Wao  ndio watakuwa wakwanza kukujulisha kama kuna sehemu kuna 
nafasi za kazi zimetangazwa.

2.SOMA MATANGAZO MBALIMBALI YA KAZI

Ukiwa unajizoesha kusoma matangazo
 mbali mbali ya nafasi za kazi utaweza kujua sifa gani 
hasa zinahitajika.
Ukiweza kufanya hili maana yake hautakurupuka kuandika wasifu wako,
 na kutuma haraka haraka kwa kuwa tu umeliona tangazo.
Ukiwa makini kuandaa wasifu,
 ambao muajiri ndio ameuhitaji utaongeza nafasi yako ya kuitwa katika usaili na kupata kazi kwa haraka.
Hapa kwetu njia kubwa inayotumika ni magazeti, 
ukienda sehemu kama maktaba ya taifa utakutana na magazeti hadi ya miaka mitano nyuma,
 hebu fuatilia sifa za waajiliwa zinazohitajika zinavyobadilika mwaka hadi mwaka ili ujiandae.

3.SOMA SANA TAARIFA YA KAMPUNI ULIZOOMBA KAZI WAKATI UNASUBIRI USAILI

Wakati unasubiri,
 kama utaitwa katika usaili au la,
 usikae vijiweni kupiga stori tu,
kila siku
 fuatilia taarifa za kampuni uliyoomba kazi hata kama ni kumi fuatilia zote kwani hujui ipi itakayoanza kukuita.

4.JIANDAE NA VIKWAZO VYAKO

Yawezekana kabisa,
 ukawa umetuma maombi yako ambayo yamepishana kidogo sana na hitaji la muajiri lakini yanaendana kimtindo,
jiandae na utetezi wa kutosha kuhusiana na ulichotuma,
 na waeleze uwiano uko wapi.
Sio kusema tu kuwa unaweza kazi waonyeshe unajua ulichofanya.

5.KUWA TAYARI KUJITOLEA

Wakati unasubiria kupata kazi ya kudumu usijilemaze,
 kukaa bila kitu cha kufanya mitaani.
Nenda katika kampuni ndogo,
 ambazo zinashughulika 
na kazi uliyosomea na jitolee 
kufanya kazi bure bila malipo.
 Hii itakupa uzoefu na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuajiliwa 
hata hapo hapo.

6.HUDHURIA MAONYESHO YA MAKAMPUNI

Katika nchi yoyote,
 makampuni mengi huwa yana utaratibu wa kufanya maonyesho 
wa shughuli zao.
Ukiwa na utaratibu wa kuhudhuria matukio kama haya,
yatakufanya utambue sifa gani huna kwa ajili ya hitaji la soko la ajira,
 na ufanye nini kuongeza ujuzi wako kabla haujaingia katika 
ushindani wa ajira.
Jitahidi siku hiyo uchukue mawasiliano yao.

7.JITENGENEZEE KADI ZA MAWASILIANO(BUSINESS CARDS)

Utaratibu wa kubadilishana mawasiliano,
 baina ya mtu na mtu ni mzuri pale unapotumiwa vizuri.
Utaratibu huu utamfanya uliyekutana naye akuone jinsi gani uko makini,
sio mpaka uwe na biashara au kampuni ndio utengeneze kadi ya
 mawasialiano yako.

8.NENDA MWENYEWE SEHEMU HUSIKA

Ukitegemea sana watu wengine ndio wakutafutie kazi wewe,
 utakuwa unapoteza bahati yako ya kuajiriwa mapema.
Yawezekana kabisa,
 kampuni inajiandaa kutoa tangazo la kazi kesho wewe umeibuka leo,
na una vigezo kwanini wasikuchukue kuliko kuandaa gharama za matangazo.
Si utakuwa umeula hapo!

9.ENDELEZA UNADHIFU

Najua wanafunzi wengi tunanawiri 
na kupendeza pale tunapokuwa mazingira ya masomo,
lakini tunapoingia mtaani tunajiacha hovyo.
Na jua wazi muonekano wako una alama zake 
kwa muajiri,
kama uko hovyo hovyo hata yeye kukuajiri atajiuliza mara mbili mbili.
Utaonekana mwizi tu.

10.JENGA MAWASILIANO NA KAMPUNI

Usikate, 
mawasiliano na kampuni uliyowahi kuomba kazi,
hata kama uliitwa katika usaili ila hukubahatika kupewa ajira,
watumie ujumbe wa 
barua pepe kuwa wasisite 
kukuita ikiwa itatokea nafasi.
Usijitie kisirani 
kuwanunia, utajuta wewe.

KILA MMOJA WETU ANAJUA JINSI GANI AJIRA NI NGUMU KUPATA KWA HARAKA.
LAKINI
TAARIFA ZA UONGO KUHUSU SOKO LA AJIRA ZIMEJAA NYINGI MITAANI.

USIMSIKILIZE MTU MWENGINE,
 KUWA AJIRA HAKUNA.

 TUMIA NJIA HIZO HAPO UONE WEWE MWENYEWE KULIKO KUKATISHWA TAMAA NA MTU MWENGINE.


Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz