Tangu demokrasia
imeingia bara la Africa,
wanasiasa wengi wenye kariba mbali mbali wamekuja na kuondoka.
Kuna wengine
wanafahamika sana na wengine hawajawahi kufahamika kabisa.
Wasomi wa kufanya maamuzi
ya nchi kwa teknolojia,
wamekuwa wengi kiasi kwamba
inasemekana ukirusha jiwe nchini
Nigeria uwezekano wa kumpiga msomi
wa chuo ni asilimia 99.
Pamoja na mahesabu yote
magumu ambayo tumekuwa tunatumia
kufanya maamuzi,
mimi nadhani tunachohitaji katika dunia ya sasa ni hesabu rahisi za
MAGAZIJUTO
(Mabano Gawanya Zidisha Jumlisha Toa)
juu ya hapo huitaji kitu kingine zaidi ya utashi na maono.
Kwa upande mwingine wakoloni
walikuja Afrika
na wakaingiwa na tamaa ya maliasili
ambazo Afrika inazo.
Wakafanya nini?
Katika ardhi yenye maliasili
za thamani
ni lazima walishawishika
kuitamani sana.
Na walianza kuwa na maono na maliasili zetu huku sisi hatujui kinachoendelea.
Lakini ngoja niseme ,
Afrika inahitaji kusonga kwa kasi ya
ajabu,
ila tu
kwa kukipata kiunganishi sahihi kilichokosekana.
Je, hicho kilichokosekana ni kipi?
Kitu tulichokosa mpaka sasa
Afrika ni
watu wenye maono.
Nchi nyingi zilizoendelea
zilifanikiwa kwa kuwa walikuwa na
watu wenye maono na
sio watu wataalamu na wasomi tu.
Na hii inatokana na kuwa maono huwa yana mantiki ndani yake na pia hudumu muda mrefu.
Mwaka 1901,
ulifanyika mkutano wa wasomi na wataalamu katika jiji la London.
Na walikuja na maadhimio yafuatayo:
1.Haiwezekani kitu kilichotengenezwa kwa chuma kuruka angani;
2.Haiwezekani kwa gari kutembea maili 36 kwa saa bila kumletea madhara mtu aliye kwenye hilo gari.
Na huu ndio ufahamu waliokuwa nao kipindi hicho.
Mwaka 1904,
ndugu wa familia ya Wright walikuwa na ujauzito wa maono ndani yao,
na wakafanikiwa kurusha ndege ya
kwanza angani.
Hakuna kingine,
unaweza ukasema kilichangia
ndugu hawa kung'ang'ania majaribio mengi
mpaka kufanikiwa
kuirusha ndege
zaidi ya kuyaamini maono na kujiamini.
Yawezekana,
ndugu hawa walijiambia
kuwa katika dunia hii
hakuna mwenye hakimiliki ya hekima ya kuamua kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.
Kuna maono ya aina mbili,
ya kwanza ni maono kutoka kwa Mungu na
ya pili ni maono ya kisomi.
Maono ya Mungu
humjia mtu pale anapokuwa amelala na
ni ya kiroho zaidi
lakini maono ya kisomi huwa yanatolewa
na akili ya mtu.
Maono ya Mungu,
mara nyingi huwa ni makubwa
na yanamfanya anayeonyeshwa
ashindwe kuyaelewa sawa sawa,
ukubwa wake ndio
unachangia mara nyingi yasitekelezwe na aliyeonyeshwa.
Hii inatokana na aliyeonyeshwa kushindwa kuyaamini maono hayo,
kwa kuwa kiwango cha akili
kinakuwa kimeishia hapo na kinaendelea kumwambia haiwezekani.
Kuna vitu vingi Afrika
tunaona haviwezekani
lakini
wakiwepo watu wa maono
vyote vitawezekana,
na si tu kuwezekana bali tutaviona kuwa rahisi.
Kwasababu tunaendelea kutumia
kiwango cha akili ile ile ya kibinadamu
maono mengi tunayaacha yakipita tu bila kufanyiwa kazi,
ambapo yangeweza kuibadilisha sura ya
Afrika kwa ujumla.
Tunapoendelea
kutumia maono ya kisomi,
mara nyingi huwa ni ya vitabuni na
ambayo yana uwezo sana wa kumbadilisha mtu mmoja na si dunia uliyopo.
Siri moja iliyojificha
ambayo wengi tunashindwa kuigundua,
ni kuwa
vitu vya kiroho ndio halisi na vile vya kimwili vimetokana na matokeo
ya vitu vya kiroho.
Kwa mfano,
mtu anapokufa kitu tunachoendelea kukiona mpaka muda wa kuzika
ni maiti ambayo haina roho,
kwahiyo kukosekana kwa roho ni kukosekana
kwa maisha.
Kwa hiyo maono ya kiroho ndio yenye
uwezo wa kuibadilisha dunia.
Kuna sababu nyingi,
sana zinazofanya maono mengi
yasifanyiwe kazi.
Lakini
mimi nitazungumzia sababu moja
ambayo ndio hutoa
kiashiria cha ukubwa wa maono yako
na si kingine ni 'upinzani'.
Mtu mwenye maono makubwa,
ndiye mwenye upinzani
mkubwa sana.
Unapokuwa na maono usikae nayo kimya,
bali yaweke wazi
kwa watu wengine.
Wengi wetu tunataka tunapoeleza maono
kwa watu wengi tusifiwe tu,
nakuambia ukweli
kama maono utakayotoa
hayapati upinzani jua kabisa hayo
sio maono bali ni hadithi
tu ya kuvutia.
Unapokutana na upinzani mkubwa,
ndio hukupa picha kuwa ulichobeba
sio kitu cha kawaida.
Ikitokea msimu wa kiangazi mvua kubwa ikanyesha kwa mtu mwema,
watu wabaya watazungumzia
sana ukubwa wa hiyo mvua/au
muda uliyotumia kunyesha.
Lakini kuna mvua ambayo,
wewe peke yako ndio unaijua ukubwa wake,
na unapaswa uwe ndio mwenye
maelezo yake.
Kwa wafanyabiashara
wenzangu jambo hili la maono yawezekana liko mbali na upeo wetu wa kufikiri.
Kwani dhumuni kuu la biashara ni kutengeneza faida ambayo huwa na mwisho wake.
lakini,
unapokuwa na maono na kuyafanyia kazi utaingiza faida isiyokwisha kwasababu utakachoacha ni urithi kwa vizazi vilivyopo
na vijavyo.
Urithi huishi milele.
Kwahiyo,
jinsi unavyoyaamini maono yako ndio itakayoamua
yatakavyofanikiwa.
Kujiamini ndio kutafanya maono
yaweze kutelezeka na
kuwa vitu halisi.
Nina maono yangu yanaitwa 'Maono ya Afrika',
hakuna kitakachonizuia
kuyafanikisha.
Maono yako hayawezi kufanana na ya mtu mwingine yeyote
ni wewe peke yako mwenye uwezo
wa kuwa nayo.
Bwana Alexander Bell alifanikiwa
kutimiza maono yake ya kutengeneza simu ya kwanza,
zaidi ya hapo wanaofuatia wanabaki kuiboresha tu aliyoianzisha yeye.
Huu ndio tunaita urithi wa milele.
YAWEZEKANA KABISA TUKAWA BADO TUNAKOSA KUJIAMINI KATIKA KUYAFANYA MAONO TULIYONAYO YAWE KWELI.
HATA KAMA UNAYAONA NI MAKUBWA SANA KWAKO NA UNAONA ITAKUCHUKUA MUDA MREFU KUYATIMIZA USIACHE.
TEMBO ANABEBA MIMBA KWA MUDA WA MIEZI 24 NA KIUMBE ANACHOKUJA KUKITOA HUWA NI KIKUBWA.
NIMETUMIWA MAKALA HII NA:
Patrick Marimo
Motivational Speaker & Dreamer of The
African Dream
pmarimo@gmail.com +255 785159444
1 comments:
Speak of which, that is the wise we are missing now_days in our Africa. Binafsi nmejifunza kitu cha muhimu kupitia article hii. Nikushauri uzi_post kwenye mitandao mikubwa ya kijamii like facebook.
Sisi vijana wa sikuhizi tumekosa elimu ya kujitambua na hekima kwahiyo tunahitaji sana maarifa kama haya. Elimu ya darasani haitutoshi kabisa pamoja na wazazi kutukaririsha kuwa elimu hiyo pekee ndo ufunguo wa maisha. Tukijitambua na kutambua majukumu yetu na kuacha uvivu basi bila_shaka tutaibadili AFRICA YETU.
Jina langu ni Shalom Mgalawe, asante.
Post a Comment