"Kuvaa na kupendeza, ni kipaji jamani!!"
Linapokuja,
suala la uvae nini ili upendeze
mara nyingi
linaumiza kichwa.
Na unapoangalia uvaaji wa kila mtu na anaonekanaje,
ndio unagundua kuvaa ni kipaji.
Kuna watu wao kila nguo wanayonunua inawapendeza.
Kwa wengine wakina sisi inakuwa ni kitendawili,
cha tuvae nini ili tupendeze.
Na kuna makosa makubwa ambayo tunayafanya wakati tunapoenda kuchagua nguo za kuvaa ni haya hapa:
1.KUNUNUA NGUO ISIYOTOSHA
Hapa unakuta unanunua nguo kubwa
au ndogo sana
kuliko mwili wako.
Nguo inapokuwa kubwa inakufanya uonekane imekuvaa,
na
inapokuwa ndogo sana
itaonekana imekuchora mwili wako na
kupendeza katika hali hiyo ni
nadra sana.
Ukiona unashindwa kabisa katika kuchagua, jenga urafiki na
fundi nguo tu.
2.KUVAA SHATI MIKONO MIFUPI NA TAI
Labda,
kama uwe unafanya kazi mgahawani,
kwahiyo
unaogopa mikono ya shati kuchafuka na vyakula vinavyomwagika mezani,
ndio uvae hivyo.
Ukiwa umevaa hivi katika mazingira mengine,
hakuna
atakayekuona umependeza.
3.KUVAA VIATU VICHAFU
Inawezekana kabisa,
ukavaa nguo zikakupendeza sana,
lakini
ukiharibu katika viatu utaonekana haujapendeza kabisa.
4.KUVAA MKANDA WA RANGI TOFAUTI
Ukikosea kuvaa mkanda,
ambao rangi yake haiendani na rangi ya nguo au viatu ulivyovaa
utachosha machoni pa watu.
5.KUFUNGA TAI NDEFU AU FUPI SANA
Ikiwa utavaa tai ambayo ni ndefu sana,
au fupi sana
utaharibu ladha ya muonekano wako.
We utakuta mtu amevaa tai kubwa
inapita hadi mkanda wa suruali au fupi sana inaishia kifuani tu,
kupendeza utaota milele.
6.KUVAA SOKSI NA VIATU VYA WAZI
Hapa bwana,
hata kama umevaa vipi huko juu
lakini
utaonekana kituko tu
katika hili.
7.KUVAA NGUO ZA RANGI ZINAZOPINGANA
Ni vizuri,
ukawa makini wakati wa
kuchagua nguo ya rangi gani
inaendana na rangi gani
sio ilimradi umevaa tu.
Na kuna muda mwengine hata ujaribu kujua rangi yako ya mwili pia
kama inaendana na rangi ya
nguo utakayovaa.
8.KUVAA NGUO ZILIZOJIKUNJA
Ni vyema,
ukazinyoosha nguo zako
kuliko
kuzivaa bila kuzinyoosha ni kujishusha muonekano wako.
Ni heri kama unajua hupendi kunyoosha basi usizitupe nguo hovyo,
tafuta kitu cha kutundikia ili isijikunje kama unajua utairudia.
9.KUVAA NGUO ZENYE RANGI NYINGI NYINGI
Wewe utakuta mtu unavaa nguo ina rangi nane tofauti tofauti
halafu eti unategemea kupendeza.
Lazima ujaribu
kuchagua nguo zenye
mchanganyiko mdogo wa rangi na
sio rangi nyingi nyingi.
10.KUVAA WIGI LA RANGI AU MTINDO USIOENDANA NA WEWE
Si kila wigi la nywele linafaa kuvaliwa na kila mtu,
kuna mawigi mengine rangi yake haiendani na wewe.
Hata kama ndio liko katika fasheni lakini usiharibu muonekano wako
kwa kuingia kichwa kichwa matika mtindo
usiokupendeza.
KILA MMOJA WETU ANAPENDA AONEKANE AMEPENDEZA,
HILO HALIPINGIKI.
NA INAWEZEKANA KABISA MAKOSA HAYA YA UVAAJI TUNAYAFANYA.
BASI TUJARIBU KUWA MAKINI TUNAPOCHAGUA NGUO ZA KUVAA.
ITAENDELEA....
0 comments:
Post a Comment