Si kila
anayefanya shughuli fulani
huwa na
utaalamu nayo,
wengine wanaifanya kwa kuwa tu nafasi ilitokea ya kuifanya.
Na hautachukua muda
kumgundua mtu anayefanya kazi zake kwa utaalamu,
na yule anayebangaiza njaa tu,
kwa jinsi wanavyoenenda na tabia zao.
Mara nyingi
waajiri na wateja
hulalamika kuwa anayewafanyia kazi
hana utaalamu.
Yawezekana humalizi kazi vizuri, umemcheleweshea au hata kumzungusha kwa muda mrefu bila taarifa sahihi.
Si mara moja tunasikia
ni jinsi gani tunatakiwa kuwa wataalamu katika
shughuli tunazofanya.
Kama unataka kupata mafanikio,
kuchukuliwa kama mtu makini,
kuonekana una mchango kwa unaofanya nao shuguli zako,
kuzifanya kitaalamu ndio njia pekee ya kukufikisha huko.
Lakini tujiulize waajiri/wateja wanatafsiri gani juu ya utaalamu?
Wengi wao watakuona mtaalamu ikiwa wewe:
*Unafika eneo la kazi katika muda unaotakiwa;
*Unaifanya kazi uliyopewa vizuri;
*Unamaliza kazi kwa wakati.
Unadhani kuna matukio mengine ambayo unahisi ukiyafanya yatakuonyesha wewe si mtaalamu?
Kuna matukio ukiwa unayafanya yanakutafsiri moja kwa moja kuwa wewe si mtaalamu wa shaghuli unayofanya.
kwa mfano ukiwa:
*Unachelewesha kazi za watu;
*Unahudhuria vikao ukiwa haujajiandaa;
*Unatumia muda mwingi kuongea umbea muda wa kazi;
*Wavunjia heshima wenzako;
*Wasubirisha wateja muda mrefu bila sababu za msingi;
*Unaiba mawazo ya watu wengine kufanyia shughuli zako bila kuwahusisha;
*Vunja ahadi zako mara kwa mara.
Hebu leo tuangalie njia kumi utakazoweza kutumia kuwa mtaalamu katika shughuli yoyote unayofanya:
Jitahidi kufanya shughuli zako kitaalamu na watu waweze kukuamini,
kukuheshimu,
na kukuona una uwezo wa kipekee.
Japo
mazingira ya kila kazi
yanatofautiana lakini
linapokuja suala la utaalamu huwa
na tafsiri moja dunia nzima.
Hebu tuangalie sifa za kuwa mtaalamu ni zipi:
1.UMAHIRI:
Lazima
uwe mahiri katika kile unachofanya,
ukitumia ujuzi na maarifa
ya kutosha katika kazi yako
lazima utaonekana mtaalamu na watu.
2.ZINGATIA MUDA:
Watu watakuwa wanakutegemea wewe
ufike katika muda unaotakiwa
ili shughuli ziende na
umalize kwa wakati.
Sio kuendelea kufanya shughuli zako kwa mazoea tu bila kujali muda,
kwani hakuna anayependa kumuamini na kumpa kazi mtu asiyemaliza kwa wakati.
3.UAMINIFU:
Unatakiwa kuwa
muwazi wa shughuli zako,
na wale unaofanya/unaowafanyia kazi nao wajue nini kinachoendelea.
Ukianza kujifanya mjanja mjanja,
katika shughuli unayofanya
huku
huwaweki wazi watu wengine
hakuna atakayekuona mtaalamu hata kidogo.
4.UADILIFU:
Utaonekana mtaalamu
ikiwa utakuwa unasimamia kanuni za
shughuli yako.
Hakuna anayependa kumpa kazi mtu asiyejua kufuata kanuni za kazi yake.
5.HESHIMA:
Kama huna heshima kwa watu wengine
unaofanya nao
au unaowafanyia shughuli
basi hautaonekana
mtaalamu hata kidogo.
6.ONGEZA UJUZI:
Tafuta ujuzi wa ziada,
usiendelee kung'ang'ania ujuzi ule ule
kila siku.
Toka nje ya yale unayoyafahamu
ili kupata mengine mapya
kuongezea katika yale unayayafahamu
ili kuboresha zaidi utendaji.
7.MTAZAMO CHANYA:
Kama wewe
kila siku unaangalia makosa tu bila
kuwa na mtazamo chanya juu ya shughuli unayofanya
kuwa mtaalamu itakuwa ndoto kwako.
8.TOA MSAADA:
Wasaidie wenzako unaofanya nao shughuli
sio kwa kuwa wewe unafahamu kitu
fulani basi hutaki
wenzako wafahamu.
Waonyeshe jinsi ya kufanya kazi vizuri pale unapoweza
na wasikilize pale wanapokuuliza
maswali.
9.TENGANISHA MATUKIO:
Usihusishe matukio ya nyumbani au
mtaani na kazi,
ukiwa katika shughuli zako weka mawazo
yako yote hapo.
Utakuwa mtu wa ajabu
kufika eneo la kazi na kuanza kushughulikia masuala ya nyumbani
huku ukiacha kazi haziendi.
10.KUWA MSIKIVU:
Kila mtu
ana hitaji la kusikilizwa pale
anapokuwa na
jambo la kusema,
Kwa hiyo wape watu nafasi ya kukuelezea
yale wanayodhani yatasaidia
katika utendaji wa kazi.
KILA MMOJA WETU ANAPENDA KUPATA MAFANIKIO KATIKA SHUGUHULI ILE ANAYOFANYA,
BASI TUANZE SASA
KUFANYA KAZI KITAALAMU ILI TUWEZE KUFIKIA YALE TUNAYOYATAKA.
0 comments:
Post a Comment