Katika maisha kuna mambo mengi sana ambayo unayatamani,
na kila siku unaomba
yawe mikononi mwako.
Tangu ulipoanza kuyatamani ulikuwa na mipango,
mawazo na mikakati mingi
sana kichwani,
lakini mpaka leo haujafanikiwa
kuwa nacho.
Na yawezekana unajiuliza kila siku na jibu mpaka leo haujapata.
Sasa hebu leo chukua hizi hatua nane halafu anza kuzifanyia kazi:
1.ANZA KUKAA NA WATU SAHIHI
Hawa ni watu ambao wewe unapokuwa nao unafurahia,
wanaokupenda, kukuthamini, na
wanaokutia moyo wa kutokata tamaa katika mambo yako.
Hawa ni wale watu ambao ukikaa nao wanakufanya ujihisi uko hai,
ambao wanaokukumbatia wewe wa sasa hivi na wanaotamani kumkumbatia yule unayetamani kuwa,
bila masharti yoyote.
2.ANZA KUWA MUAMINIFU KWA NAFSI YAKO
Kuwa muaminifu kwa jambo lipi ni sahihi kwako,
na lipi linahitaji
kubadilishwa.
Kuwa muaminifu kwa lipi unataka
kufanikisha na nani
unataka kuwa.
Ukianza kujidanganya nafsi yako mwenyewe utakuwa unakosa fursa
za kujitambua
kama unachotamani ni sahihi kwako.
3.ANZA KUTENGENEZA VIPAUMBELE VYA FURAHA YAKO
Mahitaji yako yana umuhimu sana.
Kama usipoanza kuweka vipaumbele vya vitu gani hasa vinakupa furaha,
hautaweza kujitambua
wewe ni nani.
Kama utaweza kutambua wewe
unafurahia nini itakuwa
rahisi kuwafurahisha na watu
wako wa karibu.
4.ANZA KUWEKA WAZI WAZO NA NDOTO ZAKO
Katika maisha,
kama unasubiri fursa zikufuate utangoja milele,
lakini kama ukiziuata fursa huko ziliko zitakupokea kwa
mikono miwili.
Haina maana kukaa chini na kujisifu kuwa una mawazo na ndoto nzuri,
kama haujaanza kuzitoa zionekane.
5.ANZA KUJIVUNIA ULIVYO
Kama haujaanza kujivunia vile ulivyo leo, itakuwa
ngumu kupiga hatua zako mwenyewe kuelekea mafanikio.
Ukianza kujivunia vile ulivyo
utafanya uyaone mawazo yako yana thamani, nguvu na uzuri ambao hakuna
mwengine yeyote anao.
6.ANZA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA
Kama uliwahi kukosea na ukapata funzo fulani anza kulithamini hilo funzo
kwa kuchukua mafundisho yake na
kuyafanyia kazi.
Na ukiweza kufanya hilo,
utaona kumbe kukosea ni hatua moja wapo katika kupata mafanikio.
Kwani kuna uwezekano mkubwa kabisa kama usipotaka kujifunza
kutokana na hilo basi
utakuwa unalikwepa daraja ambalo lingekuunganisha na mafanikio.
7.ANZA KUWA MKARIMU KWA NAFSI YAKO
Kama utaendelea kutumia muda mrefu katika kuilaumu nafsi yako,
na kutaka kujiadhibu utakuwa unaendelea kujirudisha nyuma.
Ukiwa mkarimu kwa nafsi yako utaona nafasi ya wewe kunyanyuka kila
unapokuwa umedondoka
bila kujikatisha tamaa.
8.ANZA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAKO
Matatizo yanayokukabili hayatoi tafsiri
ya wewe ni nani,
bali jinsi unavyoyakabili
na kuyamaliza ndiyo
tafsiri yako ilipo.
Matatizo hayawezi kuondoka mpaka wewe mwenyewe uyakabili.
Fanya jitihada zako zote pale unapoweza halafu jipongeze kwa
hatua uliyopiga.
TUANZE LEO KUCHUKUA HATUA HIZI NA YALE YOTE TUNAYOOTA YAWE YETU YATAKUWA
KWETU BILA UTATA.
0 comments:
Post a Comment