Ukiwa mzazi, au mlezi
lazima
kuna kipindi unapata hofu
na mtoto wako.
Ambaye unaona anaelekea katika rika la
ujana na kepuvuka.
Unafikiria mambo mengi ambayo wewe unayafahamu kama changamoto katika maisha ya ujana ambayo uliyapitia,
na unaona kabisa na yeye sasa anaenda kukumbana nayo.
Hofu yako kubwa ni,
hujui atatumia njia gani kukwepa mitego ya jamii
na kama ataingia kwenye mtego na
kunaswa atatokaje?
Kwani kiuhalisia kijana wako,
anapoanza kuchangamana na vijana wengine wenye historia
mbali mbali huwa katika uwezekano
wa kuchota tabia zao
kwa kuwa anatumia muda mwingi
kuwa nao kuliko wewe.
Ushahidi unaonyesha
kuwa vijana wengi ambao walikuwa wanapewa usia wa mambo ya maisha
na wazazi wao,
walifanikiwa kukwepa mitego hiyo kwa kukumbuka maneno ya mzazi, na
hofu kutotaka kwenda kinyume
na maelekezo yao.
Kuna kipindi,
wewe mzazi, mlezi,
Kaka au dada unaona
kabisa kijana wako anaonyesha mabadiliko
ya tabia,
lakini unajisikia aibu kukaa naye chini na kumpa ukweli wa mambo ulivyo.
Kwani waswahili wanasema;
"Samaki mkunje angali mbichi"
Ukishamkosea katika rika hili,
basi uombe,
awe na uzoefu binafsi wa kutambua vita iliyo mbele yake ni ya namna gani na vipi ataishinda.
Hapa tuangalie mambo 7 ambayo mzazi unapaswa uanze kuzungumza na kijana wako:
1.NGONO NA JINSIA
Kijana wako,
ambaye anakua atakutana
na taarifa nyingi sana
kuhusu ngono na jinsia.
Ambazo nyingi sana huko mtaani huwa
si sahihi.
Iwe kupitia vyombo vya habari au uzoefu atakaokutana nao
yeye mwenyewe.
Anza kuzungumza naye kuhusu masuala ya uzazi, mimba za utotoni, na utoaji wa mimba
huku ukijikita katika madhara na namna ya kujikinga navyo.
2.DAWA ZA KULEVYA,NA POMBE
Vijana wanapenda sana kuhudhuria
burudani kipindi
wakiwa mtaani,
shule au hata vyuoni miaka ya mwanzoni.
Huko
wanakuwa katika hatari ya
kutumia vilevi
kwa kuwa wanakutana na vijana wenzao wenye historia tofauti tofauti.
Kama usipomnyoosha mapema wewe mwenyewe vijana wenzake
watamnyoosha katika njia zao.
Kwani wengi wao
wanaingia katika mkumbo kwa kuwa,
hawakupata taarifa sahihi kutoka kwa wenzao juu ya madhara ya tabia hizo,
na pia kukwepa kuonekana mshamba.
3.MATUMIZI YA PESA
Kipindi cha ukuaji mahitaji na
matumizi ya kijana yanaongezeka kwa
kasi kubwa sana,
hata kutunza kidogo anachopata kwake
huwa ni tatizo.
Kaa na kijana wako umuonyeshe namna ya kutunza kidogo anachopata.
Mueleze faida za kutunza pesa zilivyo na zitamsaidiaje katika maisha yake ya kujitegemea.
4.UMUHIMU WA FAMILIA
Mara nyingi,
vijana wanapopata nafasi ya kufanya
shughuli zao wenyewe,
kukaa karibu na familia huwa ni
kitu kigumu.
Hata muda anaotumia kukaa na wanafamilia wenzake huwa ni mdogo kuliko anaotumia kukaa na marafiki.
Tumia busara zako kumuungabnisha na wanafamilia wengine ili washirikiane kwa pamoja.
5.MAHUSIANO NA MITOKO
Vijana hawaoni tabu
kubadilisha marafiki hata kwa mwezi mara nne na bado akajiona yuko juu kwa
kuwa anawabadilisha anavyotaka.
Usiruhusu kijana wako akue na misingi isiyostahili,
kwani itakuja kumuumiza siku zijazo.
Nawe hautajivunia utakayokuwa unayasikia na kuona kumhusu yeye.
Kaa naye kabla hajaingia huko,
na ujaribu kumuongoza
njia sahihi.
6.MATUMIZI YA MITANDAO
Katika zama hizi ambazo teknolojia ya mtandao wa intaneti imeenea kila mahali.
Vijana siku hizi
kama wamewekewa gundi hapo,
kinachopaswa ni wewe mzazi kumfundisha
mambo yapi yana umuhimu na yapi hayana umuhimu kwake katika
mtandao wa intaneti mapema sio mpaka ulimwengu wa nje uje umfundishe akiwa ameshaumia.
7.TAFSIRI YA KUFANIKIWA
Vijana wengi,
tuna tafsiri tofauti tofauti
juu ya maana halisi ya kufanikiwa
katika maisha.
Hapa ndipo tunapoanzia kupoteza dira kwasababu
tunayoyahangaikia kwa kudhani
ndio yatakuwa mafanikio
yanakuja kuwa sio.
Iwe katika michezo, elimu, au jambo lolote ambalo litakuwa
linahusisha nguvu na akili zake lazima umpe tafsiri sahihi ya kufanikiwa
ni kuwa na nini.
Yafuatayo unaweza ukaanza kuyafanya leo:
*Mpe usalama;
*Muonyesha upendo na kumjali;
*Weka misingi yako ambayo yeye ataifuata kipindi yupo chini yako;
*Muadhibu pale inapobidi;
*Kuwa na muda wa kutosha kukaa naye na kuzungumza naye;
*Fuatilia uhusiano wake na wengine;
*Muonyeshe mfano.
KILA MZAZI ANAPENDA KUONA MTOTO WAKE AKIWA ANAJIHUSISHA NA
MAMBO YA MSINGI KATIKA MAISHA YAKE.
UKIANZA KUMTEGENEZEA MAZINGIRA HAYO TANGU MAPEMA UTAWEZA KUJIVUNIA
TABIA YAKE YA KESHO.
ISIJE BAADAYE KIJANA WAKO AKAKULAUMU KWAMBA HUKUMUELEZA NA KWAMBA
UMECHANGIA KUHARIBU
MAISHA YAKE KWA KUKAA KIMYA.
0 comments:
Post a Comment