"Je, niko katika njia sahihi?"
Kama,
 umewahi kujiuliza hili swali,
uko karibu 
kuipata njia yako sahihi.
Wengi,
 tunajihusisha katika shughuli mbali mbali bila kujua 
kama njia tunayoifuata/tuliyochukua
 ni sahihi au 
si sahihi kwetu.

Ulishawahi kuamka usiku mnene,
huku ukijiuliza kama njia uliyaochagua ni sahihi kwako au la?

Wengi tunajiuliza,
kuwa njia sahihi maana yake ni nini?

Kujiuliza swali hili,
 ni hatua kubwa sana 
kupiga katika maisha yako ya 
kutafuta shughuli sahihi ya kufanya.
Fahamu wazi,
 kuwa unaanza kujitambua,
na ni ishara mojawapo ya kujua 
mahitaji gani ni muhimu kwako.

Yawezekana,
ukawa unalipwa vizuri,
una mazingira mazuri ya kazi,
au una 
vifaa vyote vya kufanyia kazi zako.
Linapokuja
 suala la upo sehemu sahihi au 
sio sahihi 
masuala hayo niliyotaja hapo juu
 huwekwa kando.

Ishara za kuangalia kama upo njia sahihi katika shughuli unayofanya:

1.MUDA HAUKUTOSHI

Unapokuwa unafanya hiyo shughuli,
unaona muda kama unapaa.
Kwa kuwa
kwako si kazi tu bali unafurahia 
kila dakika ya 
kitu unachofanya.
Na unapokuwa mbali 
na shughuli yako au 
hata ukiwa umelala unatamani asubuhi ifike ili urudi tena eneo lako la kazi.

2.UNAPOTEZA MUUNGANIKO NA MATUKIO YA NJE YA KAZI

Unapokuwa mzigoni unahisi kama unasafiri dunia ya kipekee,
na unapoteza mawasiliano na dunia inayokuzunguka.
Unaweza  ukawa unaongeleshwa na watu na usiwasikie kabisa,
 kwa kuwa akili yako yote imetekwa 
kwa muda huo na muda mwengine hata kula unasahau.

3.UNA IMANI NAYO MOYONI

Moyoni una imani kuwa
 hii ndiyo kazi uliyoumbwa kuifanya na hakuna 
atakayeweza kukubadilisha mawazo 
na imani yako
 uliyonayo juu ya shughuli hiyo.

4.UNA MAONO NA SHUGHULI HIYO

Una maono ya wazi kabisa ,
ya nini 
unataka kupata baada ya muda fulani, 
na hata kama kuna 
vikwazo vinajitokeza bado 
unanguvu za kutaka kufikia 
lengo lako.

5.HAUKATI TAMAA

Hata kama kuna watu, 
au mazingira 
yanataka kukurudisha nyuma
 bado hutaki kukata tamaa na 
shughuli yako.

6.UNAFURAHIA CHANGAMOTO

Pamoja na changamoto zinazojitokeza
 mara kwa mara 
unafurahia uwepo wake kwani zinakupa 
uzoefu mpya ambao mwanzo
 hukuwa nao.

7.WATU WANAKUUNGA MKONO

Watu kadhaa watachukua muda wao,
 kuwasiliana na wewe 
ili kukupa msaada na muongozo wa 
shughuli yako.
Hata wewe mwenyewe huelewi watu hawa wanakujaje katika maisha yako
 lakini
 wanakuja na msaada mkubwa sana kwako.

8.UNACHOFANYA KINALETA MABADILIKO YA KWELI KATIKA MAISHA YA WENGINE

Wewe unaweza ukaona 
unachofanya ni kitu kidogo lakini kuna 
watu kinawasaidia sana,
na mrejesho wao 
utakupa picha halisi ya jinsi unavyogusa maisha ya watu wengine.

NI VYEMA UKAANZA KUJITAFAKARI SASA,
KAMA NJIA UNAYOTAMANI 
AU ULIYOCHUKUA 
NI SAHIHI AU LA.

 HII ITAKUSAIDIA KUKUEPUSHA NA UPEPO USIO SAHIHI.

NA KUANZIA LEO,
 TAMBUA KUWA NJIA SAHIHI
 NDIO ITAKAYOKUPA MAFANIKIO YA KWELI KATIKA MAISHA YAKO.

Siku hizi,
 suala la mtu kupokwa akaunti yake ya facebook,
 na ikawa inatumiwa 
na mtu mwengine 
ni jambo limekithiri sana.
Anayepoka akaunti na 
kubadilisha alama za siri 
na email yako anakufanya usiweze kuitumia tena akaunti yako.

Na mbaya zaidi
 anaweza kuanza kuitumia kukuharibia 
uhusiano wako 
na watu wengine.
Anaweza akawa
 anaweka lugha za matusi juu ya 
ukurasa au
 hata kuwatukana watu 
unaofahamiana nao.

Watu hawa 
 hutumia njia mbali mbali katika kupata nafasi ya kukupoka
 akaunti yako:
1.Kuzifahamu alama zako za siri;
2.Kuifahamu email yako;
3.Kufahamu majibu ya maswali yako ya siri.

Na unapojaribu kuingia hili ndio unakutana nalo.
Ukishapokwa ukitaka kuingia 
utaambiwa umekosea email
 au alama za siri.

Kama ushapokwa tayari leo nitakuonyesha 
jinsi ya kuirudisha akaunti yako:

Itakuletea ukurasa 
ambao wewe kwa juu kuna nafasi ya wewe kuingiza hitaji lako.
Andika neno: "My Account Compromised"
au "My Account hacked"


2.HATUA YA PILI:
Katika ukurasa ufuatao bonyeza sehemu iliyoandikwa 
"I can't identify my account"


3.HATUA YA TATU:
Jaza majibu katika maswali yaliyoweka katika ukurasa ufuatao.

Jinsi ya kujibu maswali ya hapo juu:

*Ingiza Email address uliyotumia kufungulia akaunti yako sehemu zote mbili.

*Katika kipengele cha tatu
 Kubali kuwa unaifikia hiyo
 email address kwa kuchagua 
"Yes" 
itasaidia facebook wakupe 
nafasi ya kubadilisha alama za
 siri za email yako.

*Ingiza jina lako lote unalotumia 
uliokuwa unatumia katika 
akaunti yako.

*Ingiza tarehe yako ya kuzaliwa, 
njia mbadala ya kuitambulisha 
akaunti yako, 
na namba yako ya simu,
kwa ajili ya sababu za kiusalama.

*Ingia akaunti nyingine halafu 
ingiza jina lako 
la akaunti uliyopokwa halafu 
kopi ile anwani ya pale juu.
Njoo uipesti hapa 'Facebook profile URL'

*Kama uliwahi kuipa jina picha yako iliyo juu andika hilo jina hapo.

*Kipengele hiki cha mwisho elezea jinsi akaunti yako ilivyopokwa,
jitahidi kuorodhesha njia mbali mbali
 ambazo unahisi alaiyekupoka
 alitumia kuingia katika akaunti yako.

*Mwisho 'Submit' na facebook watakutumia meseji katika email yako.

HATUA ITAWAFANYA FACEBOOK WAKURUDISHIE UTAWALA WA AKAUNTI YAKO IKIWA NA KILA KITU ULICHOKUWA NACHO MWANZO.

JITAHIDI MTU MWENGINE ASIJUE TAARIFA ZAKO ZA SIRI KATIKA AKAUNTI YAKO.

 Eid Mubarak!

Ulimwengu jinsi ulivyo,
 hupati picha kama 
binadamu angekuwa mmoja angeishi vipi
 peke yake.
Kwani 
ukiangalia mfumo ulivyo,
 unamfanya na kumtaka 
binadamu awategemee wenzake katika kutimiza mahitaji yake,
 kuanzia kimwili hadi kihisia.
Hali hiyo humfanya kila binadamu awe tegemezi kwa binadamu wengine,
 katika kukamilisha furaha
 yake ya kila siku.

Lakini
 kwa kuwa watu unaokutana nao 
hamfanani tabia kuna kipindi 
lazima
 kutatokea utengano na hao marafiki.
Ama 
uwe wewe umechoka na mwenendo wao au wao wachoke na mwenendo wako.

Lakini 
mpaka utengano kukamilika,
 kuna dalili huwa zinajionyesha mwanzoni ambazo
 ukizisoma utagundua mapema sana kwamba kuna kitu unatakiwa ufanye ama kuuokoa au kuumaliza kabisa na wewe.

Hebu tuangalie dalili 5 unazoweza kuziangalia katuika urafiki wako:

1.MUONEKANO WA USONI

Kama
 wana nyuso za furaha 
wanapokuona,
 hapo jua wanafurahia uwepo wako.
Lakini 
ukiona umetokea tu nyuso 
za watu zimebadilika ujue hizo ni
 dalili za 
kuwa uwepo wako 
hauna umuhimu kwao.

2.MATEMBEZINI

Kama
 wanakuita katika safari zao 
za matembezi 
ya kawaida ujue wanapenda 
uwepo wako lakini kama 
kila siku unashtukia tu wanahadithiana waliyoyafanya jana ambapo wewe hukuwepo hiyo ni dalili mbaya.

3.KUKUPIGIA SIMU AU KUKUTUMIA MESEJI

Kama 
ukiona wewe haupigiwi wala 
kutumiwa meseji 
kama 
kipindi cha nyuma huku wao 
wanawasiliana
ujue dalili sio nzuri.

4.MANENO KUTOKA KWA MARAFIKI ZAO

Hata 
marafiki zako pia 
nao wana marafiki,
 kwahiyo 
endapo hawafurahii uwepo wako
 wao ndio wa kwanza kuwasimulia habari zako wasizozipenda.

5.KUKUPINGA KILA UNACHOONGEA

Yaani
mkiwa mna jadili jambo,
 wao ndio huwa wa kwanza kukucheka unachoongea.
Wanakuonyesha wazi kuwa,
 hawakubaliani na unayoongea hata kama kuna ukweli ndani yake.

KUPOTEZA MARAFIKI KATIKA MAISHA YETU
 SI KITU KIZURI.

USIPOTAFUTA TATIZO LIKO KWAKO 
AU KWAO
 UTAJIKUTA HAUDUMU NA
 MARAFIKI KAMWE. 

KAMA UKIONA URAFIKI HAUNA FAIDA 
UMALIZE 
LAKINI 
UKIONA UNAFAIDA 
PIGANIA KUUDUMISHA KWA 
KUREKEBISHA KASORO ZILIZOPO.

Najua kila mmoja wetu kuna kipindi,
 anapatwa na hasira 
pale ambapo anaona ameendewa 
kinyume na alichotarajia.
Inawezekana 
ni ofisini,
 nyumbani, 
au hata njiani hali hii ikakukuta.

Je, 
kupatwa na hasira ni upungufu wa
 afya ya akili?
Jibu ni hapana,
hasira huwa zipo na zimeumbwa kwa kila binadamu.
Kwahiyo kushikwa na hasira ni jambo la kawaida ila kutenda jambo baya la kumdhuru mtu au mali kutokana na hasira huo ni upungufu.
Kila mmoja wetu,
 anatakiwa awe makini katika kuzitawala hasira zake na aweze kujizuia pale 
anapoona zimezidi.

Hebu tuangalie njia saba zinazoweza kukusaidia kuzitawala hasira zako:

1.ONDOKA ENEO HILO

Kama upo mazingira fulani
 na ukaudhiwa 
na hasira kali ikakushika,
ondoka kwa dakika chache eneo hilo na ukafikirie vizuri.
Ukifanya hivi,
 unasaidia kupunguza uzito wa yaliyokufanya uchukie 
kwani ubongo utapata nafasi ya 
kutafakari upya.

2.ELEZEA HASIRA YAKO UKIWA NA UTULIVU

Unapoelezea,
 hasira yako kwa mtu/watu 
waliokufanya ukasirike unasaidia 
kupunguza uzito wa 
tukio moyoni mwako.
Elezea kwanini
 ulichukia na kwa utulivu kabisa bila kumuumiza mtu mwengine 
kwa maneno yako omba 
lisirudiwe tena.

3.FANYA MAZOEZI

Mazoezi ya viungo 
yanasaidia kupunguza hisia kali 
moyoni mwako pale 
zinapotaka kuripuka.
Kama unaona una hasira nzito, 
nenda eneo la mazoezi 
anza kufanya mazoezi ya kukimbia au 
kama una chumba cha mazoezi 
kwako ingia anza kufanya mazoezi na utaona mabadiliko yake.

4.FIKIRIA KABLA HUJAZUNGUMZA

Ukiwa ushapamba moto wa hasira, 
ni rahisi
 kuzungumza maneno makali ambayo 
yanaweza yakashusha utu wako au wa unayemwambia.
Chukua dakika chache,
 kutafakari
 maneno ya kutumia na uone kama hayatokuharibia au kumuharibia mwengine heshima yake.

5.FIKIRIA SULUHISHO MBADALA

Badala ya kuendelea kutafakari
 kilichokufanya uchukie,
anza kufikiria namna ya kutatua tatizo lililojitokeza 
kati yako na upande wa pili.
Yawezekana mtoto wako anaharibu vitu hovyo,
dereva wako anachelewa 
kukufuata eneo unalomtaarifu,
au mpenzi wako anachelewa kufika eneo la miadi.
Fikiria suluhisho mbadala kwani tukio 
baada hasira linaweza likaifanya 
hali kuwa mbaya zaidi.

6.USILIMBIKIZE MATUKIO 

Kusamehe matukio yaliyopita 
na kuyasahau 
ni njia inayopunguza uzito wa 
tukio jipya.
Ukisamehe watu waliokukosea utakuwa umejisaidia mwenyewe na 
wao pia kujifunza kitu kutokana 
na tukio hilo.
Kwani usitarajie binadamu mwenzako awe
 vile vile 
unavyotaka na kutamani wewe awe.

7.TAFUTA MSAADA

Jinsi ya kuzuia 
hasira ni
 changamoto kwa kila binadamu,
kwani ukishindwa kuzizuia na 
ukachukua uamuzi mbaya unawaumiza watu wanaokuzunguka.
Kwa hiyo chagua mtu wako ambaye utakuwa unaenda kuomba msaada wa ushauri 
kutokana na 
tukio lililokuudhi.

KUKASIRIKA SI DHAMBI 
ILA INAONYESHA KUWA AKILI YAKO 
INA AFYA YA KUJUA KIPI HUPENDI NA KIPI UNAPENDA KUFANYIWA.

LAKINI 
UNATAKIWA UZITAWALE HASIRA 
PALE UNAPOONA ZITAKUPELEKA KATIKA KUFANYA TUKIO BAYA DHIDI YA MWENGINE.

Njia pekee ya kutunza pesa ni
 kupunguza matumizi 
yasiyo ya lazima.
Unachohitaji ni kujua pesa unatumia 
zaidi kwenye nini,
hapo ndipo utakapojua ufanye nini ili kupunguza matumizi.

Kila mara
 weka akilini kuwa yawezekana 
unanunua kitu kwa bei rahisi
 lakini 
jiulize ufanisi wake una umuhimu wowote 
au ni kutimiza wajibu tu.

Tambua mahitaji yako 
halafu 
fanya hesabu za namna ya kutumia unachokipata kwa uangalifu.
Tambua kuwa
 ili kupunguza matumizi kufanikiwe ni lazima ubadilishe mfumo wako wa maisha na namna unavyofikiria.

Zifuatazo ni hatua unaweza kuzitumia kupunguza matumizi:

1.TAMBUA UNATUMIA PESA ZAKO KATIKA NINI ZAIDI

 Kama mpaka sasa hujui pesa 
zako unazitumia 
zaidi kwenye nini zoezi
 hili litakushinda.
Ukiwa hujui pesa yako 
unatumia kwenye nini hasa,
kila mara utakuwa mtu wa kushangaa tu 
kuwa hela yako imepungua.
Na wengine
 wanaweza kuwalaumu watu wao
 wa karibu kuwa wamewachukulia 
kumbe ni yeye mwenyewe ndiye aliyefanya matumizi.


2.EPUKA MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA

Kuna matumizi
 mengine hata wewe unayaona kabisa
 kuwa hayana ulazima 
lakini kwa kuwa 
ushazoea ndio unaona ni 
kitu cha kawaida.
Na hivi ndio
 vitu mbavyo unanunua hapa
 baada ya dakika tano ukimaliza kukitumia ushasahau kama hata ulitumia.

3.WEKA KIPAUMBELE CHA UNUNUZI

Weka mkakati wa muda mfupi
 wa kutunza pesa unayopata kwa ajili ya kununua kitu fulani ndani ya muda uliojiwekea.
 Kama kuna kitu 
unataka kununua ijue bei yake halafu anza mkakati wa kutunza pesa kwa ajili ya kukimiliki.
Hii itakusaidia kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

4.PUNGUZA MATUMIZI YA SIMU

Mawasiliano 
siku hizi ndio yamekuwa yanaongoza kwa matumizi makubwa ya pesa.
Ukiwa hujui muda gani  wa kupiga,
 na muda gani wa kutuma 
meseji utakuwa 
unajimaliza mwenyewe.
Unaweza ukaweka vipaumbele vya watu wa kuwasiliana nao.
Kama unafanya simu za biashara ni kitu kizuri lakini 
kama ni stori tupu hapo
 lazima ujizuie.


5.TENGENEZA ORODHA YA VITU VYA KUNUNUA

Unapoamua
 kuwa unataka kwenda kununua 
vitu fulani ni lazima uwe na orodha maalumu itakayokuongoza ili 
usitumie zaidi ya uliyopanga.
Usijiroge ukatoka nyumbani kwenda kununua vitu huku hujui nini hasa unaenda kununua na gharama yake ni shilingi ngapi?
Utakuja kujuta wakati ushafikia nyumbani ukiwa huna pesa kabisa.

PESA INAYOTUMIKA TU BILA KUJIONGEZA NI SAWA NA KUJIFILISI MWENYEWE.

ANZA LEO KUTUNZA KIDOGO UNACHOPATA ILI KESHO USIJE KUJILAUMU 
ZITAKAPOKWISHA KABISA.

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz