Laurie Notaro aliwahi kusema;

“If you really believe in what you're doing, work hard, take nothing personally and if something blocks one route, find another. Never give up”.

Kauli hii ikimaanisha;

 “Kama unaamini katika kile unachofanya, fanya kwa bidii, usifanye ubinafsi na kama kuna jambo litajitokeza kufunga njia moja, tafuta njia mbadala. Usikate tamaa”.

Kukata tamaa ni kitendo cha kuishiwa mbinu mbadala za kukamilisha jambo Fulani ulilokuwa unalifanya kwakuwa tu umekumbana na ugumu. Katika kila jambo tunalofanya huwa tuna matarajio ya kufanikiwa ila pia changamoto haziwezi kuepukika.


Maneno “Kata” na “Tamaa” hayatakiwi kuwa pamoja. Hata neno hapana halipaswi kuwa sehemu ya neno katika kamusi yako. Kuwa sehemu ya jamii ya watu Fulani katika dunia unakuwa ni kiumbe wa pekee kuwahi kutembea juu ya ardhi hii.

SABABU 8 ZA KWANINI HUTAKIWI KUKATA TAMAA

      1.UPO HAI,NA UNAWEZA



Yaani ilimradi una pumua pumzi ya uhai, hakuna uhalali wa wewe kusema kuna jambo limekushinda na unalikatia tamaa. Kama ukiweka akili na mawazo yako katika hilo jambo lazima utaweza kufanya japo kufanikisha sehemu yake. Hakuna lisilowezekana chini ya jua.

Christopher Reeve aliwahi kusema;
So many of our dreams at first seem impossible, then they seem improbable, and then, when we summon the will, they soon become inevitable.

Ikimaanisha; “Ndoto zetu nyingi kwa mara ya kwanza huonekana haziwezi kuwa kweli, baadae huonekana haziwezekani kabisa, ila, tunaipoita utayari wa kufanya ndani yetu, punde zinakuwa haziwezi kuepukika”

Udhuru pekee unaoweza kuutoa kwa kutoweza kutimiza ndoto zako ni ikiwa umekufa ila kama unaweza kusoma hapa, hakuna cha kukuzuia.

       2. AMINI KATIKA NDOTO ZAKO


Ukikata tamaa, unajikatia tamaa mwenyewe na si mtu mwengine yeyote. Usijiuze mwenyewe wala kuruhusu mtu mwengine akurudishe nyuma. Kama unaweza kuwa na ndoto zako mwenyewe basi hata uwezo wa kutimiza unao.

Kuna mamilioni ya watu wa kale waliokuwana na ndoto zao katika ulimwengu huu, kama na wao wangekata tamaa hapo mwanzo hii dunia isingekuwa hivi unavyoiona leo.

Chukulia mfano ndugu wawili kutoka katika familia ya Wright waliokuwa wana ndoto za kutengeneza ndege jinsi walivyokumbana  na vikwazo vya kuifanya ndogo yao kuwa kweli huku hakuna aliyedhani kama ndoto inawezekana kwa kuwacheka na kejeli. Hawakukatishwa tamaa ila walipambana kuifanya ndoto yao kuwa kweli na walifanikiwa, je usafiri wa ndege si kiunganishi muhimu katika dunia ya leo?

Langston Hughes aliwahi kusema;
“Hold fast to your dreams, for without them life is a broken winged bird that cannot fly.

Ikimaanisha;
“Shikamana na ndoto zako, kwakuwa bila ya hizo maisha ni sawa na ndege aliyevunjika mabawa asiyeweza kuruka”

      3.UNA KILA KITU UNACHOTAKA

Kila unahohitaji ili kufikia malengo yako, kimewekwa tayari ndani yako. Usiwe mtu wa kutoa udhuru, kama inawezekana kuwa na wanamichezo walemavu wenye uwezo wa kushiriki michezo katika kiwango cha olimpiki,mapungufu yako hayawezi kukuzuia kutimiza ndoto yako. Mshukuru Mungu na tumia uwezo aliokupa kufanikisha ndoto zako.

      4. HAUHITAJI KUJA KUJUTA

Majuto ni hisia mbaya sana mtu kuwa nayo. Usiruhusu nafsi yako ijiweke katika mazingira ya kuja kujuta ila unapaswa ufanye unachotakiwa kufanya sasa.

Rory Cochrane alisema;
“I do not regret the things I've done, but those I did not do

Ikimaanisha;
“Sijutii kwa vitu nilivyofanya, ila kwa yale yote ambayo sikuyafanya”

      5.UNATAKIWA UJITHIBITISHIE MWENYEWE


Unatakiwa uje ujithibitishie mwenyewe na ulimwengu mzima kwamba unaweza kufanya jambo. Usiruhusu jambo au kitu chochote kikuzuie kutimiza ndoto zako.

Kushindwa kwa kweli si kule kujaribu na kukosa, bali ni kule kutojaribu kabisa.
Wewe unaweza kutimiza ndoto zako, sababu wanaoshindwa ni watu wasiofanikiwa daima.

      6.UTAPATA MABADILIKO MAZURI


Inawezekana kabisa unapitia wakati mgumu sasa, lakini ukishikilia kwa muda utapata mabadiliko ya haraka na mazuri. Kama utaendelea kupambana hutakiwi kukata tamaa sababu huwezi jua lini ndio siku yako ya kutoboa.

Usiwe kama mtu anayechimba kisima ambaye hadi anafika mita 50 hajapata maji, anakata tamaa na kuacha lakini anakuja mwengine anachimba mita 1 tu toka pale alipoishia yeye anakutana na maji. Kama umeamua fanya kweli mpaka upate matokeo.

      7.UNAPASWA KUTIMIZA

Si kila mtu anaweza kusikia sauti ya ndani inayomwambia afanye jambo Fulani, ila kama wewe umeweza kuisikia ikikwambia timiza jambo Fulani, nakwambia usiachie bila kutimiza sababu umeumbwa ili kufanikisha hilo.

      8.HAMASISHA WENGINE

Katika maisha yetu lazima kuna watu uliowazidi watakuwa wanakuangalia kama mtu wao wa mfano, mathalani wadogo zako au hata watu wa karibu na majirani. Sasa wanapokuona wewe umekata tamaa inawakatisha tama hata wao. 

Ndio maana hutakiwi kukata tamaa sababu hujui wangapi wanakuangalia, ushindi wako utawapa hata wao nguvu ya kupambana katika safari yao kwa kuwa walishawahi kuona Fulani aliweza.



Kuna idadi ya kutosha ya mitazamo chanya ndani yako ambayo pengine haujaweza kuitambua na inasubiri kuamshwa. Na kila wakati unapopoteza motisha unapaswa kujikumbusha kwa haraka uwezo wako. 

Daima kumbuka kwamba ladha ya mafanikio daima inakabiliwa na kushindwa kwa muda. Kama wewe utakata tamaa kutokana na magumu ya muda utakuwa unajiandaa kushindwa, lakini kama wewe utaendelea kupambana utakuwa na mafanikio.

Si kila mwenye mafaniko leo hii,
 aliyapata kwa mara ya kwanza
 alipojaribu.
Mara nyingi ni watu ambao walijaribu mara nyingi bila mafanikio,
 kabla hawajapatia na 
kufanikiwa.

Na wengi wao ni wale,
 waliokuwa wamejitolea kupambana 
na vikwazo 
kutoka kwa watu
 mbali mbali na mifumo.

Wanapovuka hatua hii ya vikwazo,
 wengi wao 
wanakosa majibu ya moja kwa moja wamefikaje hatua hiyo
 ya mfanikio pamoja na vikwazo vyote walivyokutana navyo.

Kuna siri imejificha hapa?
Ndio, 
kushindwa mara nyingi na bado kuendelea kunga'ang'ania mpaka unashinda,
 inaonyesha kuna kitu
 alikiona hapo.

Ni kipi hicho?
Nadhani,
 tunahitaji makala itakayojitegemea, 
kuelezea siri iliyopo 
hapa kwa watu wengi
 waliofanikiwa.

Unapopatwa na wakati mgumu,
 iwe katika masomo au kazini 
hupaswi kukata tamaa mapema 
bali 
tumia historia fupi za watu hawa kujitia 
nguvu ya kusonga 
mbele.

Watu hawa waliofanikiwa wapo katika makundi makuu 8.
Leo tunaanza na kundi la kwanza la 
wafanya biashara.

1.Henry Ford:

Huyu ni mfanyabiashara raia wa Marekani,
alizaliwa 
30 julai 1863 katika familia ya wakulima wadogo,
 na kufa 7 Aprili 1947.
Ndiye aliyeanzisha
 kampuni kubwa ya magari aina ya Ford.
 Aliondoka kwao,
 akiwa na miaka 16 tu
 na kwenda kutafuta 
ajira ya umakenika.
Kabla hajafanikiwa,
 alifilisika kibiashara mara tano.
 Alianza kuonja mafanikio baada ya kubuni 
gari la kwanza kutengenezwa 
Marekani aina ya 
Ford Model T.


2.R. H. Macy:

Ni raia wa Marekani
 ambaye alikuja kuanzisha 
biashara ya idara ya stoo kubwa za biashara
 katika jiji la
NewYork.
Alizaliwa 30 Agosti 1822 na 
kufariki 29 machi 1877.
Kabla hajafanikiwa katika wazo hili alifeli mara saba.

3.F.W. Woolworth:
Huyu ni raia wa Marekani ambaye alifanya kazi katika stoo ya bidhaa ya 
mfanyabishara mwengine,
ambako alipokea manyanyaso 
mengi hadi yakamfanya 
aamue kukaa chini na 
kupata wazo la yeye kufungua stoo zake mwenyewe za biashara.
Alizaliwa 13 Aprili 1852 na
kufa 8 Aprili 1919. 
Hata huku Tanzania kuna maduka yenye hili 
jina lake moja 
maeneo ya Posta PPF Tower.

4.Soichiro Honda:
Ni raia wa Japan,
na muanzilishi wa kampuni ya Honda.
Aliwahi mara kadhaa kuomba 
kazi katika kampuni ya
 Toyota kama injinia,
lakini alikosa baada ya 
kufanyiwa usaili na 
kuonekana hana vigezo.
Alikaa muda mrefu sana bila kuwa na 
kazi,
 kitu kilichomfanya 
akae chini kufikiria na kuibuka na 
wazo la 
kampuni ya Honda.
Alizaliwa 17 Novemba 1906 na
 kufa 5 Agosti 1991.
 Ambayo imekuja kuwa mpinzani wa kampuni iliyomkataa.

5.Akio Morita:
Ni raia wa Japan,
na muanzilishi wa
 kampuni ya Sony.
Bidhaa yake ya kwanza,
 kuanzisha ilikuwa ni 
jiko la kupikia mchele(Rice cooker) 
ambayo ilikuwa inaunguza sana wali hivyo watu waliacha kununua bidhaa hiyo.
Lakini,
 hakukata tamaa mpaka 
alipokuja kuboresha na 
kuja kukubalika tena na bidhaa 
nyingi tofauti tofauti
 za vifaa vinavyotumia umeme.
Alizaliwa 26 Januari 1921
na kufa 3 Oktoba 1999.

6.Bill Gates:

Ni raia wa Marekani,
alizaliwa 28 Oktoba 1955 mpaka leo bado anadunda.
Alianza na mkosi wa kufukuzwa
 chuo cha Harvard
ambapo aliamua kuanzisha biashara 
na mwenzake kwa jina la kampuni 
iliyoitwa Traf-O-Data 
ambayo 
haikufanikiwa kabisa.
Alipopata wazo la kutengeneza kompyuta alilipeleka katika kampuni moja ambapo lilikataliwa.
Hakukata tamaa na mwisho wa uvumilivu wote akaja na kampuni ya 
Microsoft ambayo imempa utajiri 
usioelezeka.

7.Harland David Sanders:
Ni raia wa Marekani,
na muanzilishi wa kampuni ya kukaanga kuku ya Kentucky Fried Chicken(KFC).
Alipoanza hii biashara alikataliwa mara 1,009 na migahawa ya Marekani kumpa 
oda ya kuku anaouza.
Lakini uvumilivu wake ukaja kumpa mafanikio makubwa katika biashara hiyo hiyo.
Alizaliwa 9 Septemba 1890 na 
kufa 16 Desemba 1980.

8.Walt Disney:
Kwa wale wapenzi wa 
filamu na katuni,
huyu ndio mtu aliyewaingizia 
hiyo burudani kwa mafanikio sana.
Alianza kwa kufanya kazi ya 
uhariri wa gazeti 
ambapo alifukuzwa kwa 
kuonekana hana ubunifu.
Na alikuja kuanzisha miradi 
 mbali mbali ambayo haikuweza kudumu muda mrefu na kumfilisi kabisa.
Lakini mwisho wa uvumilivu wake akaja kufanikiwa katika 
kampuni yake ya Disney ambayo 
inajihusisha na filamu na katuni.
Alizaliwa 5 Desemba 1901 na 
kufa 15 Desemba 1966.

USIOGOPE KUSHINDWA,
KILA KITU USIPOJARIBU
 HAUTAWEZA KUKIJUA KAMWE.

KAMA WEWE UNATAKA KUFANYA BIASHARA 
AU 
ULISHAANZA,
 UKISHIDWA USIKATE TAMAA.
 ENDELEA KUNG'ANG'ANIA KAMA 
UNAJUA NDICHO KITU PEKEE UNACHOWEZA KUFANYA 
KATIKA MAISHA YAKO.

USIKATISHWE TAMAA NA WAFANYABIASHARA AMBAO WANADHANI WANAFAHAMU KILA KITU ,
KWA KUKOSOA WAZO LAKO.
 NAO PIA KUNA VITU HAWAJUI HATA KAMA WAMESHAFANIKIWA KWA HIYO PIGANIA ULICHONACHO.

                                VIZA 
             Viza ni cheti au muhuri maalumu unaowekwa 
(katika hati ya kusafiria ya mwombaji) na mamlaka ya uhamiaji ya            nchi husika ambayo mwombaji anataka kutembelea,
alama hii ina maanisha mwombaji amepewa ruhusa ya kuingia nchi                           husika kwa muda maalumu.
Kuna viza ambazo zinaweza kukuruhusu uingie mara moja na kutoka                         (Single entry visa) na 
kuna viza nyingine zinakuruhusu kuingia na kurudi zaidi ya mara             mpaka pale muda uliopangwa kuisha matumizi ufike 
                     (multiple entry visa).


                             Viza za muda
Kuna aina mbali mbali za viza za muda zinazotolewa na ubalozi wa Marekani. Aina hizi za viza zinatambulika na sheria ya Uhamiaji ya Marekani(Immigration Law)na inaenda sambamba na dhumuni la kusafiri mwombaji.

Viza hizi zimewekwa kwa ajiri ya wasafiri ambao wana nia ya kukaa Marekani kwa muda na kurudi nchini kwao.
             Aina za Viza za muda ni pamoja na:
               .       Biashara na Utalii (Mapumziko)
2              .       Matibabu
               .       Wanafunzi
     .       Mwanadiplomasia, Maofisa wa serikali, na Wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa 
               .       Wageni wa kubadilishana.
               .       Wafanyakazi wa muda
7              .       Waandishi wa habari
8              .       Wafanyakazi wa mashirika ya dini

         A.      Biashara na Utalii (Mapumziko)

Kutokana na dhumuni lako hili la kwenda Marekani, Unahitaji aina hizi za Visa B1, B2 au B1/B2 viza.

                  B1-Waingiaji wa muda Kibiashara
Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina gani ili uweze kufanya biashara Marekani?
Kama unataka kuingia Marekani kwa dhumuni la biashara unahitaji aina hii ya viza. Viza hii haitakuruhusu ukubali ajira Marekani,lakini unaweza kukubaliana mkataba, mashauriano na washirika wa kibiashara,kukutana na wateja,kushiriki makongamano na semina na kuchukua oda za wateja.
                           
       
              B2-Waingiaji wa muda Utalii (Mapumziko)
 Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina gani ili uweze kufanya utalii au kutembelea marafiki Marekani? 
Unahitaji viza hii kama una dhumuni la kuingia marekani kwa ajiri ya mapumziko, au kuitembelea familia na marafiki.

     B1/B2- Waingiaji wa muda wa biashara au utalii (Mapumziko)

Umewahi kujiuliza kama unataka kutembelea maonyesho ya biashara halafu ukitoka hapo ukashangae shangae kidogo mambo mengine?
Unahitaji viza aina ya B1/B2 kama unataka kwenda Marekani kwa dhumuni la ama biashara au mapumziko au kwa shughuli maalumu,elimu, dini, makongamano ya kitaaluma,kozi za muda mfupi, kushauriana na washirika wa kibiashara au wataalamu,kutibiwa, kushiriki katika shughuli za kujitolea katika mashirika ya misaada au kushiriki katika michezo.


                      B.      Matibabu

Ili hali yako ya ugonjwa ipewe kipaumbele unapoomba viza unatakiwa                        uwe na taarifa zifuatavyo:                       
   a) Barua iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kutoka kwa daktari wako wa hapa Tanzania:
-          Ikielezea hali yako ya ugonjwa;
-          Inayofafanua chanzo cha ugonjwa na sababu za kuhitaji matibabu Marekani.

   b)      Ushahidi wa fedha ya kutosha kwa matibabu:
-          Ushahidi wa ufadhili wa kifedha au hati ya kiapo cha ufadhili (Fomu 1-134) kutoka kwa mfadhili. Zinatakiwa hati halisi tu-faksi na nukushi hazikubaliwi.
-          Uhakika kutoka kwa mfadhili kwamba mgonjwa atakuwa na tiketi ya kurudi.
-          Barua kutoka kwa mwajiri wa mfadhili  ikiwa na anuani ya kampuni ikieleza cheo chake kazini, mshahara, na mwisho wa ajira yake.
-          Barua kutoka benki ya mfadhili ikiwa na anuani ya benki  na ikiwa imesainiwa na ofisa wa benki.
-          Ripoti ya ulipaji kodi wa mfadhili kwa mwaka uliopita.


    c)       Barua binafsi ya mfadhili kwenda ubalozi wa Marekani
-          Ikieleza wapi hasa mgonjwa atafikia wakati wote ambao atakuwa anahudhuria matibabu.
-          Ikielezea kwa nini ameamua kumfadhili mgonjwa (mwombaji wa viza), Historia kamili ya uhusiano wao, ni wa vipi na ulianza linin a anatarajia kupata nini kutokana na ufadhili wake.

    d)      Barua kutoka kwa daktari wa Marekani:
-          Ikieleza hali ya mgonjwa na utayari wa kumtibu.
-          Makadirio ya juu na ya chini ya kipindi atakachokuwa         anamtibu mgonjwa
-          Makadirio ya juu na ya chini ya gharama za matibabu (Ada       ya daktari, ada ya hospitali, gharama za vipimo,        gharama za dawa na gharama zote zitakazohusiana matibabu)
-          Uhakika kwamba gharama za matibabu zitalipwa na fungu       lipo tayari kwa ajili ya kugharamia.
-          Tarehe maalumu ya ahadi.

Sheria ya uhamiaji ya taifa la Marekani imeweka dhahania kuwa       waombaji wote wa viza za muda wana nia ya kukaa Marekani moja kwa moja. 
Kwahiyo kuwa na vigezo vya kupata aina hizi za viza za muda unahitaji kuwathibitishia kuwa dhahania yao si sawa kwako na hauna   nia ya kukaa moja kwa moja.

Unaweza kuishinda hii dhahania yao kwa kuwapa ushahidi kuwa wewe una mambo ya msingi yatakayo kurudisha nyumbani na wala huna nia ya     kuikimbia nchi yako.

Itaendelea.....

Majanga ya asili(Natural Disasters) ni matukio yanayotokea kwa wingi duniani hutumia muda mfupi lakini madhara yake huwa ni makubwa.
Katika muda mfupi yanayotumia huondoa maisha na kujeruhi watu pamoja na uharibu wa mali.
Majanga haya huwa hayana eneo maalumu popote yanaweza kutokea japo kuna baadhi ya maeneo huwa ni mara kwa mara yanajirudia.

Mara nyingi unapowauliza mashuhuda wa matukio haya ya majanga ya asili hukosa jibu kamili la kilichotokea, kwa mfano mashuhuda wengi wa kimbunga watakwambia "Niliona joka kubwa likitua juu ya nyumba na kuibomoa yote!!"
  
Hii inaashiria wakati majanga haya yanatokea taswira ya dunia huwa ni tofauti kabisa, ni kama ya mtu aliyekasirika na kukunja uso.
Hebu tujaribu kuyajua majanga 5 makubwa ambayo yanapotokea uharibifu wake huwa ni mkubwa sana.
1.UMEME(lightning):
Umeme hutokea pale ambapo kunakosekana ulingani wa chaji za umeme katika anga(Electric charge unbalance).
Kitendo hiki husababisha eneo moja la mawingu lenye chaji nyingi, kuachilia chaji zake(Electrostatic Discharge),ili kwenda kujaza eneo lililopungukiwa na hivyo chaji hizo zinapokutana na chaji za mawingu mengine zinazolingana husababisha kusukumana na kuanguka na kuambatana na sauti kubwa ya radi(Thunder).

2.MOTO WA MSITUNI(WILD FIRE)
Nyasi ndogo za msituni zinapopigwa na jua kwa muda mrefuhukauka kabisa na kuanza kushika moto.
Matukio ya moto wa msituni hutokea zaidi katika majira ya kiangazi na kipupwe ambapo huchangia kusambaa kwa kasi kwani matawi mengi ya miti huwa yamekauka hivyo kushika haraka moto huo na unachagizwa zaidi na upepo mkali.

3.MLIPUKO WA VOLKANO(VOLCANIC ERUPTION):
Magma iliyoyeyuka chini ya miamba husababisha mlipuko wa miamba pale inapopigwa presha kupita katika njia ndogo na hivyo huruka juu na kuanza kusambaa juu ya ardhi.

4.BANGUKO(AVALANCHE):
Huu ni muanguko wa mapande makubwa ya barafu kutoka juu milimani na kushuka chini kwa kasi kubwa na kuleta uharibifu kwa wakazi wa karibu na eneo husika.

5.MAJIVU YA VOLKANO(VOLCANIC ASH):
Janga hutokea pale ambapo volkano imelipuka na kutoa majivu mazito ya miamba iliyosagwa angani.
Wataalamu wanasema moshi huu ndio huchangia kuua watu wengi kwani huwa na sumu. 
Kwa mfano Mlima mmoja Iceland mwaka 2011 ulipo lipuka na kutoa hayo majivu mazito yalisukumwa na upepo na kusababisha nchi nyingi za ulaya kusitisha safari zao za ndege.

 6.KIMBUNGA(HURRICANES):
Ni dhoruba kubwa inayoweza kuchukua eneo la umbali hadi wa maili 600 ikiambatana na upepo mkali unaozunguka na kuelekea juu kwa kasi ya maili 75 mpaka 200 kwa saa.

7.DHORUBA YA MCHANGA(SANDSTORMS):
Dhoruba hii hutokea pale ambapo upepo mkali unapovuma eneo ambalo lina mchanga mwingi ulioachana na kuunyanyua kuelekea unapoelekea wenyewe.

8.TSUNAMI

Hili ni dhoruba linaloanzia katika kina cha bahari ambapo miamba iliyoshikamana, inapoachana huku mmoja unaelekea chini na mwengine juu unasababisha kunyanyuka na maji kuelekea ufukweni.
Hali hiyo husababisha maji kuingia kwa kasi maeneo ya kuishi watu na kufanya uharibifu.

9.TORNADO(KIMBUNGA CHA NCHI KAVU):
Huu ni mkusanyiko mkubwa wa hewa inayozunguka ikiwa imeshuka hadi kugusana na ardhi ambayo inaweza kuanzishwa na umeme unavyotokea.
Kuzunguka huko kwa hewa iliyo kwenye kasi kubwa husababisha kuzoa na kuharibu kitu chochote itakachokutana nacho.

10.TETEMEKO LA ARDHI(EARTHQUAKES):
Hili janga husababishwa na mpasuko miamba wa chini ya ardhi ambapo hupelekea nguvu ya mawimbi ya seismic(Seismic waves) kuzalishwa na kusababisha ardhi kutikisika.
Haya majanga yote yana madhara makubwa pindi yanapotokea eneo lolote juu ya uso wa dunia.









 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz