Laurie Notaro aliwahi kusema;
“If you really believe
in what you're doing, work hard, take nothing personally and if something
blocks one route, find another. Never give up”.
Kauli hii ikimaanisha;
“Kama unaamini katika kile unachofanya, fanya
kwa bidii, usifanye ubinafsi na kama kuna jambo litajitokeza kufunga njia moja,
tafuta njia mbadala. Usikate tamaa”.
Kukata tamaa ni kitendo cha kuishiwa mbinu mbadala za
kukamilisha jambo Fulani ulilokuwa unalifanya kwakuwa tu umekumbana na ugumu.
Katika kila jambo tunalofanya huwa tuna matarajio ya kufanikiwa ila pia
changamoto haziwezi kuepukika.
Maneno “Kata” na “Tamaa” hayatakiwi kuwa pamoja. Hata neno
hapana halipaswi kuwa sehemu ya neno katika kamusi yako. Kuwa sehemu ya jamii
ya watu Fulani katika dunia unakuwa ni kiumbe wa pekee kuwahi kutembea juu ya
ardhi hii.
SABABU 8 ZA KWANINI HUTAKIWI KUKATA TAMAA
1.UPO
HAI,NA UNAWEZA
Yaani ilimradi una pumua pumzi ya
uhai, hakuna uhalali wa wewe kusema kuna jambo limekushinda na unalikatia
tamaa. Kama ukiweka akili na mawazo yako katika hilo jambo lazima utaweza
kufanya japo kufanikisha sehemu yake. Hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Christopher Reeve aliwahi kusema;
“So many of our dreams at first seem impossible, then they
seem improbable, and then, when we summon the will, they soon become
inevitable.
Ikimaanisha; “Ndoto zetu nyingi kwa mara ya kwanza huonekana haziwezi
kuwa kweli, baadae huonekana haziwezekani kabisa, ila, tunaipoita utayari wa
kufanya ndani yetu, punde zinakuwa haziwezi kuepukika”
Udhuru pekee unaoweza kuutoa kwa kutoweza kutimiza ndoto zako ni ikiwa
umekufa ila kama unaweza kusoma hapa, hakuna cha kukuzuia.
2. AMINI KATIKA NDOTO ZAKO
Ukikata tamaa, unajikatia tamaa mwenyewe na si mtu mwengine yeyote.
Usijiuze mwenyewe wala kuruhusu mtu mwengine akurudishe nyuma. Kama unaweza
kuwa na ndoto zako mwenyewe basi hata uwezo wa kutimiza unao.
Kuna mamilioni ya watu wa kale waliokuwana na ndoto zao katika ulimwengu
huu, kama na wao wangekata tamaa hapo mwanzo hii dunia isingekuwa hivi
unavyoiona leo.
Chukulia mfano ndugu wawili kutoka katika familia ya Wright waliokuwa
wana ndoto za kutengeneza ndege jinsi walivyokumbana na vikwazo vya kuifanya ndogo yao kuwa kweli
huku hakuna aliyedhani kama ndoto inawezekana kwa kuwacheka na kejeli.
Hawakukatishwa tamaa ila walipambana kuifanya ndoto yao kuwa kweli na walifanikiwa,
je usafiri wa ndege si kiunganishi muhimu katika dunia ya leo?
Langston Hughes aliwahi kusema;
“Hold fast to your dreams, for without them life is a broken winged
bird that cannot fly.”
Ikimaanisha;
“Shikamana na ndoto zako, kwakuwa bila ya hizo maisha ni sawa na ndege
aliyevunjika mabawa asiyeweza kuruka”
3.UNA
KILA KITU UNACHOTAKA
Kila unahohitaji ili kufikia malengo yako, kimewekwa tayari ndani
yako. Usiwe mtu wa kutoa udhuru, kama inawezekana kuwa na wanamichezo walemavu
wenye uwezo wa kushiriki michezo katika kiwango cha olimpiki,mapungufu yako hayawezi
kukuzuia kutimiza ndoto yako. Mshukuru Mungu na tumia uwezo aliokupa
kufanikisha ndoto zako.
4. HAUHITAJI
KUJA KUJUTA
Majuto ni hisia mbaya sana mtu kuwa nayo. Usiruhusu nafsi yako ijiweke
katika mazingira ya kuja kujuta ila unapaswa ufanye unachotakiwa kufanya sasa.
Rory Cochrane alisema;
“I do not regret the things I've done, but those I did not do”
Ikimaanisha;
“Sijutii kwa vitu nilivyofanya, ila kwa yale yote ambayo sikuyafanya”
5.UNATAKIWA
UJITHIBITISHIE MWENYEWE
Unatakiwa uje ujithibitishie mwenyewe na ulimwengu mzima kwamba unaweza
kufanya jambo. Usiruhusu jambo au kitu chochote kikuzuie kutimiza ndoto zako.
Kushindwa kwa kweli si kule kujaribu na kukosa, bali ni kule
kutojaribu kabisa.
Wewe unaweza kutimiza ndoto zako, sababu wanaoshindwa ni watu wasiofanikiwa
daima.
6.UTAPATA MABADILIKO MAZURI
Inawezekana kabisa unapitia wakati mgumu sasa, lakini ukishikilia kwa
muda utapata mabadiliko ya haraka na mazuri. Kama utaendelea kupambana hutakiwi
kukata tamaa sababu huwezi jua lini ndio siku yako ya kutoboa.
Usiwe kama mtu anayechimba kisima ambaye hadi anafika mita 50 hajapata
maji, anakata tamaa na kuacha lakini anakuja mwengine anachimba mita 1 tu toka
pale alipoishia yeye anakutana na maji. Kama umeamua fanya kweli mpaka upate
matokeo.
7.UNAPASWA KUTIMIZA
Si kila mtu anaweza kusikia sauti ya ndani inayomwambia afanye jambo Fulani,
ila kama wewe umeweza kuisikia ikikwambia timiza jambo Fulani, nakwambia
usiachie bila kutimiza sababu umeumbwa ili kufanikisha hilo.
8.HAMASISHA
WENGINE
Katika maisha yetu lazima kuna watu
uliowazidi watakuwa wanakuangalia kama mtu wao wa mfano, mathalani wadogo zako
au hata watu wa karibu na majirani. Sasa wanapokuona wewe umekata tamaa
inawakatisha tama hata wao.
Ndio maana hutakiwi kukata tamaa sababu hujui
wangapi wanakuangalia, ushindi wako utawapa hata wao nguvu ya kupambana katika safari
yao kwa kuwa walishawahi kuona Fulani aliweza.
Kuna idadi ya kutosha ya mitazamo chanya ndani yako
ambayo pengine haujaweza kuitambua na inasubiri kuamshwa. Na kila wakati
unapopoteza motisha unapaswa kujikumbusha kwa haraka uwezo wako.
Daima kumbuka
kwamba ladha ya mafanikio daima inakabiliwa na kushindwa kwa muda. Kama wewe utakata
tamaa kutokana na magumu ya muda utakuwa unajiandaa kushindwa, lakini kama wewe
utaendelea kupambana utakuwa na mafanikio.
0 comments:
Post a Comment