Majanga ya asili(Natural Disasters) ni matukio yanayotokea kwa wingi duniani hutumia muda mfupi lakini madhara yake huwa ni makubwa.
Katika muda mfupi yanayotumia huondoa maisha na kujeruhi watu pamoja na uharibu wa mali.
Majanga haya huwa hayana eneo maalumu popote yanaweza kutokea japo kuna baadhi ya maeneo huwa ni mara kwa mara yanajirudia.

Mara nyingi unapowauliza mashuhuda wa matukio haya ya majanga ya asili hukosa jibu kamili la kilichotokea, kwa mfano mashuhuda wengi wa kimbunga watakwambia "Niliona joka kubwa likitua juu ya nyumba na kuibomoa yote!!"
  
Hii inaashiria wakati majanga haya yanatokea taswira ya dunia huwa ni tofauti kabisa, ni kama ya mtu aliyekasirika na kukunja uso.
Hebu tujaribu kuyajua majanga 5 makubwa ambayo yanapotokea uharibifu wake huwa ni mkubwa sana.
1.UMEME(lightning):
Umeme hutokea pale ambapo kunakosekana ulingani wa chaji za umeme katika anga(Electric charge unbalance).
Kitendo hiki husababisha eneo moja la mawingu lenye chaji nyingi, kuachilia chaji zake(Electrostatic Discharge),ili kwenda kujaza eneo lililopungukiwa na hivyo chaji hizo zinapokutana na chaji za mawingu mengine zinazolingana husababisha kusukumana na kuanguka na kuambatana na sauti kubwa ya radi(Thunder).

2.MOTO WA MSITUNI(WILD FIRE)
Nyasi ndogo za msituni zinapopigwa na jua kwa muda mrefuhukauka kabisa na kuanza kushika moto.
Matukio ya moto wa msituni hutokea zaidi katika majira ya kiangazi na kipupwe ambapo huchangia kusambaa kwa kasi kwani matawi mengi ya miti huwa yamekauka hivyo kushika haraka moto huo na unachagizwa zaidi na upepo mkali.

3.MLIPUKO WA VOLKANO(VOLCANIC ERUPTION):
Magma iliyoyeyuka chini ya miamba husababisha mlipuko wa miamba pale inapopigwa presha kupita katika njia ndogo na hivyo huruka juu na kuanza kusambaa juu ya ardhi.

4.BANGUKO(AVALANCHE):
Huu ni muanguko wa mapande makubwa ya barafu kutoka juu milimani na kushuka chini kwa kasi kubwa na kuleta uharibifu kwa wakazi wa karibu na eneo husika.

5.MAJIVU YA VOLKANO(VOLCANIC ASH):
Janga hutokea pale ambapo volkano imelipuka na kutoa majivu mazito ya miamba iliyosagwa angani.
Wataalamu wanasema moshi huu ndio huchangia kuua watu wengi kwani huwa na sumu. 
Kwa mfano Mlima mmoja Iceland mwaka 2011 ulipo lipuka na kutoa hayo majivu mazito yalisukumwa na upepo na kusababisha nchi nyingi za ulaya kusitisha safari zao za ndege.

 6.KIMBUNGA(HURRICANES):
Ni dhoruba kubwa inayoweza kuchukua eneo la umbali hadi wa maili 600 ikiambatana na upepo mkali unaozunguka na kuelekea juu kwa kasi ya maili 75 mpaka 200 kwa saa.

7.DHORUBA YA MCHANGA(SANDSTORMS):
Dhoruba hii hutokea pale ambapo upepo mkali unapovuma eneo ambalo lina mchanga mwingi ulioachana na kuunyanyua kuelekea unapoelekea wenyewe.

8.TSUNAMI

Hili ni dhoruba linaloanzia katika kina cha bahari ambapo miamba iliyoshikamana, inapoachana huku mmoja unaelekea chini na mwengine juu unasababisha kunyanyuka na maji kuelekea ufukweni.
Hali hiyo husababisha maji kuingia kwa kasi maeneo ya kuishi watu na kufanya uharibifu.

9.TORNADO(KIMBUNGA CHA NCHI KAVU):
Huu ni mkusanyiko mkubwa wa hewa inayozunguka ikiwa imeshuka hadi kugusana na ardhi ambayo inaweza kuanzishwa na umeme unavyotokea.
Kuzunguka huko kwa hewa iliyo kwenye kasi kubwa husababisha kuzoa na kuharibu kitu chochote itakachokutana nacho.

10.TETEMEKO LA ARDHI(EARTHQUAKES):
Hili janga husababishwa na mpasuko miamba wa chini ya ardhi ambapo hupelekea nguvu ya mawimbi ya seismic(Seismic waves) kuzalishwa na kusababisha ardhi kutikisika.
Haya majanga yote yana madhara makubwa pindi yanapotokea eneo lolote juu ya uso wa dunia.









Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz