VIZA
Viza ni cheti au muhuri maalumu unaowekwa
(katika hati ya
kusafiria ya mwombaji) na mamlaka ya uhamiaji ya nchi husika ambayo mwombaji
anataka kutembelea,
alama hii ina maanisha mwombaji amepewa ruhusa ya kuingia
nchi husika kwa muda maalumu.
Kuna viza ambazo zinaweza kukuruhusu uingie mara moja na
kutoka (Single entry visa) na
kuna viza nyingine zinakuruhusu kuingia na kurudi
zaidi ya mara mpaka pale muda uliopangwa kuisha matumizi ufike
(multiple entry visa).
Viza za muda
Kuna aina mbali mbali za viza za muda zinazotolewa na ubalozi wa Marekani. Aina hizi za viza zinatambulika na sheria ya Uhamiaji ya Marekani(Immigration Law)na inaenda sambamba na dhumuni la kusafiri mwombaji.
Kuna aina mbali mbali za viza za muda zinazotolewa na ubalozi wa Marekani. Aina hizi za viza zinatambulika na sheria ya Uhamiaji ya Marekani(Immigration Law)na inaenda sambamba na dhumuni la kusafiri mwombaji.
Viza hizi zimewekwa kwa ajiri ya wasafiri ambao wana nia ya
kukaa Marekani kwa muda na kurudi nchini kwao.
Aina za Viza za muda ni pamoja na:
.
Biashara na Utalii (Mapumziko)
2 .
Matibabu
.
Wanafunzi
.
Mwanadiplomasia, Maofisa wa serikali, na
Wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa
. Wageni wa kubadilishana.
. Wageni wa kubadilishana.
.
Wafanyakazi wa muda
7 .
Waandishi wa habari
8 .
Wafanyakazi wa mashirika ya dini
A.
Biashara na Utalii (Mapumziko)
Kutokana na dhumuni lako hili la kwenda
Marekani, Unahitaji aina hizi za Visa B1, B2 au B1/B2 viza.
B1-Waingiaji wa muda Kibiashara
Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina
gani ili uweze kufanya biashara Marekani?
Kama unataka kuingia Marekani kwa dhumuni
la biashara unahitaji aina hii ya viza. Viza hii haitakuruhusu ukubali ajira Marekani,lakini unaweza kukubaliana mkataba, mashauriano na washirika wa kibiashara,kukutana na wateja,kushiriki
makongamano na semina na kuchukua oda za wateja.
B2-Waingiaji wa muda Utalii (Mapumziko)
Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina gani ili uweze kufanya utalii au kutembelea marafiki Marekani?
Unahitaji viza hii kama una dhumuni la kuingia marekani kwa ajiri ya mapumziko, au kuitembelea familia na marafiki.
Umewahi kujiuliza unahitaji viza ya aina gani ili uweze kufanya utalii au kutembelea marafiki Marekani?
Unahitaji viza hii kama una dhumuni la kuingia marekani kwa ajiri ya mapumziko, au kuitembelea familia na marafiki.
B1/B2- Waingiaji wa muda wa biashara au utalii
(Mapumziko)
Umewahi kujiuliza kama unataka kutembelea maonyesho ya biashara halafu ukitoka hapo ukashangae shangae kidogo mambo
mengine?
Unahitaji viza aina ya B1/B2 kama unataka
kwenda Marekani kwa dhumuni la ama biashara au mapumziko au kwa shughuli
maalumu,elimu, dini, makongamano ya kitaaluma,kozi za muda mfupi, kushauriana
na washirika wa kibiashara au wataalamu,kutibiwa, kushiriki katika shughuli za
kujitolea katika mashirika ya misaada au kushiriki katika michezo.
B.
Matibabu
Ili hali yako ya ugonjwa ipewe kipaumbele
unapoomba viza unatakiwa uwe na taarifa zifuatavyo:
a) Barua iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza
kutoka kwa daktari wako wa hapa Tanzania:
-
Ikielezea hali yako ya ugonjwa;
-
Inayofafanua chanzo cha ugonjwa na sababu za
kuhitaji matibabu Marekani.
b)
Ushahidi wa fedha ya kutosha kwa matibabu:
-
Ushahidi wa ufadhili wa kifedha au hati ya kiapo
cha ufadhili (Fomu 1-134) kutoka kwa mfadhili. Zinatakiwa hati halisi tu-faksi
na nukushi hazikubaliwi.
-
Uhakika kutoka kwa mfadhili kwamba mgonjwa
atakuwa na tiketi ya kurudi.
-
Barua kutoka kwa mwajiri wa mfadhili ikiwa na anuani ya kampuni ikieleza cheo
chake kazini, mshahara, na mwisho wa ajira yake.
-
Barua kutoka benki ya mfadhili ikiwa na anuani
ya benki na ikiwa imesainiwa na ofisa wa
benki.
-
Ripoti ya ulipaji kodi wa mfadhili kwa mwaka
uliopita.
c)
Barua binafsi ya mfadhili kwenda ubalozi wa
Marekani
-
Ikieleza wapi hasa mgonjwa atafikia wakati wote
ambao atakuwa anahudhuria matibabu.
-
Ikielezea kwa nini ameamua kumfadhili mgonjwa
(mwombaji wa viza), Historia kamili ya uhusiano wao, ni wa vipi na ulianza linin
a anatarajia kupata nini kutokana na ufadhili wake.
d)
Barua kutoka kwa daktari wa Marekani:
-
Ikieleza hali ya mgonjwa na utayari wa kumtibu.
-
Makadirio ya juu na ya chini ya kipindi
atakachokuwa anamtibu mgonjwa
-
Makadirio ya juu na ya chini ya gharama za
matibabu (Ada ya daktari, ada ya hospitali, gharama za vipimo, gharama za dawa na
gharama zote zitakazohusiana matibabu)
-
Uhakika kwamba gharama za matibabu zitalipwa na
fungu lipo tayari kwa ajili ya kugharamia.
-
Tarehe maalumu ya ahadi.
Sheria
ya uhamiaji ya taifa la Marekani imeweka dhahania kuwa waombaji wote wa viza za
muda wana nia ya kukaa Marekani moja kwa moja.
Kwahiyo kuwa na vigezo vya kupata
aina hizi za viza za muda unahitaji kuwathibitishia kuwa dhahania yao si sawa
kwako na hauna nia ya kukaa moja kwa moja.
Unaweza
kuishinda hii dhahania yao kwa kuwapa ushahidi kuwa wewe una mambo ya msingi
yatakayo kurudisha nyumbani na wala huna nia ya kuikimbia nchi yako.
Itaendelea.....
9 comments:
Asante kwa elimu uliotupa, ila nina maswali mawili,
1:Malipo ya visa ni Tsh ngapi au $?
2:na vigezo au sababu za muhimu kuachia utalii mf nataka kwenda kuishi huko bt najua hawatakubali nitumie njia gani kwa.convince wanipe visa...? Asanteni
Asante kwa elimu uliotupa, ila nina maswali mawili,
1:Malipo ya visa ni Tsh ngapi au $?
2:na vigezo au sababu za muhimu kuachia utalii mf nataka kwenda kuishi huko bt najua hawatakubali nitumie njia gani kwa.convince wanipe visa...? Asanteni
Kwakweli nahitaji visa niende america kwa shughuli za kimuziki na kujifunza mambo machache huko nifanyaje??????
Naitwa john benoit naishi south Africa nikuwa napenda kujuwa bei ya visa ya marekani iko ku dollar ngapi ...pia na visa ya Australia pia iko ku dollars ngapi?
Visa
Naitwa Richard Frank niko dar nataka kujua njia gani za kufata ili kupata visa ya American maana nimejarbu kusoma hapo sipati majibu sahihi ya kufata
Nataka viza ya kwenda marecani kutembeaa je niende na vigezo au vitu gani wanavyo itaji ubalozi
Thanks for being given an education
Okay Asante sana kwa elimu.
Lakini naomba kujua nahitaji Nini ili nipaye B2 viza
Post a Comment