Uaminifu ni kitu muhimu kitakacho waonyesha watu wewe ni nani,
 na unafanya nini katika
 jamii inayokuzunguka.
Jamii yoyote inapenda kuishi na mtu ambaye anaeleweka na hana tabia ya kuongopa ongopa kwa wengine.

Kama umetoa ahadi fulani halafu umeshindwa kuitimiza,
ni heri ukaongea ukweli kuliko kutunga uongo ili upate kuaminiwa na wengine.

Yawezekana kabisa kuna ukweli fulani hautaki ujulikane na wenzako,
ni heri ukakaa kimya kuliko kuongea jambo la uongo ili kuuficha ukweli.

Je, kila jambo linalonihusu wengine wanapaswa kulijua undani wake?
Hapana, 
jambo lako liwe baya au zuri unapaswa wewe ndiye uamue kulisema au la,
lakini usitumie muda wako kusema uongo ili kulificha zaidi.
Na hapa ndio wengi wetu tunaingia katika mtego wa kuongopa kwa kujaribu kuuficha ukweli kupitia uongo.


Kama utaanza kuigiza hadi maisha ili tu uonekane mtu wa aina fulani na 
siku watu wakija kugundua uaminifu wao kwako utaondoka kabisa.
Ukiona watu wako wa karibu wanasema hausomeki yaani ujue bado hawajajua msimamo wako katika maisha uko wapi na hivyo kukuamini ni nadra sana.

Hebu leo tuangalie faida za kuwa muaminifu:

1.UNAJITENGENEZEA THAMANI MBELE YA WENGINE

Wenzako watajua umesimamia upande gani na wao wasimame upande gani kwako.
Ukiwa muaminifu kwa wengine unajitengenezea mazingira ya kuthaminiwa.
Na wenzako watajisikia wako salama wao na mali zao wanapokuwa karibu na wewe.
Ukiwa muaminifu huitaji kujieleza mbele za wengine ukoje bali tabia yako itajionesha tu na wao watakuelewa vizuri tu.

2.UNAKUWA HURU

Unapokuwa msema kweli hauna muda wa kujilaumu wala kulaumiwa kutokana na utakachoongea.
Moyoni mwako utakuwa unajua wazi kuwa ulichofanya au kuongea ni kitu sahihi kwahiyo hofu haitakuwepo kamwe.

3.URAHISI WA MAISHA

Ukiwa muaminifu unajitengenezea maisha mepesi kwani watu wanaokuzunguka hawataona tabu kukukopesha au kukuachia vitu vyao vya thamani.
Hata unapotaka kuzungumza kitu mbele za watu hutakuwa na kazi ngumu ya kufikiria namna ya kuongopa,
itakuwa tu aidha ndio au hapana na maelezo yako mafupi yenye ukweli ndani yake.

4.UTAJENGA KUJIAMINI

Hutokuwa na muda wa kutafakari kama watu wanakupenda au wanakuchukia 
kwasababu msema kweli siku zote hupendwa na wengi na hivyo utakuwa unajiamini mbele ya hiyo jamii yako,
 japo kuna wachache watakuchukia lakini usiwajali.

5.WATU WATAKUJALI

Hakuna binadamu anayependa kujenga uaminifu na mtu asiye mkweli.
Na wengi watakuwa bega kwa bega na wewe pale wanapoona upo katika hali tofauti na walioizoea,
kwa kujitokeza na kukupa msaada wa karibu unaouhitaji.

KUISHI MAISHA YA KUTOAMINIWA NA WATU NI KUJITESA SANA,
UTAJIKUTA UNAKOSA FURSA ZA MAISHA KWA KUWA TU WATU HAWAKUAMINI.

HEBU TUANZE LEO KUONYESHA UAMINIFU KWA WATU WETU WA KARIBU WANAOTUZUNGUKA ILI KILA MMOJA APATE KUJUA THAMANI YAKE.

Share this post:

Digg it StumbleUpon del.icio.us Google Yahoo! reddit

0 comments:

Post a Comment

 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz