JE, WEWE NI MMOJA KATI YA WATU WENYE AIBU MBELE ZA WATU WENGINE? SOMA UJIELIMISHE NAMNA YA KUPAMBANA NA HALI HIYO
Watu wenye aibu ndani yao wanafahamu fika kuwa kuna mambo mazuri yanawapita lakini wanahisi hawana jinsi ya kubadilisha hali hiyo.
Aibu kimahesabu ni sawa na:
AIBU = KUKOSA FURSA + KUKOSA FURAHA + KUFAHAMIANA NA WATU WACHACHE
Aibu ni kizuizi kikubwa sana kwa mwenye nayo kufikia mambo mazuri katika jamii.
Lakini naomba nikuambie hata kama wewe ni mmoja wao kuanzia leo
unaweza kubadilisha hali hiyo kwa kutumia hatua zifuatazo:
1.MTAZAMO WAKO JUU YA WATU WENGINE
Watu wenye aibu mara nyingi wanajaribu kujitofautisha na
watu wapya wanaokutana nao na kuwapa hadhi inayowazidi wao.
Hali hiyo itakufanya ujione huna jipya la kumueleza au kuzungumza mbele ya watu hao.
Unachopaswa kufanya ni
kumuona kila mtu mpya unayekutana naye kama wa kawaida na hana alichokuzidi na kwamba hata yeye kuna vitu hajui
au hana ambavyo wewe unavyo.
2.TAMBUA HATA WENGINE WANA AIBU PIA
Usijiweke peke yako kama ndio mtu mwenye aibu kupita wote na kwamba wengine
hawako kama wewe.
Kuanzia leo tambua kuwa kila mtu ameumbwa na aibu ndani yake pale anapokutana na mtu mpya kwahiyo ukiwa
mbele ya watu wapya
jua hata wao pia wanakuonea aibu kwa kuwa hawajui ulichonacho ni nini.
3.KUSANYA TAARIFA NYINGI KICHWANI
Mtu mwenye aibu siku zote hujiona hana chochote cha maana
kuwashirikisha wengine.
Kuna wengine wanakuwa kweli hawana vitu vya kuzungumza mbele za watu wengine na kuna wengine ni
kujidharau tu na kuona taarifa walizo nazo hazina maana.
Jaribu kuwa na tabia ya kusoma vitu vipya na kuwaeleza watu wengine
na hapo utafanya uwezo wako wa kusimama au kujitokeza mbele ya watu wengine kuwa mkubwa kwa kuwa kichwani
una kitu cha kuwashirikisha.
4.ONGEZA KUJIKUBALI
Ukiwa na tabia ya kujidharau mwenyewe na kujiona huna thamani
mbele ya wengine utafanya aibu ikuteke
daima.
Thamini uwezo wa pekee
ulionao na upe thamani kuwa hakuna mwengine alionao kwahiyo hata wewe
unaweza kuwaonyesha maajabu wasiyoyajua.
Ukijiweka katika kundi
hili hautakuwa muoga wa kuwasiliana
na watu wapya kila siku.
5.ACHA KUZIAMINI HISIA HASI
Mtu mwenye hofu siku zote anatengeneza hisia ndani yake kuwa baada
ya yeye kufanya au kusema jambo fulani
basi watu wengine watafanya
kitu fulani kwake.
Mathalani anaweza akaanza kuhisi kuwa baada ya yeye kukosea kitu
watu watamcheka au kumsema vibaya
kwa wengine.
Na anapoiamini hiyo picha kichwani kwake anaongeza aibu na kushindwa kuitumia fursa iliyopo mbele yake.
Na mara nyingi hizi hisia huwa hazina ukweli wowote katika matukio
halisi ila ni hofu tu anayojijengea mwenyewe.
Anza kujitengenezea hisia chanya kuwa watu watakupongeza kwa kujaribu.
KUNA MSEMO USEMAO:
"AIBU YAKO NDIO UMASIKINI WAKO"
HAINA UBISHI UKIENDEKEZA TABIA YA KUONA AIBU MBELE ZA WATU KAMWE HAKUNA FURSA UTAKAYOPATA.
TAMBUA PIA: "MAFANIKIO YA MTU YAPO MIKONONI MWA MTU"
NI KUPITIA BINADAMU WENZETU NDIO TUNAFIKIA NDOTO NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YETU HIVYO USIIACHE AIBU IKUTENGE NA NDOTO YAKO.
JE, WEWE NI MSIKILIZAJI MZURI WA MUZIKI, UNAFAHAMU NAMNA YA KUUTUMIA KUKUONGEZEA UFANISI KATIKA MAISHA? SOMA UJIELIMISHE
Muziki uko kila mahali tunapoenda,
iwe umeusikia kupitia redio,
katika mgahawa, nyumba za ibada au katika maeneo ya starehe.
Hakuna utafiti wowote uliowahi kufanywa ambao uliweza kuthibitisha madhara yanayotokana na mtu kusikiliza muziki,
ila tafiti nyingi zimeegemea katika kutoa faida za muziki katika maisha yetu ya kila siku.
Haijalishi aina gani ya muziki unaipenda sana kusikiliza ilimradi unaupenda utakusaidia kitu tu.
Hebu tuangalie faida japo chache ambazo zinaletwa na kusikiliza muziki.
1.KUTUNZA KUMBUKUMBU
Haijalishi sasa hivi una umri gani lakini kila mara kuna wimbo ukiusikia lazima utakukumbusha matukio yaliyopita ambapo wakati unapitia kipindi hicho wimbo huo ndio ulikuwa unapigwa.
Na utajikuta unaanza kufurahi na kuzidi kuziimarisha kumbukumbu zako za matukio ya zamani.
Si kitu cha ajabu kumsikia mtu akisikia wimbo fulani unaanza kusema "Aah! wimbo wangu huo!"
2.KUIMARISHA UMAKINI
Ukiwa ni msikilizaji mzuri wa nyimbo mara nyingi unatengeneza tabia ya kusikiliza wimbo kuanzia mashairi hadi midundo yake na hii si kazi rahisi hata kidogo kwani unatakiwa umakini wa hali ya juu kufanya jambo hili.
Cha ajabu utamkuta mtu anaupenda wimbo lakini hajui hata mashairi yanazungumzia nini,
tabia itakufanya hata uwezo wako wa kusikiliza mtu anapoongea uwe mdogo kwani kitendo cha kusikiliza na kutafsiri papo kwa papo kina umuhimu sana katika ulimwengu wa kujifunza.
3.HULETA HISIA ZA UTULIVU
Muziki sio lazima uwe na midundo,
lakini hata mashairi tupu yanaweza kukuletea utulivu unaoufanya ubongo upumzike vizuri.
Na ndio maana unapomuimbia mtoto mdogo hachelewi kulala.
Na watu wazima mara nyingi husinzia na kupumzika haraka wanaposiliza nyimbo za taratibu kwani ndizo ambazo zinaupa ubongo hisia nzuri kwa muda huo.
4.HUONGEZA NGUVU WAKATI WA SHUGHULI
Mathalani unapokuwa unafanya shughuli fulani ambayo ni kutumia nguvu nyingi muziki husaidia kuongeza utendaji kazi wako muda huo.
Na ndio maana hata washauri wa mazoezi wanapenda kuwaeleza wateja wao wanapofanya mazoezi ya kukimbia au yoyote ya kutumia viungo ni vyema wakaweka muziki ambao utakuwa unawasindikiza ili wasichoke haraka.
5.UNAONGEZA MANENO
Hata kama wewe ni mtumiaji mzuri wa lugha yako lakini kuna maneno unaweza ukawa hujawahi hata kuyatumia katika maisha yako.
Sasa unapokuwa msikilizaji mzuri wa mashairi ya nyimboi inakusaidia kuongeza maneno na maana zake.
6.CHANGAMOTO ZA UWEZO WA KUHOJI
Muziki mara zote kama unausikiliza kwa makini unakuletea changamoto za kujiuliza kama kinachoimbwa ni sawa au sio sawa.
Na kitu pekee kitakachokupa uwezo wa kutambua hilo ni uwezo wako wa kuhoji mashairi kutokana na tafsiri yako uliyopata.
Na ndio maana sitashangaa kumkuta mtu anaimba mashairi ya lugha yake lakini hajui hata aliyeimba alikuwa ana maanisha nini.
7.KUTIA HAMASA
Mara kwa mara si kitu cha ajabu kukuta unasikiliza wimbo ambao mashairi yake yanakugusa moja kwa moja,
na bahati nzuri anatoa na suluhisho la tatizo humo humo.
Na hali hiyo itakufanya ujione hauko peke yako mwenye hisia kama hizo hivyo kukutia hamasa ya kusonga kusonga mbele.
Na ndio maana kuna nyimbo kuzisahau kwako inakuwa ni ndoto kwani katika kipindi fulani cha maisha yako ulikugusa kiukweli.
8.HUONGEZA UBUNIFU
Muziki wenyewe tu ni kazi ya ubunifu kuanzia melodi ya mashairi hadi midundo yake.
Japo si kila msikilizaji wa muziki anaweza kuja kuwa msanii lakini utafiti unaonyesha watu wengi waliokuja kuwa wasanii wa muziki walikuwa wasilikzaji wazuri wa muziki.
Hata watu wengine wanaofanya kazi nyingine za sanaa wanatumia muziki kama chombo moja wapo cha kuwaongezea ubunifu kwa mfano waandishi, wachoraji, wachezaji au wanaofanya kazi za kutumia umakini mkubwa wa ubongo.
9.HUBADILISHA HALI YA UBONGO
Muziki unaweza ukakusaidia kubadilisha hali unayojisikia iwe ya huzuni, mawazo, upweke, hofu au hata hasira.
Na ndio maana wataalamu wanashauri ikiwa uko na hali mojawapo nilizozitaja hapo juu uwe unatumia njia ya kuimba nyimbo unazozipenda kukurudisha katika hali yako ya kawaida.
10.HUONGEZA UFANISI WA KAZI
Haijalishi kazi gani unayofanya,
ukimya utakufanya akili yako ihamie kwingine ambako utaufanya ubongo upoteze umakini na shughuli unayofanya muda huo.
Ila kwa kutumia aina ya muziki unaoupenda utaifanya akili ijisikie vizuri na hata kuzuia kuchoka haraka.
NAJUA KUNA WATU SI WAPENZI WA KUSIKILIZA MUZIKI KABISA.
NA MAKALA HII HAIPO KWA AJILI YA KUKUSHAWISHI UANZE TABIA AMBAYO HUKUWAHI KUWA NAYO KABLA ILA IPO KWA AJILI YA WALE WAPENZI WA MUZIKI ILI WAUTUMIE MUZIKI HUO KATIKA KUBORESHA SHUGHULI ZAO.
HIVI, UNAYATAMBUA MAKOSA AMBAYO WENGI WETU TUNAYAFANYA TUNAPOTOKA MTOKO NA MTU WA JINSIA TOFAUTI SIKU ZA MWANZONI? SOMA UJIELIMISHE
Iwe ni mara yako ya kwanza,
au umezoea kutoka na mtu wa jinsia tofauti lazima kuna vitu uzingatie ili usiharibu ladha na maudhui ya mtoko wako.
Kwani ni ukweli ulio wazi kuwa mpaka umekubali kupata mtoko na mtu wa jinsia tofauti maana yake unafurahia uwepo
wake karibu yako.
Na pengine ushaanza fikiria mipango ya baadaye ukiwa naye.
Lakini kuna makosa ambayo tunayafanya wengi wetu siku ya kwanza unapotoka na mtu wa jinsia tofauti.
Pitia vipengele vifuatavyo ugundue unafanya wapi makosa na uyaepuke.
1.USIMZUNGUMZIE MTU WAKO ALIYEPITA
Hili ndio kosa kubwa la kwanza ambalo wengi wanalifanya wanapokuwa katika mtoko na mtu mwengine wa jinsia tofauti.
Tambua wazi si kwamba utamuonyesha kuwa una hisia na watu unaowahi kuwa nao,
lakini ujue unamuudhi mtu uliyetoka naye.
Kuleta suala la mtu mwengine aliyepita wakati uko na mwengine halina maana yoyote kama umekosa la kuongea heri unyamaze hadi uulizwe.
2.USIZUNGUMZIE NGONO
Kabla hujajua kama unayetoka naye anapendelea mazungumzo ya aina gani,
usikurupuke kuzungumzia habari hizo kana kwamba wewe ni mtaalamu sana ukidhani utamvutie uliyetoka naye.
Kama uliyetoka naye ana malengo ya mbali utamfanya afikirie mara mbili kama utamfaa siku za mbele.
3.USIJIZUNGUMZIE WEWE KILA WAKATI
Kujizungumzia wewe kila wakati itamuonyesha uliyetoka naye kuwa una ubinafsi ndani yako.
Kila mtu angependa kupata nafasi ya kujielezea mbele ya mwenzake lakini kama wewe unamkatisha na kujizungumzia wewe tu utamtisha.
Ukionyesha unampa nafasi ya kumsikiliza anachoongea yeye utamfanya aone wewe ni msikivu.
Na ukiwa msikivu kwa mwenzako utapata nafasi ya kumtambua uliyetoka naye anapendelea mazungumzo ya aina gani.
4.IJUE HISTORIA YAKE
Tafuta taarifa za mtu unayetaka kutoka naye kabla haujafanya hivyo,
kwasababu wengine wana tabia ya kurudia matukio mabaya waliyoyafanya siku za nyuma.
Ukijichanganya kutoka na mtu bila kujua ana tabia gani anapofanya mtoko na mtu wa jinsia tofauti usije ukakumbana na balaa.
Wengi walipatwa na mabaya kwa kutojua historia ya wanaotoka nao na baadaye kujutia.
5.USITUMIE LUGHA CHAFU
Hata kama ni kawaida yako kuzungumza kwa
lugha chafu,
unapotoka na mtu kwa mara ya kwanza jitahidi kuficha mizuka yako.
Kutumia lugha chafu kwa kudhani utamuonyesha uliyetoka naye kuwa unajiamini na umuogopi ni kujiongopea.
6.KUVAA HOVYO
Tabia ya kumchukulia poa unayetoka naye na kuvaa hovyo ili ujionyeshe kuwa unaamua unalotaka,
unaharibu taswira yako kwake.
Kwani wengi huona kama umeshindwa kumuonyesha kumuheshimu siku ya kwanza au kabla hamjawa pamoja inawezekana ukamuonyesha dharau zaidi utakapokuwa naye.
7.USIBEBE ZAWADI ZA GHARAMA
Kumbuka huo ni mtoko tu na sio sherehe.
Unapobeba zawadi za gharama kubwa kwa mwenzako si kwamba utamfurahisha lakini ndani yake utamfanya akuone kuwa upendo wako pia unajengwa zaidi na vitu vya gharama.
8.USISHAMBULIE WENGINE
Ukiwa umetoka na mtu usianze kumzungumzia vibaya mtu au watu wengine,
kwani utamuonyesha wazi kuwa ipo siku na yeye itakuwa zamu yake.
9.USINYWE MPAKA UKALEWA
Hata kama ulikuwa na kiu kubwa ya kunywa pombe angalia usivuke kiwango mpaka ukalewa na usijielewe.
Tabia hii itamuonyesha ishara mbaya juu yako.
UFANYE MTOKO WAKO KUWA WA KAWAIDA,
MSAFI, KUFURAHISHA,
NA WAKUKUMBUKWA.
ANZA SASA KUWA MAKINI UNAPOKUWA UMETOKA NA MTU WA JINSIA TOFAUTI ILI USIHARIBU SIKU YAKO YA KWANZA YA MTOKO NA KUMPOTEZA MTU AMBAYE UNGETAMANI AWE KARIBU YAKO.
JE, UNAAMINIWA NA WATU WENGINE KATIKA JAMII YAKO? SOMA UJIELIMISHE FAIDA ZA KUWA MUAMINIFU KWA WATU.
Uaminifu ni kitu muhimu kitakacho waonyesha watu wewe ni nani,
na unafanya nini katika
jamii inayokuzunguka.
Jamii yoyote inapenda kuishi na mtu ambaye anaeleweka na hana tabia ya kuongopa ongopa kwa wengine.
Kama umetoa ahadi fulani halafu umeshindwa kuitimiza,
ni heri ukaongea ukweli kuliko kutunga uongo ili upate kuaminiwa na wengine.
Yawezekana kabisa kuna ukweli fulani hautaki ujulikane na wenzako,
ni heri ukakaa kimya kuliko kuongea jambo la uongo ili kuuficha ukweli.
Je, kila jambo linalonihusu wengine wanapaswa kulijua undani wake?
Hapana,
jambo lako liwe baya au zuri unapaswa wewe ndiye uamue kulisema au la,
lakini usitumie muda wako kusema uongo ili kulificha zaidi.
Na hapa ndio wengi wetu tunaingia katika mtego wa kuongopa kwa kujaribu kuuficha ukweli kupitia uongo.
Kama utaanza kuigiza hadi maisha ili tu uonekane mtu wa aina fulani na
siku watu wakija kugundua uaminifu wao kwako utaondoka kabisa.
Ukiona watu wako wa karibu wanasema hausomeki yaani ujue bado hawajajua msimamo wako katika maisha uko wapi na hivyo kukuamini ni nadra sana.
Hebu leo tuangalie faida za kuwa muaminifu:
1.UNAJITENGENEZEA THAMANI MBELE YA WENGINE
Wenzako watajua umesimamia upande gani na wao wasimame upande gani kwako.
Ukiwa muaminifu kwa wengine unajitengenezea mazingira ya kuthaminiwa.
Na wenzako watajisikia wako salama wao na mali zao wanapokuwa karibu na wewe.
Ukiwa muaminifu huitaji kujieleza mbele za wengine ukoje bali tabia yako itajionesha tu na wao watakuelewa vizuri tu.
2.UNAKUWA HURU
Unapokuwa msema kweli hauna muda wa kujilaumu wala kulaumiwa kutokana na utakachoongea.
Moyoni mwako utakuwa unajua wazi kuwa ulichofanya au kuongea ni kitu sahihi kwahiyo hofu haitakuwepo kamwe.
3.URAHISI WA MAISHA
Ukiwa muaminifu unajitengenezea maisha mepesi kwani watu wanaokuzunguka hawataona tabu kukukopesha au kukuachia vitu vyao vya thamani.
Hata unapotaka kuzungumza kitu mbele za watu hutakuwa na kazi ngumu ya kufikiria namna ya kuongopa,
itakuwa tu aidha ndio au hapana na maelezo yako mafupi yenye ukweli ndani yake.
4.UTAJENGA KUJIAMINI
Hutokuwa na muda wa kutafakari kama watu wanakupenda au wanakuchukia
kwasababu msema kweli siku zote hupendwa na wengi na hivyo utakuwa unajiamini mbele ya hiyo jamii yako,
japo kuna wachache watakuchukia lakini usiwajali.
5.WATU WATAKUJALI
Hakuna binadamu anayependa kujenga uaminifu na mtu asiye mkweli.
Na wengi watakuwa bega kwa bega na wewe pale wanapoona upo katika hali tofauti na walioizoea,
kwa kujitokeza na kukupa msaada wa karibu unaouhitaji.
KUISHI MAISHA YA KUTOAMINIWA NA WATU NI KUJITESA SANA,
UTAJIKUTA UNAKOSA FURSA ZA MAISHA KWA KUWA TU WATU HAWAKUAMINI.
HEBU TUANZE LEO KUONYESHA UAMINIFU KWA WATU WETU WA KARIBU WANAOTUZUNGUKA ILI KILA MMOJA APATE KUJUA THAMANI YAKE.
JE, UNAWEZA KUZUNGUMZA LUGHA NGAPI MPAKA SASA? UNAJUA FAIDA ZA KUFAHAMU LUGHA ZAIDI YA MOJA KATIKA MAISHA YAKO? SOMA UJIELIMISHE
Kujifunza lugha mpya sio kitu rahisi,
lakini
kuna faida nyingi sana kwa mtu anayefanikiwa kujifunza lugha zaidi ya moja.
Kila mtu anajifunza lugha fulani kwasababu zake tofauti na mwengine.
Kama unaenda mahali fulani halafu ukashindwa kuwasiliana na wenyeji,
hata kuishi kwako kutakuwa kugumu sana.
Unapochukua uamuzi wa kujifunza lugha
nyingi nyingi
kuna watu wasioelewa wataona kama
unajishaua hivi,
lakini
usijali kuonekana hivyo kwani faida zake utakuja kuziona wewe na sio wao.
Sidhani kama utafurahia,
endapo utakutana na mtu ambaye hamuelewani lugha hata kidogo,
na wewe unahitaji msaada kutoka kwake.
Katika mazingira haya utakuwa kama nguo ambayo inatembea bila mwili.
Lakini hapa tutaangalia faida tano za kujifunza lugha mpya.
1.KUZIFAHAMU TAMADUNI NYINGINE
Watu wanaofanikiwa kutambua tamaduni zaidi ya moja wanakuwa waelewa wa mambo mengi sana vichwani.
Kwani wanauwezo wa kwenda taifa lolote ambalo lugha yake wanaijua na kufahamu namna ya kuwasiliana na wenyeji katika kutambua utamaduni wao ukoje na kupata huduma muhimu kwa urahisi.
2.KUJUANA NA WATU WA MATAIFA MBALI MBALI
Watu wengi hupenda kukaa karibu,
na mtu mwenye uelewa wa mambo mengi kwani wanajua kuna kitu cha kujifunza
kutoka
kwa mtu huyo.
Wengi wanapenda kusikia taarifa mpya ambazo wao kabla hawakuweza kuwa nazo kutoka
katika mataifa mengine.
Na wanaposafiri nchi nyingine inakuwa rahisi kwao kuelewana na wenyeji na pia kupendwa kwani ataonekana ana taarifa mpya ambazo watu wengine wangependa kujifunza.
3.RAHISI KUWA MGUNDUZI WA VITU VIPYA
Utafanikiwa kugundua vitu vingi vipya katika nchi uliyotembelea na kuvileta katika nchi yako na kuwa mgunduzi wa
kwanza nchini kwako.
Kwani taarifa nyingi muhimu ambazo unapaswa uzifahamu zinakuwa katika lugha ya kigeni.
4.KUKUZA UWEZO WA KUELEWA NA KUMBUKUMBU
Unapojifunza vitu vipya unafungua nafasi kwa ubongo wako kuongeza uwezo wa kutafsiri mambo mapya na kuyashika kichwani.
Kwani zoezi la kujifunza lugha mpya linakutaka uwe na uwezo mkubwa wa kuhifadhi maneno hayo bila kusahau mapema na
hivyo kukujengea uwezo mkubwa wa kumbukumbu.
5.INAONGEZA FURAHA
Sababu mojawapo ya kujifunza lugha mpya ni kukuongezea furaha katika maisha.
Unapojua lugha nyingi unaongeza wigo wa wewe kuzifahamu taarifa nyingi
zitakazo kuongezea furaha katika maisha yako.
Unapojifunza lugha mpya kama haufurahii kuijua itakuwa ndoto.
*Sasa ushafahamu japo kwa ufupi faida za kujifunza lugha mpya,
itakuwa ni vyema kama utajitokeza na kwenda kujifunza lugha mpya.
Kujua lugha yako tu haitakufanya wewe uonekane ndio mzawa kuliko wengine,
lakini
kama unaangalia mbali,
utagundua mipaka ya mataifa imefunguka kila mahali.
Watu wa mataifa tofauti wanazidi kufahamiana.
Hali hii
huongeza fursa za kufanikiwa katika maisha.
KUJUA LUGHA MOJA TU,
SI KITU CHA KUJIVUNIA KATIKA MAISHA YETU.
KWANI
LEO TUPO HAPA NCHINI NA KESHO HUTUJUI TUTAANGUKIA ENEO GANI LA DUNIA HII AMBAYO MPAKA SASA IMEKUWA KAMA KIJIJI KIMOJA.
JE, UMEWAHI KUKATA TAMAA, AU UMEPANGA KUKATA TAMAA JUU YA JAMBO LINALOKUPA WAKATI MGUMU? SOMA UJIELIMISHE
Kama umeshindwa jambo
na unafikiria
kuwa upo mwisho wa safari yako
na huna sehemu nyingine ya kwenda,
tambua
unajidanganya nafsi yako.
Umejifunga jela mwenyewe
na mawazo yako ya
kujikatisha tamaa.
Kwa kufikiria hivyo
ni kujitengenezea nafasi ndogo ya kufanikiwa katika unalofanya,
na nafsi yako itaanza kuamini wewe ni
mtu wa kushindwa.
Tunaishi katika ulimwengu wenye njia nyingi za kufanikiwa katika
yale tunayojihusisha nayo.
Haya ndiyo unapaswa uyafikirie kabla ya kukata tamaa:
1.UMERIDHIKA NA KUSHINDWA?
Kushindwa si kuanguka chini;
ila ni kushindwa kunyanyuka wakati una nafasi ya kunyanyuka.
Mara nyingi ni lazima kushindwa mara nyingi ili ufanikiwe.
Na ndio maana unaposhindwa mara moja sio mwisho wa kila kitu.
Wazo lako lolote ambalo limeshindwa
kufanya kazi,
linafungua njia ya wazo litakaloshinda.
Ukishindwa na ukaanza kukubaliana na
hilo maana yake ni
kuridhika na kushindwa.
2.UMEJIFUNZA NINI LA MUHIMU?
Maisha siku zote yanatoa nafasi ya pili,
ili usahihishe makosa.
Lakini
nafasi hii ya pili haitakuwa na
maana yoyote kama hakuna ulilojifunza
katika kosa lililopita.
Unatakiwa ukubali udhaifu wako
lakini
kusanya nguvu kupitia hayo na ujifunze kitu ndani yake.
Unapofanya kosa
chukua nafasi ya kutafuta nafasi ya pili kusahihisha kosa hilo
na ukusanye uzoefu mpya.
3.WEWE NDIO WA KWANZA KUKUTANA NA MAGUMU?
Maisha huanza na maisha huisha,
kuna muda maisha yanacheka na maisha yanalia,
maisha yanakata tamaa na
maisha yanajaribu.
Maisha yana picha tofauti katika macho ya kila binadamu aliye juu ya ardhi.
Ukweli ni kuwa vile ulivyokuwa zamani,
ulivyo sasa na
yule utakayekuja kuwa ni
watu watatu tofauti.
4.MAUMIVU YAMEKUSAIDIA NINI?
Kuna muda lazima mambo yabadilike ili na
wewe ubadilike.
Lazima kuna muda upate maumivu ili ukue kiuzoefu.
Kuumia ni lazima ili upate hekima ambayo haukuwahi kuiwaza kama utaipata.
Lazima uumie moyo
ili uanze kuufuata moyo wako katika
maamuzi sahihi.
5.KUFANIKIWA NI KUWA NA NINI?
Usiruhusu mahangaiko yako ndio yakutambulishe kwa watu wewe ni nani.
Sio kila kitu unavyokitarajia kiwe kitakuwa hivyo hivyo ulivyodhani wewe.
Na ndio maana unapaswa kuacha kuishi matarajio,
ishi wakati ulionao na fuata mkondo na si kwenda kinyume na njia ya mkondo.
Jikumbushe kuwa ni ukamilifu kutokuwa mkamilifu.
Mafanikio si kitu unachopata,
ila ni uwezo wako wa kufanyia kazi uliyojifunza na kuyatumia kwa ufanisi katika uhalisia wa maisha yako.
6.KUNA NJIA NYINGINE YOYOTE?
Tofauti ya njia nyembamba na ndogo inajengwa na mtazamo wako.
Na hapo ndio unapaswa ujue kuwa ili kubadilisha kitu ni lazima ubadilishe
mtazamo wako.
Kutoweza kuona njia mbadala
katika maisha yako inatokana na
mtazamo wako
kujifungia eneo moja la maisha.
7.KUNA JAMBO LINAWEZA KUFANIKIWA BILA KIKWAZO?
Hata kama haupo
sehemu ambayo ulitamani kuwa haimaanishi kuwa hautakuwa siku moja.
Kufanikiwa kunaambatana na kujitambua ambapo kutakusaidia kupambana
mpaka mwisho.
Mafanikio bila ya vikwazo vitakufanya usione thamani yake
na unaweza kuyatumia vibaya.
Ukuta uliokutenga na ndoto yako unakusaidia kufahamu ni jinsi gani utajitoa kufikia unalotamani kwa kuuvunja.
8.ZURI NI HILO TU?
Unaweza ukawa umekutana na mabaya wakati unatafuta mazuri fulani,
lakini
haimaanishi hayo mazuri uliyoyakosa ndio pekee yaliyopo duniani.
Maisha yana mambo mengi mazuri na
si yale tunayodhani sisi
kuwa ni mazuri na kuyaona mengine kuwa mabaya kwa kuwa ndivyo tunavyodhani.
KUKATA TAMAA KATIKA MAISHA,
SI KITU
CHA KUKIFIKIRIA KWANZA PALE UNAPOKUMBANA
NA MAGUMU.
HAKUNA UTAKALOPANGA KULIPATA,
UKALIPATA KIRAHISI RAHISI KAMA WENGI WETU TUNAVYOTAMANI IWE.
TUMIA MASWALI HAYO HAPO JUU,
KUJIULIZA PALE UNAPOKUMBANA
NA WAKATI MGUMU ILI USIKATE TAMAA.
Subscribe to:
Posts (Atom)