Mwaka 2000 mwezi wa tisa nchi wanachama wa umoja wa mataifa zipatazo 189 zilikutana na kuasisi mpango wa maendeleo wa milenia ulioitwa Millenium Development Goals(MDGs) kwa lugha ya kiingereza.
Nchi hizi wanachama ulizitaka nchi zilizoendelea na zinazoendelea kushirikiana kwa pamoja ili kupunguza Umasikini, Njaa, Magonjwa, Vifo kwa akina mama na watoto, Fursa sawa kwa wanawake na Afya bora ya mazingira.
Nchi wanachama zilianza kuchukua takwimu za mwaka 1990 mpaka 2015 ambapo ndio lengo linapaswa kuwa limeshafikiwa na nchi wanachama.
Moja ya nchi wanachama ni Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo ili kufikia lengo hilo iliandaa mikakati pande zote mbili za muungano(Tanzania bara na Zanzibar).
Tanzania bara ilianzisha MKUKUTA(Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania) na Zanzibar ukaanzishwa MKUZA(Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini Zanzibar).

Intaneti bila waya, ni teknolojia ambayo huwezesha kuunda mtandao wa kompyuta(Laptops) au vifaa vyenye uwezo kupokea mawimbi ya intaneti(iPhone, iPads) viwili au zaidi viweze kuwasiliana bila ya kuwa vimeunganishwa kwa kutumia waya wenye mawimbi ya Intaneti.
Teknolojia hii maarufu kama WLAN(Wireless Local Area Network) hutumika zaidi nyumbani, kampuni za mawasiliano, vyuoni, maktaba na hata maeneo ya kibiashara kwa kutumia kifaa maalumu kinachoitwa Router kwa lugha ya kiingereza ambacho pia ufahamika kama Access Point.
Router(Access Point) huwa imeunganishwa kwa waya ambao una mawimbi ya intaneti na yenyewe huyasambaza mawimbi hayo hewani na pia huweza kupokea mawimbi ya nje ili kuwezesha vifaa ambavyo havijaungwa kwa waya viwe sehemu ya mtandao na kuwasiliana kwa pamoja katika eneo lisilozidi umbali maalumu ambao Router(Access Point) ina uwezo wa kusambaza mawimbi yake.
Ili kifaa hicho iwe kompyuta au simu iweze kupokea mawimbi hayo ya intaneti bila waya ni lazima iwe imetengenezwa na uwezo huo na hubandikwa lebo ya Wi-Fi(Wireless Fidelity) au IEEE802.11a,b,g, au n kutoka kwa watengenezaji.
Maeneo mengi ya kibiashara siku hizi mfano restauranti, hoteli na maeneo mengine ya burudani hutoa huduma hii bure kwa wateja wake wanapoenda kupata huduma za chakula na malazi.
Ukiwa maeneo haya ya biashara yenye huduma hii kama una kifaa chenye uwezo huo usisite kuunganisha intaneti na kama imewekwa alama za siri(Password) usiogope kuulizia na utapatiwa ili utumie.
Teknolojia hii hupunguza gharama kubwa za kununua waya kwa ofisi au nyumba ambazo hupenda kuunganisha watumiaji wa intaneti mfano mnaweza kuwa na Router au MoDem moja ikaweza kuhudumia watu wengi kwa wakati mmoja.
Asanteni hii ni taarifa ya teknolojia kwa leo.


 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz