Kuacha kutazama picha za ngono kunahitaji nidhamu, 
ujasiri na imani ndani yake.
Kwani bado madhara yake huwa hayaonekani mbele ya macho ya mtumiaji.
Je, kuangalia picha za ngono kuna madhara gani?

1.MAHUSIANO:

Si tu katika mahusiano yako na mchumba wako bali hata kwa marafiki,
 familia, wanafunzi wenzako, na hata wafanyakazi wenzako.
Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha wazi kuwa watu wanaoangalia picha za ngono,
 wana msongo mkubwa wa mawazo na kujihisi wapweke kuliko wasioangalia.

2.UBONGO:

Sehemu ya ubongo inaathirika na mihemko bandia inayotengenezwa  na anayeangalia,
 na hivyo kusababisha unalemaa na kushindwa kabisa kujibu mihemko halisi.
Picha hizi zitakufanya ujitenge na jamii yako, kwani kila muda utataka uwe peke, 
yako eneo unalokaa ili upate wasaa wa kuangalia vizuri kwa kujinafasi.
Maisha yanakosa shauku ikiwa ubongo utazoeshwa kujibu mihemko ya bandia
 kwa kiwango cha juu.

3.KUFURAHIA MATUKIO:

Unaweza ukajikuta kila kitu kwako kinachukiza kuangalia au kujihusisha nacho,
hata ukiangalia kitu kingine utaona bora kiishe ili uangalie picha zako.
Na hii ni hatari kubwa sana kwani utaufanya ubongo ukose taarifa za ziada na zile za ngono ndio zitatawala.

Fuata hatua zifuatazo kujiachisha na tabia hii:

1.AMUA KUACHA LEO USISEME KESHO:

Mara kwa mara watu ambao wamebobea katika uangaliaji wa picha hizi,
 wanapomaliza kuangalia hujipa ahadi kwamba kesho tu nitaacha kuangalia.
Baadaye wanajikuta kesho haifiki,
 kwani kila siku ina kesho yake.
Ukitaka kweli kuacha amua muda uliopo sasa usipange kesho ambayo hujaifikia.

2.USIKAE KARIBU NA MAZINGIRA YA PICHA HIZO:

Ukitaka kujisaidia kuondokana na tatizo hili, hakikisha una kaa mazingira
 ambayo hayajatawaliwa 
na picha za ngono.
Kama unatumia kompyuta, simu au 
hata iPad ambayo 
ndani yake umehifadhi picha hizo zifute sasa,
na ikiwa unatumuia 
DVD au CD ziharibu usikae nazo ndani,
 na hata katika 
historia ya anwani ya 
mitandao uliyotembelea,
 kama zipo zifute kabisa kwani ukiziona utarudi kule kule.

3.USIHESABU SIKU AMBAZO HUJAANGALIA:

Mara nyingi kama umebobea kuangalia huwa haipiti siku bila 
kutupia jicho picha hizo.
Na kuna muda mwingine unabanwa na shughuli nyingi kukupelekea 
kufikisha siku kadhaa hujaangalia,
sasa usikae chini kuanza 
kuhesabu siku ambazo hujaangalia utajikuta unajipa kibali cha 
kutaka kuziangalia haraka iwezekanavyo.

4.USIKAE MAZINGIRA YA PEKE YAKO:

Mara nyingi kama uliwahi kuangalia picha za ngono na ukajikuta uko 
mazingira ya peke yako,
 ya ama unaangalia tamthilia au 
kusoma kitabu chochote kitakachokuwa na habari ya masuala ya watu 
kujamiana itakukumbusha kamchezo kako.
Usichague pia kuangalia
 peke yako picha ziliwekwa
 alama ya miaka 18 zitakuchochea urudi ulipotoka.

5.EPUKA MAZUNGUMZO MACHAFU NA MARAFIKI:

Mara nyingi tunapokaa na marafiki zako ambao wanapenda kuhadithia 
masuala ya ngono tu watakuchochea.
Maana kuna wengine ni mafundi wa kuhadithia hizo vitu,
 kana kwamba wao ndiyo watengenezaji,
sasa unapoona wanaanzisha hizo habari kama huwezi kuwasimamisha basi ni heri ujitenge nao.

6.EPUKA HISIA CHOCHEZI ZA NDANI:

Siri kubwa katika hizi picha zinampa hisia nzuri mtazamaji,
 na kuona hakuna chenye thamani yoyote muda huo.
Kwa hiyo epuka hisia za hasira, 
upweke, na huzuni kwani 
zitakufanya uone eneo pekee la kwenda kujipumzisha ni kuangalia picha hizo.

7.FUTA FIKRA POTOFU:

Achana na fikra potofu za mtaani kuwa kuangalia picha za
 ngono ni kujifurahisha nafsi na hazina madhara.
Lakini kiuhalisia madhara yanayoambatana na tukio lake utayaona baadaye.
Kuna wengine watakwambia kuwa usipoangalia hizo picha utakuwa mshamba na hauendi na wakati.

8.USIJISEMESHE KUWA HUWEZI KUACHA:

Unapokuwa unaangalia hizi picha mara nyingi akili yako inajizoesha,
 na kuona ni utaratibu 
wake wa kila siku.
Kwa hiyo moyoni utakuwa unajisemesha kuwa kuacha kitendo hiki 
hautaweza kamwe,
kitu ambacho kitakufanya uwe dhaifu wa kujitawala.

9.ACHA KUJIKUMBUSHA PICHA ULIZOANGALIA:

Mara nyingi unapokuwa mazingira fulani ya kuwaza mambo mbali mbali, 
mawazo ya picha ulizoangalia ukiyatanguliza kwanza utajifanya 
uwe na shauku ya kwenda kuangalia upya.
ukiona kuna kazi unafanya kazi
 katika kompyuta au umeshika kifaa chochote chenye uwezo wa kukuonesha 
picha hizo ni heri ukizime 
kwa muda huo halafu fikiria kitu kingine kwa haraka.

LINAPOKUJA SUALA LA KUACHA TABIA,
 HII NI VYEMA UKAFIKIRIA ZAIDI KAMA KUNA FAIDA YOYOTE UNAYOPATA.
 NA JE KUNA SIKU UTAKAYOKAA CHINI KUJIVUNIA ULICHOPATA KWA KUANGALIA HIZI PICHA? 

CHUKUA LEO HATUA YA KUACHA ILI KUEPUKA MADHARA YATAKAYOKUJA KUTOKEA SIKU ZIJAZO.


WEKA NIA, UNAWEZA.



Kitu pekee duniani, ni kuwa kila binadamu amepewa uwezo wa kufanya kitu cha pekee ndani yake,
 lakini hautaambiwa unaweza kufanya nini mpaka wewe mwenyewe utafute.

Hautakuja kujua wewe ni 
mzuri kwenye kitu gani kama huna tabia ya kujaribu vitu tofauti tofauti.

Ukichukua hatua ya kutafuta wewe unaweza kufanya kitu gani kwa ufanisi utajishangaa mwenyewe,
kwani utajikuta unaweza kufanya vitu ambavyo mwanzo ulikuwa unaona haiwezekani kwako.

Yawezekana kabisa kuna kitu huwa unatamani kufanya na unadhani hautaweza,
ukweli ni kuwa hautajua kama huwezi au unaweza mpaka ujaribu.
Watu wote waliofanikiwa katika maisha yao nao pia hawakuwa na uhakika kama wanachofanya watakiweza,
lakini kwa kujaribu wakajikuta wanaweza na kufurahia.

Unapofanikiwa kutambua kipaji chako ni nini,
ndio muda utakaoona utamu wa maisha yako ulipo, 
kwani utafunguka macho na kuanza kuiona dunia katika mtazamo tofauti
 na uliokuwa nao mwanzo.
Na hii inatokana na siku zote kitu unachoweza kukifanya vizuri ndio kitakuwa kinabeba furaha yako ya kila siku.

Sasa jaribu kufuata hizi hatua  uone jinsi gani zitakusaidia kutambua kipaji chako:

1.CHUNGUZA UNAFURAHI SANA UKIFANYA NINI:

Sehemu nzuri ya kuanza kujitafuta ni kutafakari wewe mwenyewe kitu gani ukifanya unafurahia sana
 huwa unaomba muda usiishe.
Lakini angalizo;
   kiwe kinakubalika na jamii.
Kama unapenda kitu fulani sana acha kung'ang'ania kuwa shabiki,
 hebu anza na wewe kufanya uone kitatokea nini.
Ushahidi upo wa watu wengi waliokuwa mashabiki wa muziki, 
maigizo, na hata mpira walipoamua kujitoa katika ushabiki 
walikuja kuwa na mafanikio makubwa kupitia fani hizo.

2.JIFUNZE KITU KIPYA:

Hata kama kwa sasa kuna kitu unajishughulisha nacho,
jaribu kufanya na shughuli nyingine ambayo utapata changamoto mpya na kuongeza ujuzi mwengine.
Hakuna ambaye anapenda afanye kitu katika mazingira magumu,
ukitoka katika mazingira hayo kutafuta mapya utaona mabadiliko yako.
Hautaweza kugundua kipaji chako kama utaendelea kun'gang'ania mazingira magumu na kuogopa kujaribu kitu kipya.

3.TEMBELEA MAENEO MAPYA:

Yawezekana maeneo unayoishi shughuli fulani ndio maarufu sana,
 na wewe unajihusisha nayo kwa kuwa hakuna nyingine ya kufanya.
Kwahiyo unapoenda mazingira mapya utafanya akili yako ifunguke kuona fursa ya kujifunza vitu vipya.

4.SOMA HABARI MBALI MBALI:

Kusoma habari mbali mbali ziwe za mtu au mazingira fulani,
 zitakufanya kupata uzoefu wa kutambua vitu vipya.
 Vitu hivyo ambavyo mwanzo hukuwa na uelewa navyo.
Tabia hii itakujengea hamu ya kutaka kufahamu vitu zaidi,
 na hivyo itakupunguzia uoga wa kujaribu mambo mapya.
Hasa hapa www.lishaubongo.blogspot.com lazima utabadilika mtazamo na utajitambua.

5.HUDHURIA SEMINA FUPI FUPI:

Ukiwa una tabia ya kuhudhuria semina 
utakuwa unafungua ubongo wako 
kulishwa mambo mapya na kukujengea mazingira ya kujitambua.
Usiogope kuingia gharama kulipia semina 
ambayo inaweza kukusaidia wewe 
kuja kuishi maisha ya furaha siku zote.

6.ULIZA MARAFIKI:

Mara nyingi mwenye kipaji ni ngumu kukitambua yeye mwenyewe,
 kwa kuwa siku zote yeye anaona anafanya kitu cha kawaida.
 Lakini watu wa pembeni ndio wanaochizika na kile anachofanya.
Kama una marafiki ambao mna upendo kwa kila mmoja hawatokuficha kipi wanakifurahia kwako unapokifanya.
Shikiria hapo sasa.

7.CHAGUA MTU WAKO WA MFANO:

Katika maisha kama wewe unapenda kitu fulani kinachofanywa na binadamu,
 lazima kuna mtu mmoja ambaye anapofanya hicho kitu wewe anakufurahishwa sana,
 na unatamani kuwa kama yeye.
Angalizo, 
siyo lazima uje kufanya anachofanya yeye lakini unaweza ukachukua 
ari yake na juhudi ya ufanyaji ukawekeza katika shughuli unayopenda wewe.

9.JIUNGE KATIKA VIKUNDI:

Kuna vikundi mbali mbali vya vijana vinajishulisha na 
shughuli tofauti tofauti unaweza ukajiingiza huko na kujifunza 
vitu usivyoweza.

10.TAFAKARI KILA UNACHOANGALIA NA KUSIKIA:

Wengi wetu tumekuwa mashabiki wa filamu, muziki au hata habari za uchunguzi katika televisheni na redio.
Lakini si kila unachosikia na kuangalia hakuna cha kujifunza,
naamini mpaka umepata nafasi ya kusikiliza na kuona basi ujue kuna kitu 
unatakiwa ujifunze.
Usikubali kuendelea kuishi na taarifa zile zile kila siku,
anza kujifunza mpya sasa.


NAJUA KUNA WENGI WETU TUNASEMA HATUNA KIPAJI CHOCHOTE,
LAKINI AMINI LEO KWAMBA HAKUNA AMBAYE HAJAUMBWA NA KITU CHA PEKEE CHA KUMFANYA AYAFURAHIE MAISHA YAKE.
  
HUJACHELEWA ANZA SASA KUJICHUNGUZA NA FANYIA KAZI UTAONA UPANDE SAHIHI WA MAISHA YAKO.


26.JIAMINI KUWA UNAWEZA:

Ukitaka kuwa mjasiliamali 
ni lazima ujiamini wewe 
mwenyewe kuwa unaweza kufanikisha unachotaka kufanya.
Wewe ukijiamini na hata
 ukaweza kusimama mbele
 za watu kuwaeleza kuwa unaweza hata wao watakuamini.

27.SOMA SANA:

Mjasiliamali mzuri ni yule
 anayewekeza muda wake 
katika kutanua uwezo 
wake wa kuelewa mambo.
Kwa njia ya kusoma kila kinachohusu mambo anayoshughulika nayo, 
ndipo anapoongeza ujuzi wa biashara yake na ubunifu.
Hakuna njia itakayokupa
 maarifa makubwa kama
 kujisomea mwenyewe maandiko mbali mbali na si lazima uwe darasani.

28.KUWA JASIRI:

Mjasiliamali wa ukweli huwa ni
 jasiri na yuko tayari kulinda analoliamini ni sahihi kwa 
gharama yoyote.
Yawezekana kuna watu wakataka kubadilisha wazo lako kwa kuwa tu 
wao wanaona halifai,
unapaswa  utoe msimamo wako wa dhahiri mbele yao.

29.IFAHAMU VIZURI BIASHARA YAKO:

Unaweza ukajitolea kufanya kazi bure kwa mtu anayefanya shughuli 
unayopenda kuja kufanya ili kuijua nje na ndani ikoje na 
changamoto zake.
Ukishapata uzoefu kwa kipindi fulani ndio unaweza kutoka na kwenda
 kuanza harakati zako,
na sio kuvamia biashara usiyojua changamoto zake.

30.JITOKEZE:

Kama unataka kuwa mjasiliamali
 ni vyema ukaondoa aibu 
ya kushindwa kusimama mbele za watu wakuone na wakufahamu.

31.CHOCHEA WAZO LAKO:

Jipe mwenyewe mizuka ya 
ndani kuwa hili wazo ni zuri na utafanikiwa kupitia hilo pasipo 
kusubiri maoni ya nje.
Unaweza ukatenga muda 
wako wa kukaa kila siku na kulipalilia wazo lako ndani kwa ndani 
huku ukifikiria zaidi kuwa litafanikiwa.

32.ANZA LEO:

Ni uchizi kukaa chini na 
kusema siku zijazo nitaanza ujasiliamali,
unapaswa utambue kama
 kweli uko ndani yako 
hauhitaji kusubiri kesho ndio uanze, anza leo harakati zako.

33.FANYA UTAFITI WA KINA:

Chunguza soko lako kwa 
makini huku ukiangalia vitu kama mshindani wako ni nani,
na utawezaje kujitofautisha 
naye katika bidhaa au huduma anayotoa.

34.TAMBUA UNACHOWEZA NA USICHOWEZA:

Ukitaka kuwa mjasiliamali 
mzuri ni lazima ujue maeneo gani wewe sio mzuri na maeneo 
gani wewe ni mzuri.
Tumia muda mwingi kufikiria
 zaidi kuboresha maeneo
 ambayo wewe ni mzuri, 
achana na kule ambako uwezo wako ni mdogo patakupotezea muda.

35.KUWA NA NJAA:

Unatakiwa uwe na njaa ya 
kweli kabisa ya kutaka 
kula unachofikiria unastahili kula.
Kama hutokua na njaa y
a kweli ukikutana na 
changamoto utajikuta unarudi nyuma kwa kukosa uvumilivu.

36.TAFUTA WASHIRIKA:

Ukiwa mjasiliamali ni 
lazima utafute watu wa kushirikiana nao ambao unaamini wana
 mtazamo na ari kama yako kibiashara.

37.TENGENEZA WAZO RAHISI KUELEWEKA:

Ikiwa jina la biashara yako ni 
gumu na linampa wakati mgumu 
mteja kuioanisha na bidhaa au huduma unayotoa utapata tabu katika soko.
Hakikisha mteja anapoona 
jina la biashara yako awe 
anapata picha halisi ya nini kinachoendelea katika kampuni yako.

38.ZIJUE FAIDA NA HASARA ZA SOKO:

Unpotaka kufanya ujasiliamali 
ni lazima uangalie kwa
 makini faida na hasara za soko unalotaka kulihudumia.

39.KUWA RAFIKI KWA WATU:

Mjasiliamali wa kweli ni 
lazima anakuwa karibu na watu ambao anawahudumia,
wateja wanapoona mtoa 
huduma yuko karibu nao wanajenga moyo wa kumuamini na kumpenda.

40.TUNZA PESA:

Kama unataka kuwa mjasiliamali 
anza leo kujua namna ya
 kutunza kile kidogo unachopata,
kama unafanya kazi mahali
 jiwekee utaratibu wa 
kuweka kando sehemu ya mshahara wako ili uje uwekeze.

41.FANYA KAZI NA MTU MWENYE UJUZI TOFAUTI:

Kama wewe una ujuzi wa 
aina fulani usitafute mtu 
mwenye ujuzi huo huo mfanye kazi moja, tafuta mtu ambaye unaona
 mmetofautiana ujuzi lakini wote mnataka kuhudumia soko moja.

42.THAMINI WAZO LAKO:

Kuna watu wakati unaelezea wazo lako wanaweza wakakueleza kuwa 
hauna jipya na kwamba wazo kama hilo lako tayari lipo.
Lakini wewe pambana kwasasbabu hata kama mwengine anafanya 
hatoweza kufanya kama
 wewe utakavyofanya,
unachotakiwa wewe ni kujitofautisha tu.

43.UVUMILIVU:

Kuwa mjasiliamali unataka uwe na uvumilivu wa hali ya juu, kwani si 
kila siku utakuwa 
katika hali hiyo hiyo.
Kuna kipindi utakataliwa na wateja wako na uspokuwa mvumilivu
 unaweza ukaacha unachofanya.

44.UNDA TIMU YA UHAKIKA:

Ukiwa na timu ya uhakika ya 
watu wachapakazi na 
wenye mtazamo kama wako,
ukirogwa kumuingiza kundini mtu mwenye mtazamo tofauti na wewe 
mtasumbuana na anaweza kupoteza ari ya kundi kufanya kazi.

45.USIRIDHIKE:

Ukitaka kuwa mjasiliamali,
 ni lazima uwe na moyo wa kuona hauridhishwi na hali iliyopo,
na kwamba unataka kufanya kitu ili ufanye mabadiliko.

ANZA SASA KUFANYIA KAZI WAZO LAKO LA UJASILIAMALI NA UTAONA MAFANIKIO YAKE.



 
Copyright 2013-2017 Lisha Ubongo
| Branded by www.pixelbase.co.tz