JE, KUNA VITU ULITAMANI KUWA NAVYO LAKINI MPAKA LEO HAUJAWEZA KUWA NAVYO? SOMA HAPA UZIJUE HATUA ZA KUCHUKUA ILI UBADILISHE HALI YAKO.
Katika maisha kuna mambo mengi sana ambayo unayatamani,
na kila siku unaomba
yawe mikononi mwako.
Tangu ulipoanza kuyatamani ulikuwa na mipango,
mawazo na mikakati mingi
sana kichwani,
lakini mpaka leo haujafanikiwa
kuwa nacho.
Na yawezekana unajiuliza kila siku na jibu mpaka leo haujapata.
Sasa hebu leo chukua hizi hatua nane halafu anza kuzifanyia kazi:
1.ANZA KUKAA NA WATU SAHIHI
Hawa ni watu ambao wewe unapokuwa nao unafurahia,
wanaokupenda, kukuthamini, na
wanaokutia moyo wa kutokata tamaa katika mambo yako.
Hawa ni wale watu ambao ukikaa nao wanakufanya ujihisi uko hai,
ambao wanaokukumbatia wewe wa sasa hivi na wanaotamani kumkumbatia yule unayetamani kuwa,
bila masharti yoyote.
2.ANZA KUWA MUAMINIFU KWA NAFSI YAKO
Kuwa muaminifu kwa jambo lipi ni sahihi kwako,
na lipi linahitaji
kubadilishwa.
Kuwa muaminifu kwa lipi unataka
kufanikisha na nani
unataka kuwa.
Ukianza kujidanganya nafsi yako mwenyewe utakuwa unakosa fursa
za kujitambua
kama unachotamani ni sahihi kwako.
3.ANZA KUTENGENEZA VIPAUMBELE VYA FURAHA YAKO
Mahitaji yako yana umuhimu sana.
Kama usipoanza kuweka vipaumbele vya vitu gani hasa vinakupa furaha,
hautaweza kujitambua
wewe ni nani.
Kama utaweza kutambua wewe
unafurahia nini itakuwa
rahisi kuwafurahisha na watu
wako wa karibu.
4.ANZA KUWEKA WAZI WAZO NA NDOTO ZAKO
Katika maisha,
kama unasubiri fursa zikufuate utangoja milele,
lakini kama ukiziuata fursa huko ziliko zitakupokea kwa
mikono miwili.
Haina maana kukaa chini na kujisifu kuwa una mawazo na ndoto nzuri,
kama haujaanza kuzitoa zionekane.
5.ANZA KUJIVUNIA ULIVYO
Kama haujaanza kujivunia vile ulivyo leo, itakuwa
ngumu kupiga hatua zako mwenyewe kuelekea mafanikio.
Ukianza kujivunia vile ulivyo
utafanya uyaone mawazo yako yana thamani, nguvu na uzuri ambao hakuna
mwengine yeyote anao.
6.ANZA KUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA
Kama uliwahi kukosea na ukapata funzo fulani anza kulithamini hilo funzo
kwa kuchukua mafundisho yake na
kuyafanyia kazi.
Na ukiweza kufanya hilo,
utaona kumbe kukosea ni hatua moja wapo katika kupata mafanikio.
Kwani kuna uwezekano mkubwa kabisa kama usipotaka kujifunza
kutokana na hilo basi
utakuwa unalikwepa daraja ambalo lingekuunganisha na mafanikio.
7.ANZA KUWA MKARIMU KWA NAFSI YAKO
Kama utaendelea kutumia muda mrefu katika kuilaumu nafsi yako,
na kutaka kujiadhibu utakuwa unaendelea kujirudisha nyuma.
Ukiwa mkarimu kwa nafsi yako utaona nafasi ya wewe kunyanyuka kila
unapokuwa umedondoka
bila kujikatisha tamaa.
8.ANZA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAKO
Matatizo yanayokukabili hayatoi tafsiri
ya wewe ni nani,
bali jinsi unavyoyakabili
na kuyamaliza ndiyo
tafsiri yako ilipo.
Matatizo hayawezi kuondoka mpaka wewe mwenyewe uyakabili.
Fanya jitihada zako zote pale unapoweza halafu jipongeze kwa
hatua uliyopiga.
TUANZE LEO KUCHUKUA HATUA HIZI NA YALE YOTE TUNAYOOTA YAWE YETU YATAKUWA
KWETU BILA UTATA.
JE, UNA WAZO LA KUTOA AU KUMSAIDIA MTU KUTOA MIMBA? SOMA HAPA UYAJUE MADHARA YAKE ILI UYAEPUKE MAPEMA KWAKO NA KWA MTU WAKO WA KARIBU.
Utoaji wa mimba(Abortion),
katika jamii yetu siku hizi limekuwa jambo la kawaida sana,
kiasi kwamba hakuna anayezungumzia madhara tena.
Na jamii inalichukulia kuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.
Tafsiri potofu inayotolewa na watu huko mtaani,
kwenda kwa wageni wa jambo hili ndio unalifanya liendelee kukithiri.
Mara nyingi,
wanaofanikiwa kutoa kwa usalama,
madhara wanakuja kukutana nayo siku za mbele sana na hapo ndio hawaoni tatizo katika kitendo hiki.
Lakini,
leo hapa tuzungumze na wale ambao,
hawajawahi na wanafikiria,
au wamewahi na kuna matatizo wanakutana nayo bila kujua chanzo ni nini,
au wanataka kumshawishi mtu akafanye.
hebu tuangalie matatizo ambayo anaweza kukutana nayo mtu anayefanya utoaji wa mimba:
1.KUTOBOKA KWA KIBOFU CHA MKOJO
Ikiwa,
mfuko wa uzazi utatobolewa,
kuna uwezekano mkubwa kabisa na kibofu chako cha mkojo kutobolewa.
Na inaleta maumivu makali sana na matibabu yake ni
mpaka oparesheni.
2.KUTOBOLEWA KWA UTUMBO MDOGO
Kama mfuko wa uzazi utatobolewa,
basi pia kuna uwezekano
mkubwa wa utumbo mdogo kutolewa kwa
urahisi kabisa.
Na dalili zitakazoonekana ni pamoja na kichefu chefu, kutapika, maumivu ya tumbo, homa, damu katika haja kubwa,
na hata kifo kama
isipogundulika mapema.
3.KANSA YA MATITI
Kwa wanawake wanaofanya utoaji wa mimba,
wako katika hatari kubwa
ya kupata kansa ya matiti
siku zijazo
za maisha yao.
4.MIMBA IJAYO KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI
Kwa wale ambao,
wanakuwa washafanya utoaji wa mimba
inakuwa ni rahisi kwa kukamata mimba zinazofuata zikiwa zimetungwa nje ya mfuko wa uzazi.
Na endapo hautagundulika mapema kwamba mimba imetunga nje ya mfuko wa uzazi,
utapoteza maisha
kwa kuvuja damu nyingi sana,
kwa kuwa mimba ya nje ya mfuko wa uzazi ina kawaida ya kupasuka.
Madhara mengine ambayo yanaweza kuja kutokea ikiwa utapata mimba nyingine:
*Kuna uwezekano mkubwa kabisa ukaendelea kupata siku zako kwa muda wa miezi mitatu ya mwanzo.
*Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa hautazaa kwa kutumia mfumo uliozoeleka.
*Mtoto atakaye zaliwa atakuwa katika hatari ya kupoteza maisha miezi ya mwanzoni kabisa.
*Mtoto ajaye anaweza kuwa na uzito mdogo kuliko kawaida.
*Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa mtoto ajaye atazaliwa kabla ya muda wake kufika.
5.KUPUNGUKIWA DAMU
Na hili huwa ni tatizo ambalo lina uwezekano mkubwa wa kutokea,
kwani unapoteza damu nyingi sana wakati wa zoezi hilo.
6.MIMBA KUHARIBIKA
Kwa wale ambao wamefanya utoaji wa mimba zaidi ya mara mbili,
wako katika hatari ya mimba zao kuwa zinatoka na kuharibika
kabla ya wakati.
7.VIPANDE VYA MWILI KUBAKIA
Kwa kuwa,
anayekutoa huwa haoni ndani kuna nini hasa kimebaki,
zaidi yeye anachojua ni kuingiza kifaa chake na kuanza kuvuta viungo vya kiumbe kimoja kimoja.
Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kabisa akashindwa kutoa vyote.
8.UTASA
Baaada ya kufanya zoezi hili,
unaweza usiwe na uwezo wa kupata
mimba tena.
9.KANSA YA SHINGO YA KIZAZI
Hapa hatari huwa kubwa,
kwasababu kuna uwezekano mkubwa wakati unafanyiwa shingo ya
kizazi ikakwanguliwa na hivyo kusababisha kansa siku
za baadaye.
10.MATATIZO YA SAIKOLOJIA
Mhusika wa utoaji mimba,
huwa anaweweseka sana pale anapokuwa amefanya tukio hilo kila
anapoenda kulala.
Japo kwa wale wazoefu hawajali lakini kwa wewe mgeni itakufanya ukose raha muda wote wa maisha yako.
NADHANI TUMEONA BAADHI YA MADHARA AMBAYO YANAWEZA KUMKUTA MUHUSIKA.
BASI TUJITAHIDI KUTUNZA UHAI WA VIUMBE HAO AMBAO HAWANA HATIA.
KWANI JANGA UNALOLIKIMBIA NI DOGO KULIKO UTAKALOLISABABISHA BAADA YA KUFANYA TUKIO HILI.
HIVI, UNAYAFAHAMU MAKOSA TUNAYOYAFANYA WAKATI WA KUCHAGUA NGUO ZA KUVAA? SOMA HAPA UYAFAHAMU ILI TUYAEPUKE
"Kuvaa na kupendeza, ni kipaji jamani!!"
Linapokuja,
suala la uvae nini ili upendeze
mara nyingi
linaumiza kichwa.
Na unapoangalia uvaaji wa kila mtu na anaonekanaje,
ndio unagundua kuvaa ni kipaji.
Kuna watu wao kila nguo wanayonunua inawapendeza.
Kwa wengine wakina sisi inakuwa ni kitendawili,
cha tuvae nini ili tupendeze.
Na kuna makosa makubwa ambayo tunayafanya wakati tunapoenda kuchagua nguo za kuvaa ni haya hapa:
1.KUNUNUA NGUO ISIYOTOSHA
Hapa unakuta unanunua nguo kubwa
au ndogo sana
kuliko mwili wako.
Nguo inapokuwa kubwa inakufanya uonekane imekuvaa,
na
inapokuwa ndogo sana
itaonekana imekuchora mwili wako na
kupendeza katika hali hiyo ni
nadra sana.
Ukiona unashindwa kabisa katika kuchagua, jenga urafiki na
fundi nguo tu.
2.KUVAA SHATI MIKONO MIFUPI NA TAI
Labda,
kama uwe unafanya kazi mgahawani,
kwahiyo
unaogopa mikono ya shati kuchafuka na vyakula vinavyomwagika mezani,
ndio uvae hivyo.
Ukiwa umevaa hivi katika mazingira mengine,
hakuna
atakayekuona umependeza.
3.KUVAA VIATU VICHAFU
Inawezekana kabisa,
ukavaa nguo zikakupendeza sana,
lakini
ukiharibu katika viatu utaonekana haujapendeza kabisa.
4.KUVAA MKANDA WA RANGI TOFAUTI
Ukikosea kuvaa mkanda,
ambao rangi yake haiendani na rangi ya nguo au viatu ulivyovaa
utachosha machoni pa watu.
5.KUFUNGA TAI NDEFU AU FUPI SANA
Ikiwa utavaa tai ambayo ni ndefu sana,
au fupi sana
utaharibu ladha ya muonekano wako.
We utakuta mtu amevaa tai kubwa
inapita hadi mkanda wa suruali au fupi sana inaishia kifuani tu,
kupendeza utaota milele.
6.KUVAA SOKSI NA VIATU VYA WAZI
Hapa bwana,
hata kama umevaa vipi huko juu
lakini
utaonekana kituko tu
katika hili.
7.KUVAA NGUO ZA RANGI ZINAZOPINGANA
Ni vizuri,
ukawa makini wakati wa
kuchagua nguo ya rangi gani
inaendana na rangi gani
sio ilimradi umevaa tu.
Na kuna muda mwengine hata ujaribu kujua rangi yako ya mwili pia
kama inaendana na rangi ya
nguo utakayovaa.
8.KUVAA NGUO ZILIZOJIKUNJA
Ni vyema,
ukazinyoosha nguo zako
kuliko
kuzivaa bila kuzinyoosha ni kujishusha muonekano wako.
Ni heri kama unajua hupendi kunyoosha basi usizitupe nguo hovyo,
tafuta kitu cha kutundikia ili isijikunje kama unajua utairudia.
9.KUVAA NGUO ZENYE RANGI NYINGI NYINGI
Wewe utakuta mtu unavaa nguo ina rangi nane tofauti tofauti
halafu eti unategemea kupendeza.
Lazima ujaribu
kuchagua nguo zenye
mchanganyiko mdogo wa rangi na
sio rangi nyingi nyingi.
10.KUVAA WIGI LA RANGI AU MTINDO USIOENDANA NA WEWE
Si kila wigi la nywele linafaa kuvaliwa na kila mtu,
kuna mawigi mengine rangi yake haiendani na wewe.
Hata kama ndio liko katika fasheni lakini usiharibu muonekano wako
kwa kuingia kichwa kichwa matika mtindo
usiokupendeza.
KILA MMOJA WETU ANAPENDA AONEKANE AMEPENDEZA,
HILO HALIPINGIKI.
NA INAWEZEKANA KABISA MAKOSA HAYA YA UVAAJI TUNAYAFANYA.
BASI TUJARIBU KUWA MAKINI TUNAPOCHAGUA NGUO ZA KUVAA.
ITAENDELEA....
HIVI, UNAZIFAHAMU TABIA ZINAZOKERA SANA KATIKA MTANDAO WA KIJAMII WA FACEBOOK? SOMA HAPA UJIELIMISHE ILI TUZIACHE KAMA TUNAHUSIKA.
Mtandao wa kijamii wa Facebook,
ndio umetokea kuwa mtandao wa kijamii wenye mashabiki wengi kuliko wowote uliowahi kuanzishwa.
Wewe uliyejiunga,
katika mtandao huu utajikuta unakutana na watu uliopotezana nao
miaka mingi iliyopita,
na wengine wapya ambao haungezani kama utawahi kuwasiliana nao.
Kati ya watu hawa utakao kutana nao wengine wanakuwa na tabia za ajabu mpaka muda mwengine wanaumiza kichwa.
Hebu soma hapa uzijue hizo tabia kama haujakumbwa na balaa hizo basi ujipange.
1.KUWEKA UJUMBE WA AINA MOJA MARA NYINGI KATIKA UKURASA WA MTU
Kitu chochote kinapozidi kiwango huwa kinachefua hata kuangalia,
hata kama unamjali mtu
huwezi kuweka ujumbe mmoja
mara kibao utakuwa unamfanya apoteze
ladha ya ujumbe.
We mtu anaposti"duh!"x10 hadi inachosha kusoma.
2.KU'LIKE' STATUS ZA HUZUNI
Yaani hata kama unashindwa kutofautisha habari za huzuni na furaha
basi fikiria kabla huja'like'.
We mtu amepost picha ya
marehemu ndugu au mzazi
halafu wewe una'like',
ni heri uandike kitu kuliko 'like'
3.KUPOSTI KILA DAKIKA KITU UNACHOFANYA
Utakuta mtu anapoamka asubuhi anaanza kuposti:
"Ndio naamka sasa wadau/marafiki"
baada ya muda kidogo;
"Napiga chai na chapati hapa karibuni waungwana"
tena;
"Nasubiria basi pande hizi kwa manyanya teja ana kelele huyo"
halafu;
"Dah! naingia ofisini hakuna hata mtu"
halafu;
"Natamani muda wa chakula ufike nina njaa kinoma"
Nadhani watu aina hii ushakutana nao sana tu na wanachosha kwa kweli.
4.KUWEKA VITU BINAFSI KATIKA UKURASA WAKE
Lazima,
utambue kuwa facebook ni mtandao wa kijamii kwa hiyo kila mtu
anayefungua ukurasa wako awe rafiki asiwe rafiki ataona tu.
Sasa wewe,
unaweka mapicha yako ya chumbani tena ukiwa umelala!!
jaribu kutofautisha vitu gani vya kushirikisha kila mtu na vitu gani unapaswa kushirikisha watu wako wachache.
5.KUWEKA LUGHA ZA MATUSI
Lazima utambue,
kuwa si kila mtu anapendelea kukutana na lugha za matusi juu
ya ukurasa wako.
Yawezekana unataka kufikisha hisia zako kwa mtu fulani ni heri
utumie njia nyingine lakini si
kuweka matusi ya wazi juu.
6.KUWA'TAG' MARAFIKI PICHA CHAFU
Utakuta mtu anamtag rafiki yake,
picha chafu zisizofaa katika ukurasa wake,
hata kama wewe
hakuna watu wa heshima wanaofungua ukurasa wako,
jua kuna wengine wazazi wao wanafungua kurasa zao wanapokutana
na hizo picha unafikiri
wanapata picha gani?
7.KUPOSTI KATIKA UKURASA WAKO STATUS NDEFU KINOMA
Ni heri hata kama unaichukua mahali hiyo status,
jua kuichuja basi kuliko unaposti status kama insha'
unategemea nani anamuda wa kusoma status ndefu hivyo
jali muda wa wenzako.
Ndio maana mwengine kabla haijamliza kujua maana yake analike tu bila kujua maana yake,
eeh!eeh! ushamchosa hivyo.
8.KUTAKA KUCHAT NA MTU KILA UNAPOMUONA HEWANI
Si kila wakati,
mtu anaingia facebook kutaka kuchat na watu, kuna muda,
anakuja kuchati na mtu maalumu,
lakini wewe unalazimisha kuchati
naye kila wakati,
unaandika
tu maujumbe mengi
ukiona hakujibu.
JAMANI HUU NI MTAZAMO,
TU JARIBU KUCHUJA VITU VYA KUFANYA KATIKA UKURASA WAKO NA WA WATU WENGINE.
ILI USIPOTEZE MARAFIKI KWANI RAHA YA MTANDAO WA KIJAMII NI KUWASILIANA NA WATU.
WATU WENGI TUPO KATIKA MKUMBO HUU, TUJIREKEBISHE BASI ILI MAISHA YA FACEBOOK YAWE MAZURI KWA KILA MMOJA WETU.
Subscribe to:
Posts (Atom)




































